Mtwara: Akutwa amejinyonga jirani na nyumba ya mkewe

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linafanya uchunguzi wa tukio la mwanaume mmoja kujinyonga katika kijiji cha Majengo kata ya Ziwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Mwanaume huyo amekutwa amejinyonga jirani ya nyumba ya mkewe ambaye walikorofishana.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Februari 19,2024, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP-Mtaki Kurwijila amesema mwili ulikutwa jana Jumapili Februari 18, 2024 saa 12 asubuhi ukining’inia kwenye mti wa mkorosho.

Amesema kwa mujibu wa mkewe, mumewe alitoka nyumbani kwake Februari 12 na kwenda kusikojulikana baada ya kutoelewana.
 
Kila siku tunasema, mapenzi yakiisha achaneni kwa amani hamsikii.
Unakufa juu ya mtu ambaye hakupendi tena ili iweje?

Ugomvi, kutokuelewana ni kawaida, ila vikizidi ni hatari kwa afya ya akili. Ndio mambo kama haya.
Wakati mwingine mtu anashindwa ku-control akili na hisia zake. Nikuchekeshe. Kuna dada mmoja jirani aligombana na mumewe na akatishia kujiua. Ni vizuri kwanza kujua kuwa huyo dada alikuwa mtu wa hasira za haraka haraka kweli. Basi hiyo siku tukasikia kelele. Kwenda tukakuta dada wa watu amekaa kwenye kochi, amejiniga kwa mikono yote miwili shingoni eti anajinyonga.
 
Back
Top Bottom