magafumukama
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 743
- 198
Mambo NDINDINDI hapo ndo tutajua Tundu ni mwanasheria au mhalifu. Nilimsikiliza sana Bwana TRA nikajiuliza hii ni nini? Sijapata jibu
Nakubaliana na wewe mkuu, TRA hoja yao ni kwamba benki zinatakiwa kulipa serikali 18 % ya charges wanazotukata, yeye anakuja na habari tofauti kwamba benki ni wakusanyaji tuu wa hiyo 18 %.Huyu gavana hana msaada wowote nchini.ydio maana BOT ina mauzauza kibao..atoke tu hizi nyakati zimemzidi uwezo.
Ina maana kipindi inaandaliwa hiyo sheria BOT na wadau wengine wa maswala ya fedha na kodi hawakushirikishwa?
Mlizoea kona kona sasa zimebanwa ...mlikuwa mnawakamua wananchi tu halafu mrejesho kwa serikali hakuna...
mlikuwa mnakopesha serikali fedha yake sasa hakuna...
kibaya zaidi wanajichanganya changanya,Mpango anaiita excise duty,TRA wanaiita VAT lakini mzigo mnamdondokea Taasisi ya Fedha(Kituko hiki) na BOT nao wanasema hii mzigo unaenda kwa mlaji(final consumer)..Yaan ''vurugu mechi''...Naungana na Tyta kosa la kwanza ni kuita hilo tozo VAT, hapo ndio mzizi wa fitna unapoanzia. TRA nao wanasemaje mabenki hayalipi kodi wakati wakiweka taarifa zao za kifedha kuna kua na before tax au after tax? Sasa kama hizo charges ni sehem ya hiyo faida, si ndio unakua imejumuishwa kwenye income tax zinazolipwa na mabenki? Any way, vyovyote itakavyokua, mwananchi ndio akataeumia.
Mkuu usiseme siyo makato mapya,ni makato mapya kwa sababu awali yalikuwa hayakatwi. Benki zinafanya biashara ni lazima ziongeze tozo kufidia hiyo kodi itakayotozwa na serikali. Vat inalipwa na mteja,benki zinakusanya kwa niaba ya tra. Prof.ndullu yupo sahihi sana!!Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee
Gazeti la Mwananchi: Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk, BOT imesema mabenki yapo sawa!
Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.
Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA
View attachment 362128
Hii vita tamu kwel, mwanasiasa tra vs Msomi Bot tamu kwel.... acha wararuane tuone huu uchumiGazeti la Mwananchi: Wakati TRA ikiitaka BOT izichukulie hatua bank zilizotangaza kuongeza gharama za huduma za kibenk, BOT imesema mabenki yapo sawa!
Prof.Ndulu anasema mabenk watakuwa mawakala wa TRA tu katika kukusanya VAT lakini si walipaji,kwa hiyo hawezi kuwachukulia hatua.
Beno Ndulu ametolea mfano unapokua unauza duka unakuwa wakala tu wa TRA na sio mlipaji.....KUMEKUCHA
View attachment 362128
VAT (value added tax) ukisoma uchumi huo ni mzigo wa final consumer.Huyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee
Hahahaa...mkuu hii mada imewachanganya watu mpaka inakua ngumu kutambua ambae haelewi ni yupi na ambaye anaongea sarcastically ni yupi
Mkuu me mwenyewe sijawai hata kusoma hayo masomo siju accounts..sijui bookkeeping...sijui commerce ila nimemuelewa vzuri Kabisa....Na nilishabishana sana Na watu kuhusu hii kitu kuwa mzigo utakuwa kwa mlaji wa Mwisho ila baadhi ya watu hawaelewi Kabisa mkuu...ni ishu ndogo sana ila kama ulivosema kama mtu alienda shule kimkumbo hawezi kuelewa Kabisa alichosema Gavana..Ni watu wachache sana wanaoweza kujua prof kazungumzia nini huwezi kumuelewa kama ulienda shule kwa ushabiki
Kama kamishna ameshindwa kuelezea VAT pamoja na waziri wake wa fedha, kweli wataweza complex terms za uchumi wa viwanda?
Nchi nyingine kwa sasa kamishna angekua amefukuzwa kazi.
Kamishna anaposhindwa kuelezea VAT kwa sababu za kisiasa, anatoa picha gani kwa muekezaji, kwamba TRA will interpret the tax law however it wants -- in a populist manner -- and you shall pay.
Body language yake inaonyesha haamini anachokiongea.
Mkuu unavijua vyanzo vya mapato kwenye bank??Zamani walikuwa hawatozwi na walikuwa wanatukata.. Basi wangeacha kukata.. Au wanataka walipe na zile zote za nyum?
Wewe ndo hujui,walikuwa wanakusanya wapi wakati hii kodi kwenye miamala ya fedha na imeanza Jana,ccm imekuharibu ubongo mpaka hujielewi,usikute mtu mwenye unae tusumbua umeishia darasa la piliHuyo prof naye hajui. TRA wamesema mabenki yalikuwa yakusanya bila kulipa. Sio new makato. Mwee
BOT iko chini ya nani?
Halafu cha kushangaza zaidi...waziri wa fedha safari hajateuliwa tu mwanasiasa..ameopolewa mtu ambaye tulitegemea ni mbobezi kutoka TRA..akapewa ubunge na uwaziri. Sasa kama ubobezi wenyewe ndio huu...kwakweli nchi hii hatuna msalia mtume.