Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Gavana Prof. Ndulu: Benki wapo sahihi

Tozo (fees/charges) wanazotoza benki kama vile makato ya kila mwezi, ATM withdraw fees, nk zinalipwa na mtumiaji wa huduma za benki (mteja wa benk). Serikali inachosema ni kuwa hizo fees kwa sasa zitakuwa na VAT (inclusive VAT) yaani ndani yake kutakuwa na 18% ya serikali.
Mfano: Kama gharama ya kutoa fedha kwenye ATM ni shs 1,000 fedha yote hii ilikuwa inachukuliwa na benki. Kwa utaratibu mpya ni kuwa fedha hiyo sasa benki watailipa serikali 18%, yaani benk watachukua shs 847 na Serikali watachukua shs 153 kama kodi ya ongezeko la thamani, VAT. Utaona kuwa gharama kwa mtumiaji wa benki inaendelea kuwa ile ile shs 1,000.
Utaratibu huu benki hawataki kwa sababu utapunguza mapato yao ya hizo tozo kwa 18%. Benki wanachotaka ni kuwa waongeze 18% kwenye tozo wanazotoza saa hivi, yaani kwenye 1000 waongeze 18% na kuwa sh 1180 na hivyo kusukuma hilo ongezeko kwa mtumiaji wa mwisho wa huduma za benki kwa ongezeko la gharama za huduma za benki.
Mpaka sasa benk wanawatoza wateja wao gharama kubwa na wanachokirudisha kwa wateja wao kama riba ni kidogo sana, riba ya mkopo wa benki ni kati ya 20% hadi 25% kwa mwaka lakini ukiweka fedha zako benki utapata riba ya kati ya 2% na 6%, bado hizo fedha wanazifanyia biashara na kupata faida kubwa. Utaona kuwa hata hizo fees hazikupaswa kuwepo na kama zinapaswa kuwepo zinatakiwa ziwe kidogo sana.
Benki zetu haziko tayari kuwasaidia wateja wao kujikwamua na hali ngumu ya maisha badala yake wamekuwa zikandamiza wateja wako. Nashangaa hata huyo Prof wa BOT anawasapoti ili hiyo 18% iende kwa watumiaji wa mwisho (wateja wa benk).
Tukumbuke serikali imeweka kodi, 18% kwenye fees ambazo benki tayari walikuwa wanazikusanya lakini walikuwa hawazilipii kodi.
 
Gazeti la Mwananchi: Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk, BOT imesema mabenki yapo sawa!

Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.

Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA

View attachment 362128

TRA jana na waandishi wa habari walipinga ongezeko hilo la gharama za kifedha kwa wananchi iliyofanywa na mabenki wakisema ni upotoshaji na kutaka BOT iwashughulikie

Beno yupo sahihi maana anayestahili kulipa kodi ya ongezeko la dhamani ni mlaji wa mwisho. Muuzaji ni wakala wa TRA wapo kukusanya hizo fedha. Nadhani Serikali haijajipanga kabisa.
 
kitendo cha ile kodi kuiita VAT,Basi mzigo unaenda moja kwa moja kwa mlaji.Labda ibadilishwe jina na isiwe VAT.Profesa yuko sahihi.TATIZO HII NCHI KWA SASA MAAMUZI YA TULIOWAPA DHAMANA YANATOLEWA KWA HOFU YA KUTUMBULIWA.
Ni kweli kabisa kwa haya unenayo
 
Hahahahaa. Mnawachanganya team lumumba
.... Sasa watasapoti prof. au tra maana yote ni matawi yao
 
Hapa ilitakiwa serkall iseme makato yanayofanywa na benki ni makubwa

Mfano kama ni tshs 1000
Basi kuanzia julaii makato yabaki ni 1000 na katika hiyo 750 iende bank na 250 iwe kusanyo la kodi.

Hapo bado anayelipa kodi bado ataendelea kuwa mlaji na faida kubwa ambayo benk ingepata itapungua
Sa faida ya benki ikipungua na corporate tax si itapungua
 
Mkuu acha wajae hofu ili mali zetu zipone
Maana yangu hapo ni kwamba kila mkuu wa idara anajitokeza katika vyombo vya habari ili aonekane kwa mkulu anafanya kazi asije akatumbuliwa. Hakuna weledi.
 
cc.jingalao
maana jana ulileta uzi hapa kuwa mabenki yashitakiwe kwa uhaini.tuambie sasa kati ya TRA na Benki Kuu nani wanapaswa kushitakiwa kwa uhaini.
 
BOT wako sahihi pia BOTinatakiwa ijitegemee kimaamuzi TRA na waziri wa fedha wao walifikiria kukusanya mapato tu ila walikosa knowledge ya uhasibu
 
Swali la msingi ni Je wizara husika walipopitisha kodi hii waliwashirikisha BOT,TRA na wahusika wengine kama watendaji wa juu wa Benki zilizopo Tanzania ili kufikikia makubaliano ya utekelezaji wa makusanyo haya?

Inashangaza kuona mamlaka mbili zilizopo chini ya serikali moja kutoa matamko tofauti kwenye swala moja linalowagusa/kuwaunganisha wakati utekelezaji wa maamuzi ya serikali umeshaanza na unawagusa wananchi moja kwa moja.

Kwa nini gavana wa BOT ama mabenki hawakutuonya/kutoa tamko kabla ya makusanyo hayo kuanza? Au hawakushirikishwa katika hatua za awali za uundaji wa utaratibu huu mpya wa ukusanyaji kodi na hivyo hawakuwa na namna ya kuzuia mfumo huo zaidi ya kukubaliana nao na kuhamishia gharama kwa mteja.

Either way hii haijakaa vizuri kwa serikali maana wananchi ndio wanaachwa katikati hawajui washike tamko la nani, cha msingi ni kujiandaa kisaikolojia kwa lolote sitashangaa nikisikia benki zilizopandisha tozo kufungiwa ama kunyang'anywa leseni maana lolote linaweza kutokea kutokana na maamuzi ya viongozi wetu ambayo hayajaona/hayajatambua madhara kamili ya utekelezaji wake.
utekelezaji umeenza baadhi ya benki zimewataarifu wateja juu ya VAT mi mwenyewe nimestushwa kuona tasisi kubwa sana za baba moja serikali zikitofautiana juu ya VAT walikuwa wapi kufafanua kabla ya kupitishwa bungeni.au ni hofu ndo wanaogopa kutumbuliwa.ni heri ukatumbuliwa ukiwa unasimamia ukweli kuliko kunyamaza na kusubiri matokeo hasi ndo utoke kufafanua kweli inakuweka huru inakulinda sijui watamuaje maana huduma za benki zitakuwa garama kwa wateja na watu watakwepa kutumia benk
 
Siku zote kodi yoyote mlaji(consumer) ndio mlipaji namshangaa Kadata anaposema benki ndio zitalipa wao benki hizo hela watazitoa wapi? ni lazima wazikusanye toka kwa mlaji wa mwisho
 
Tozo (fees/charges) wanazotoza benki kama vile makato ya kila mwezi, ATM withdraw fees, nk zinalipwa na mtumiaji wa huduma za benki (mteja wa benk). Serikali inachosema ni kuwa hizo fees kwa sasa zitakuwa na VAT (inclusive VAT) yaani ndani yake kutakuwa na 18% ya serikali.
Mfano: Kama gharama ya kutoa fedha kwenye ATM ni shs 1,000 fedha yote hii ilikuwa inachukuliwa na benki. Kwa utaratibu mpya ni kuwa fedha hiyo sasa benki watailipa serikali 18%, yaani benk watachukua shs 847 na Serikali watachukua shs 153 kama kodi ya ongezeko la thamani, VAT. Utaona kuwa gharama kwa mtumiaji wa benki inaendelea kuwa ile ile shs 1,000.
Utaratibu huu benki hawataki kwa sababu utapunguza mapato yao ya hizo tozo kwa 18%. Benki wanachotaka ni kuwa waongeze 18% kwenye tozo wanazotoza saa hivi, yaani kwenye 1000 waongeze 18% na kuwa sh 1180 na hivyo kusukuma hilo ongezeko kwa mtumiaji wa mwisho wa huduma za benki kwa ongezeko la gharama za huduma za benki.
Mpaka sasa benk wanawatoza wateja wao gharama kubwa na wanachokirudisha kwa wateja wao kama riba ni kidogo sana, riba ya mkopo wa benki ni kati ya 20% hadi 25% kwa mwaka lakini ukiweka fedha zako benki utapata riba ya kati ya 2% na 6%, bado hizo fedha wanazifanyia biashara na kupata faida kubwa. Utaona kuwa hata hizo fees hazikupaswa kuwepo na kama zinapaswa kuwepo zinatakiwa ziwe kidogo sana.
Benki zetu haziko tayari kuwasaidia wateja wao kujikwamua na hali ngumu ya maisha badala yake wamekuwa zikandamiza wateja wako. Nashangaa hata huyo Prof wa BOT anawasapoti ili hiyo 18% iende kwa watumiaji wa mwisho (wateja wa benk).
Tukumbuke serikali imeweka kodi, 18% kwenye fees ambazo benki tayari walikuwa wanazikusanya lakini walikuwa hawazilipii kodi.
Duuuu......mpaka watu waelewe hii kitu Kazi ipo...ila hapa shida inakuja pale unapoingiza siasa kwenye ishu za kitaalamu...umeeleza weeeee...ila ukweli utabaki pale pale...
 
Tozo (fees/charges) wanazotoza benki kama vile makato ya kila mwezi, ATM withdraw fees, nk zinalipwa na mtumiaji wa huduma za benki (mteja wa benk). Serikali inachosema ni kuwa hizo fees kwa sasa zitakuwa na VAT (inclusive VAT) yaani ndani yake kutakuwa na 18% ya serikali.
Mfano: Kama gharama ya kutoa fedha kwenye ATM ni shs 1,000 fedha yote hii ilikuwa inachukuliwa na benki. Kwa utaratibu mpya ni kuwa fedha hiyo sasa benki watailipa serikali 18%, yaani benk watachukua shs 847 na Serikali watachukua shs 153 kama kodi ya ongezeko la thamani, VAT. Utaona kuwa gharama kwa mtumiaji wa benki inaendelea kuwa ile ile shs 1,000.
Utaratibu huu benki hawataki kwa sababu utapunguza mapato yao ya hizo tozo kwa 18%. Benki wanachotaka ni kuwa waongeze 18% kwenye tozo wanazotoza saa hivi, yaani kwenye 1000 waongeze 18% na kuwa sh 1180 na hivyo kusukuma hilo ongezeko kwa mtumiaji wa mwisho wa huduma za benki kwa ongezeko la gharama za huduma za benki.
Mpaka sasa benk wanawatoza wateja wao gharama kubwa na wanachokirudisha kwa wateja wao kama riba ni kidogo sana, riba ya mkopo wa benki ni kati ya 20% hadi 25% kwa mwaka lakini ukiweka fedha zako benki utapata riba ya kati ya 2% na 6%, bado hizo fedha wanazifanyia biashara na kupata faida kubwa. Utaona kuwa hata hizo fees hazikupaswa kuwepo na kama zinapaswa kuwepo zinatakiwa ziwe kidogo sana.
Benki zetu haziko tayari kuwasaidia wateja wao kujikwamua na hali ngumu ya maisha badala yake wamekuwa zikandamiza wateja wako. Nashangaa hata huyo Prof wa BOT anawasapoti ili hiyo 18% iende kwa watumiaji wa mwisho (wateja wa benk).
Tukumbuke serikali imeweka kodi, 18% kwenye fees ambazo benki tayari walikuwa wanazikusanya lakini walikuwa hawazilipii kodi.

Mkuu ukishaintroduce VAT kwenye bidhaa/huduma ambayo ilikua haina VAT..uamuzi wa kama bei iwe VAT inclusive au VAT iongezwe kwenye bei ya awali ni wa mfanyabiashara/mto huduma. Yani yeye ndio wakuamua apunguze faida yake ili kuabsorb hiyo VAT na kumpunguzia makali mteja..au amtwishe mzigo...ila sheria inamruhusu kumtwisha mzigo mteja. Unless biashara iwe kwenye regulated sector. Kwa mfano kama serikali ingeamua kuleta VAT kwenye mafuta..ewura ndio angekua na mamlaka ya kuamua kama vat iongezwe au bei ya sasa iwe vat inclusive. Lakini sekta ya benki haipo regulated..wanajiamulia bei zao.
 
kibaya zaidi wanajichanganya changanya,Mpango anaiita excise duty,TRA wanaiita VAT lakini mzigo mnamdondokea Taasisi ya Fedha(Kituko hiki) na BOT nao wanasema hii mzigo unaenda kwa mlaji(final consumer)..Yaan ''vurugu mechi''...
Dr mpango kashtuka amejichanga,sasa amebadili gear angani
 
Bank Charges Haziepukiki,ziwe na kodi ndani yake ama zisiwe na kodi ndani yake.Kumbuka Zile ni sehemu ya gharama unazotozwa kwa huduma unazopata za kibenki.Sasa kama Serikali yako haikuwa inatoza chochote kwenye charge hizo si kosa la Benki ama jukumu la benki kuiambia Serikali iwacharge.Na vyovyote vile,Tozo hiyo ikiitwa VAT basi automatically jukumu linakuwa kwa mlaji,na hata iwe excise duty nyingine,Mabenki yatatafuta namna ya kuongeza mzigo kwa wateja kwa kigezo cha kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Kazi sana, mm ni mteja wa benj ya ughaibuni WESTPAC sijawah katwa nikitoa pesa, kutuma pesa wala nini kwa acc yangu ya savings. Tz why wasiige huo mfano, kuangalia salio tu unakatwa..unakatwa..unakatwa
 
Huyo prof nae ni msanii, hatuambie kwanza hizo huduma na hayo makato ni VAT inclusive au la?, na kama yalikuwa vat inclussive wao walipaswa kupeleka makato ya VAT huko TRA,kama walikuwa hawapeleki sasa wanapaswa kupeleka hayo makato na sio kutuongezea mzigo
 
Naona umejitahidi kuchangia lkn I hope uelewi unachoandika kama unao ufahamu wa kutosha on how these things are operating
Value-Added Tax (VAT) is a tax on consumer spending. It is collected by VAT-registered traders on their supplies of goods and services effected within the State, for consideration, to their customers.kwishaaaa!!!!
C&P
 
Nimefuatilia kwa makini michango ya mabingwa humu na nimejiridhisha pasi na shaka kwamba KOSA NAMBA MOJA lililofanywa na Serikali na Bunge ni jina la kodi yenyewe yaani VAT. Hii inaonesha jinsi mihimili hii hususan ule wa Bunge ulivyokosa japo weledi wa kurekebisha kosa la kijinga kama hili.

This is a proof beyond reasonable doubt kwamba Bunge letu haliko makini na mambo hufanywa kwa mtindo wa bora liende as long as limeletwa na Serikali hakuna wa kuhoji kwa umakini au kukosoa bila woga. Hii sio kuisaidia Serikali au nchi bali ni hujuma ya wazi.
 
Back
Top Bottom