Gazeti letu la Udaku JF..

Gazeti letu la Udaku JF..

Khaaa, hivi kumbe bado sijakutambulisha eeh? Nilifikiri shemeji langu uporoto amekupa taarifa! Sorry swahiba sijachelewa sana. Tunatarajia kufunga ndoa kwenye mkesha wa x'mass. Naimani mtakubali kuwa wasimamizi wetu wewe na uporoto! Ukiona mtu anammendea nistue nije na viwembe!

heheeh hawajui kuwa hili gazeti la udaku wengine limetusaidia kupata mchumba. Honey! jana nimekuona kivuli chako kwenye povu la shampoo bafuni.
 
umeniona eeh! mzembe nina manyota mpaka kwenye zipu za suruali. Leo nikirudi tutapiga kiduku kwa style ya "kuvamia bengazi" (huu si udaku ni kweli)
Hahaha.... Jamani darling umeanza kuntengua mbavu mwenzio, staili ya kuvamia bengazi ndio ipi tena?...lol.
 
heheeh hawajui kuwa hili gazeti la udaku wengine limetusaidia kupata mchumba. Honey! jana nimekuona kivuli chako kwenye povu la shampoo bafuni.
Tehe, tehe, tehe!.. Hawajui, waache waendelee kukodoa macho kwenye gazeti la udaku, wenzao tupo stage two... Lidumu milele penzi letu...
 
Khaaa, hivi kumbe bado sijakutambulisha eeh? Nilifikiri shemeji langu uporoto amekupa taarifa! Sorry swahiba sijachelewa sana. Tunatarajia kufunga ndoa kwenye mkesha wa x'mass. Naimani mtakubali kuwa wasimamizi wetu wewe na uporoto! Ukiona mtu anammendea nistue nije na viwembe!

poa swahiba, ngoja nianze kutengeneza apitaiti. Shemeji nitakulindia, mi pia natembea na viwembe. Uwezo wa kununua bunduki hatuna, hata viwembe tukose!
 
ukitaka kujui jinsia yangu si uangalie avatar yangu hapo..!?
udaku ni habari ambazo hazijasibitishwa rasmi, nikiangalia hapo itakuwa sio udaku tena. Lol. Naomba unipe udaku mpya wa klorokwini.
 
superman na husninyo wazua varangati bar...ni baada ya superman kujidai predeshee na kumpeleka husninyo bar kumbe jamaa hela zenyewe chenji za madafu..matokeo yake husninyo kaagiza vitu vya bei mbaya na kuingia mitini kinyemela..jamaa kushtuka bili yaja laki 6..yasemekana superman alikuwa na buku 9 tu mfukoni..ndipo mabaunsa wa bar hiyo walipoanza kumla mande ....

Duuh Mkuu hii ni noma sasa! Unanikumbusha Fleva ya bongo ya Starehe Gharama!
 
TF niaje Kamanda?

Nikisoma hivi vichwa vya habari vya kubuni naona hujakaaa vizuri. Ni salamaaa au Vifuu Tundu tu?
Kamanda salama kabisa...dah watu wameniandama na skendo kibao kweli hii sredi itabidi nipeleke polisi waandishi wote wa udaku...
 
Ujauzito wa Dena Amsi mashakani:

Yule mwanadada anaesifika hapa jamvini kwa kurekebisha lugha ya kiswahili leo amekimbizwa hospitali kwa kile kinachofunuliwa kuwa kilitokana na kichefu chefu cha mimba, swahiba wa karibu wa mdada huyo anaekwenda kwa jina la Wiselady amefunuka kuliambia gazeti hili kuwa Dena Amsi alishikwa na kichefu chefu na kizungu zungu na akavuta chupa aliyozani ilikuwa na juisi ya ukwaju bila kujua kumbe ilikuwa chupa ya detol. Habari kamili UK wa 5

Ha ha ha ha mweeehhh

Mie hizi siziwezi nasoma na kucheka tu kha??
 
inasemekana bishanga ndio member mwanaume anaeongoza kwa kukaribisha members wanawake kwa njia ya pm. Katavi ni katibu wa bishanga katika hiyo biashara ya kukaribisha wageni.
halafu wewe Husn wewe usitake kuniharibia ndoa,hivi niko kitandani na Eliza wa tegeta tunasoma post zako,shauri lako atakwendea pemba.
 
Jibaba hili sredi kitaa dah...watu wote wananiandama kweli kudadekii lazima nimlie timing TANMO nimng'oe masaburi..lol

hehe ibuka na ID mpya jibaba, mimi majuzi niliingia na ID flani mpya na nikatoka na album ya natafta waifu, nilishangaa wadada kibao maselebriti wa JF walileta ma CV yao tena kwa mapoz.
JF bana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom