Mshamba wa Kijijini
Member
- Oct 5, 2007
- 74
- 1
Mbona haina Muhuri?
Mbona haina Muhuri?
katika anuani ya gavana katika hii barua kuna kitu hii
Cable:41024 "BENKUU"
what is "BENKUU" ? does it mean "BENKIKUU"?. I'am a little bit suspicious.
Zakia Meghji. Waziri wa fedha atoa taarifa kuwa wizara yake haina taarifa juu ya kujiuzulu kwa Gavana.
Zakia Meghji. Waziri wa fedha atoa taarifa kuwa wizara yake haina taarifa juu ya kujiuzulu kwa Gavana.
Kithuku, you have a point there.
Hiyo barua imechapwa katika stationary yenye heading ya BOT. Ukifikiria pia kuwa Balali wakati akienda Boston kwa 'check-up' hakujua kuwa itabidi ajiuzulu katika mazingira haya, hivyo si rahisi kuwa alienda na stationary za BOT.
Kwa hiyo mtazamo mzuri ni kuwa hiyo barua ilitayarishwa na kuchapwa Dar halafu akapelekewa huko Boston na kuambiwa ai-sign, mtu akaondoka nayo au ikatumwa kurudi Bongo. Kwa kufanya hivyo inaongeza pia uwezekano wa ku-leak, which is what happened.
Tatizo ni kuwa barua hii ilikuwa imetumwa Ikulu; sasa mjanja mmoja akaamua kuilikisha kwa waandishi kabla haijafika Ikulu/haijatangazwa rasmi. Na binafsi kitu kimoja kinachoweza kutokea na msishangae ni kuwa Rais akiamua kukataa kujiuzulu kwa Balali kuwakomoa wale waliolikisha barua hii. Hata hivyo kuna jambo jingine hapa kuhusu mama Meghji, Balali hayuko chini ya Meghji (at least not directly) ndiyo maana barua imeelekezwa kwa Rais na ni jukumu la Ikulu kuvitangazia vyombo vyake kuwa Balali amejiuzulu.