Ajinyonga kisa kukosa nauli ya kwenda ukweni.

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,842
Kijana William Bahati (20) Mkazi wa Kijiji cha Kashero Wilayani Mbogwe Mkoani Geita amefariki Dunia kwa kujinyonga na kamba ya kufungia mbuzi huku sababu zikitajwa kuwa ni kukosekana kwa nauli ya kwenda ukweni kumzika Baba Mkwe wake.

Akiongea kuhusu tukio hilo Mke wa Marehemu, Grace Jeremiah Mkazi wa Kijijini hapo amesema sababu za Mumewe kujinyonga zimetokana na kushindwa kupata nauli ya kwenda ukweni ambako kulikuwa na Msiba wa Mkwewe .

"Mume amejinyonga baada ya kukosa nauli ya kwenda msibani nyumbani kwetu, tulikuwa ndani mida ya saa 11 akawa anasikitika kuwa anaumia kukosa nauli ya kusafiri yeye na Mimi kwenda kumzika Baba, sasa aliamka kitandani akavaa nguo akatoka akasema ngoja niende shambani ndio tukamkuta sasa ameshajinyonga”

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kashero Alfred Msukuzi amesema tukio hilo limetokea October 2 mwaka huu ambapo amekiri kuwa Kijana huyo amejinyonga kwa kukosa pesa ya kwenda ukweni.
#MillardAyoUPDATES
 
Maisha haya ndugu why umejitoa uhai kisa kukosa hela ya nauli? Kwani huo msiba una umuhimu gani kushinda uhai wako? Au alirogwa nini maana si bure huyu mwenzetu
 
Shida sio nauli tu.
Ni kwamba dogo alikuwa na maisha magumu sana. Imefika kiasi cha kukosa hata nauli ya kwenda mazikoni.

Ukute hapo tu wamelala njaa au wanakula chakula hafifu sana
 
Kijana William Bahati (20) Mkazi wa Kijiji cha Kashero Wilayani Mbogwe Mkoani Geita amefariki Dunia kwa kujinyonga na kamba ya kufungia mbuzi huku sababu zikitajwa kuwa ni kukosekana kwa nauli ya kwenda ukweni kumzika Baba Mkwe wake.

Akiongea kuhusu tukio hilo Mke wa Marehemu, Grace Jeremiah Mkazi wa Kijijini hapo amesema sababu za Mumewe kujinyonga zimetokana na kushindwa kupata nauli ya kwenda ukweni ambako kulikuwa na Msiba wa Mkwewe .

"Mume amejinyonga baada ya kukosa nauli ya kwenda msibani nyumbani kwetu, tulikuwa ndani mida ya saa 11 akawa anasikitika kuwa anaumia kukosa nauli ya kusafiri yeye na Mimi kwenda kumzika Baba, sasa aliamka kitandani akavaa nguo akatoka akasema ngoja niende shambani ndio tukamkuta sasa ameshajinyonga”

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kashero Alfred Msukuzi amesema tukio hilo limetokea October 2 mwaka huu ambapo amekiri kuwa Kijana huyo amejinyonga kwa kukosa pesa ya kwenda ukweni.
#MillardAyoUPDATES
Kujinyonga ndo kafika ukweni?!!!!
 
Shida sio nauli tu.
Ni kwamba dogo alikuwa na maisha magumu sana. Imefika kiasi cha kukosa hata nauli ya kwenda mazikoni.

Ukute hapo tu wamelala njaa au wanakula chakula hafifu sana
Maisha yanasikitisha sana, sasa kashajitoa uhai kaacha familia utaishije na pengine labda ndio alikuwa tegemeo lao itakuwaje sasa
 
Kijana William Bahati (20) Mkazi wa Kijiji cha Kashero Wilayani Mbogwe Mkoani Geita amefariki Dunia kwa kujinyonga na kamba ya kufungia mbuzi huku sababu zikitajwa kuwa ni kukosekana kwa nauli ya kwenda ukweni kumzika Baba Mkwe wake.

Akiongea kuhusu tukio hilo Mke wa Marehemu, Grace Jeremiah Mkazi wa Kijijini hapo amesema sababu za Mumewe kujinyonga zimetokana na kushindwa kupata nauli ya kwenda ukweni ambako kulikuwa na Msiba wa Mkwewe .

"Mume amejinyonga baada ya kukosa nauli ya kwenda msibani nyumbani kwetu, tulikuwa ndani mida ya saa 11 akawa anasikitika kuwa anaumia kukosa nauli ya kusafiri yeye na Mimi kwenda kumzika Baba, sasa aliamka kitandani akavaa nguo akatoka akasema ngoja niende shambani ndio tukamkuta sasa ameshajinyonga”

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kashero Alfred Msukuzi amesema tukio hilo limetokea October 2 mwaka huu ambapo amekiri kuwa Kijana huyo amejinyonga kwa kukosa pesa ya kwenda ukweni.
#MillardAyoUPDATES
Umaskini wa akili na hela, so sad.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom