Geita: Akutwa amejinyonga ndani ya nyumba ya wageni inayomilikiwa na mumewe

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
KATIKA hali isitokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwananzoka inayomilikiwa na mumewe Siki Mwananzoka.

-----
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa mji mdogo Katoro wilayani Geita mkoani hapa amekutwa amejinyonga kwa kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na mumewe.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Tukio hilo limetokea Februari 3, 2022 saa 12 jioni baada ya mwanamke huyo kufika kwenye nyumba ya wageni na kumtaka mmoja wa wahudumu amsaidie mtoto mwenye umri wa miezi minne kwa kuwa yeye anajisikia vibaya.

Akizungumzia tukio hilo, mhudumu wa nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Monica Paul amesema, mke wa mwajiri wake alifika kwenye eneo hilo saa 8 mchana na kumtaka amsaidie mtoto ili yeye apumzikekwa kuwa hayuko vizuri kiafya.

Amesema baada ya hapo alipewa chumba, lakini baadaye walikuta mwili ukining’inia juu chooni, baada ya mteja mwingine kuomba huduma ya choo alichojinyongea mwanamke huyo.

Kiongozi wa eneo hilo, Stephano Bandola amesema hawajajua chanzo cha mwanamke huyo kujinyonga lakini akadai inaweza kuwa mgogoro wa kifamilia.

Juhudi za kumpata mume wa mwanamke huyo hazikufanikiwa baada ya kuelezwa yuko safarini nje ya Katoro.

MWANANCHI
 
KATIKA hali isitokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwananzoka inayomilikiwa na mumewe Siki Mwananzoka.
Hangayaaaaaaaah aah!
 
Ni kajinyonga au kanyongwa?
 
3B159E3F-B55A-4837-9583-2993B3ABA591.jpeg
 
KATIKA hali isitokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwananzoka inayomilikiwa na mumewe Siki Mwananzoka.
Vifo vimekithiri sijui chanzo ni nini
 
Kajinyonga!!kwani alikuwa na mtoto wa miezi 6, akamuachia dada wa mapokezi, na kumwambia mshike mtoto mimi nikajipumzishe kidogo, cjisikii vizuri!!kumbe chooni kuna ngazi inayotumiwa na mafundi, ndio akapanda juu ya dali na kujitundika!!kisa ni kuwa mme wake alikuwa hampi matunzo ya watoto!!
Duh .. Apumzike kwa amani
 
KATIKA hali isitokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Mwananzoka inayomilikiwa na mumewe Siki Mwananzoka.
Huyu kanyongwa, hakuna Cha kujinyonga hapo. Hizo Ni drama ti
 
Unajinyonga kwa sababu ya maisha magumu?,nani kasema maisha ni rahisi rahisi tu pasipo kupambana?,apumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom