Jamani jamani mwogopeni Mungu kidogo na muwe na huruma ya kulinda shahidi wa taifa badala ya kumshutumu.
Kutoka mitaani, kuna ushahidi mkubwa kuwa Dr. Balali kakimbia Bongo kwa usalama wa maisha yake baada ya kuombwa na baadhi ya watu waliokuwa karibu naye hasa navyosikia baada ya yeye kutoa madai kama ya dada yetu marehemu AC kuwa yupo tayari kuyataja majina ya viongozi waliohusika.
Kwa hiyo twende taratibu na swala hili na kama kweli kuna uwezekano Dr. Bilali ahojiwe akiwa huko aliko na sio kuvuta hasira zetu ovyo.
Dr. Balali ni wanted na Mafia ya Bongo na kumtakia mabaya yeye ni kupoteza kabisa uwezekano wa kufahamu kilichotokea benki kuu.
Katibu Tarafa,
Ukisha kuwa ndani ya mafia hilo neno angekwisha Sema... halipo kabisa kuna code of silence kule na msemaji yeyote huitwa panya hukumu yake ni kifo hata kama ni baba yako mzazi.... Dr.Balali ni msomi anayajua haya na Mafia ya Bongo isikie tu mjomba ktk bomba, hawakosei kabisa. Wameondolewa makomandoo itakuwa mchovu Balali.
Kwa usalama gani tuliokuwa nao ambao unaweza kumlinda kabla na baada!.
Kama hasemi watu watakuwa sawa kumjumuisha katika mafisadi.Kama gavana mwenye integrity, hata kama wangemuwekea bunduki kichwani alitakiwa kuukataa ufisadi (si ndiyo kutetea interest za taifa kwa uwezo wako wote huko?). Sasa hii biashara ya kufanya deal, halafu ukishtukiwa mambo ya "Sorry, we gofed" haifai.Vipi kama dili lisingeshtukiwa? angejiuzulu hata kujiuzulu sembuse kusema?
Sasa hivi it is too late hata kama akisema mi nitamuona mzushi tu anataka kutetea legacy yake.Wakati wa kusema ulikuwa mwanzo wakati mafisadi wanafanya vitu vyao.
Mkuu Jasusi,
Heshima mbele, nakumbuka kule nyuma ulimwambia Masanja, kuwa when the time is right ukweli utajitokeza na kumsafisha gavana, na mimi siku zote nilisema kwamba lets give it a time kujua ukweli wote kabla ya kumhukumu gavana, nakumbuka Mwafrika wa Kike alivyonitwanga, lakini nika-maintain kuwa gavana apewe time, now here comes this news za yeye kujiuzulu kama ilivyotabiriwa, tena akiwa nje ya nchi!
Sina wasi wasi na ukweli wa barua ya Mzee MMJ, kwa sababu najua ameipata wapi, mkuu kwa kweli ninasubiri what you have to say na this topic kwa ujumla!
Jamani jamani mwogopeni Mungu kidogo na muwe na huruma ya kulinda shahidi wa taifa badala ya kumshutumu.
Kutoka mitaani, kuna ushahidi mkubwa kuwa Dr. Balali kakimbia Bongo kwa usalama wa maisha yake baada ya kuombwa na baadhi ya watu waliokuwa karibu naye hasa navyosikia baada ya yeye kutoa madai kama ya dada yetu marehemu AC kuwa yupo tayari kuyataja majina ya viongozi waliohusika.
Kwa hiyo twende taratibu na swala hili na kama kweli kuna uwezekano Dr. Bilali ahojiwe akiwa huko aliko na sio kuvuta hasira zetu ovyo.
Dr. Balali ni wanted na Mafia ya Bongo na kumtakia mabaya yeye ni kupoteza kabisa uwezekano wa kufahamu kilichotokea benki kuu.
Mkandara,
Hakuna lolote, huyu Balali anahusika na ndio maana kakimbia nchi na kujificha huko bila kutamka hata neno moja.
Yeye yuko nje ya nchi, anaogopa nini kusema?
Inabidi ifike mahali tuachane kabisa na mambo ya kuwatetea hawa wanaotuibia.
Yeye kama ana ushahidi aseme wazi, ameogopa kusema akiwa TZ, sasa anaogopa kusema akiwa USA?
Hakuna jipya hapo, jamaa alikuwa anajua, alikuwa mshiriki, sasa
wenzake wanaanza kumruka, yeye anabwabwaja huko aliko?
Mbona hata hospitali alikolazwa hataki kusema? Tulijua Nyerere kalazwa wapi ndio awe fisadi Balali?
Balali asikubali kufa na hizo siri, sasa yuko shimoni, ni bora atoke clean kwa kusema yote.
Mwafrika wa kike said:Mkulu FMES,
Heshima mbele mkuu, nimekuwa alerted na system kuwa unataka nikupe jibu la niliyosema hapa last time. Sitakuwa na muda mwingi sana wa kujibu maana matumizi ya internet nilipo sasa hivi yako very limited. Mengine zaidi nitajaribu kukujibu jumatatu au baada ya krismams.
Nilikubaliana nawe kuwa Balali anaweza kuwa na pesa zake za kutoka na ajira yake ya WB. Nilipingana nawe kuwa, mshahara wa Balali wa WB hautoshi kumfanya jamaa amiliki majumba kibao na biashara kibao anazomiliki ndani na nje ya nchi. Document zipo na achive yangu na ya Mzee Mwanakijiji inazidi kupokea nyingi zaidi.
Balali sasa hivi ni bilionea ile mbaya, swali je hizi pesa zote ametoa wapi? Unajua kwa nini Balali ameshindwa kufanya alichofanya yule Githongo wa Kenya?
Inawezekana Balali hakupata mgawo mkubwa kwenye skendo ya Meremeta na zingine zilizomweka Kikwete madarakani ila naye ana skendo zake kibao tu ambazo kama akiwasema kina Kikwete basi RO na vijana wa usalama watamwaga file la Balali (wameanza kumwaga sasa hivi ndio maana watu kama sisi tunapata vitu kibao vya balali) ili naye apoteze.
Balali sio safi, anahusika moja kwa moja na ule wizi wa BOT kama Dr Slaa alivyosema kwenye report yake. Kama angekuwa safi angekataa (kumbuka Rutihinda na Kibona) au angefanya chochote kuwazuia Kikwete na the company wasichote mabilioni na kutumia kwenye uchaguzi.
Alternative nyingine aliyonayo ingekuwa ni kufika tu marekani na kuwapigia simu waandishi wa washington post au 60 minutes (ambao so far wanaaminika kwa kutunza siri) ili aseme story yake na baada ya hapo hata mafia hao wa bongo wangeogopa kummaliza.
Mimi na memba fulani hapa JF tumemtafuta Balali tuongee naye na ikiwezekana tumuunganishe na waandishi wa habari hapa US lakini jamaa hataki na anaogopa kila mtanzania aliyeko marekani. Kuna mawili hapa, Balali ni mwizi na anaogopa kuwataja wezi wenzake au Balali anaogopa kila mtu wakiwemo waaandishi wa habari.
So far, hakuna uthibitisho wowote ambao barua yake ya kujiuzulu itaonyesha kuwa Balali ni msafi, labda kama unao mkuu uuutoe..
Otherwise uwe na sikukuu njema na mwaka mpya wenye mafanikio..
Samahani kama sitajibu haraka hoja zako niko mbali sana na ulimwengu wa fast life ya marekani sasa hivi!
Pundit,
Kuna nchi za kufanya hayo siyo Tanzania. Leo AC yuko wapi na amefanikisha kitu gani hata kama report ipo kwa mkulu. Watu kwa uzalendo wenu mlidai zaidi ayaseme kwa wanahabari. Dr. Balali is smart than that, kwani akisema ama asiposema results ni sawa, lakini kaokoa uhai wake na familia yake.
Kumbuka msemo wangu hapo juu, hukumu ya wanancchi haitamwacha nje bora mbakie mkikisia hivyo hadi siku sisi wote tutakapo weza kujenga uzalendo wa namna hiyo na kusimama kuweka vifua vyetu mbele kuwatetea watu wanaojaribu kutukomboa.
Mtanzania,
Akisema then what?...
Unajua uswahilini mtu yeyote anayejaribu kuvunja ndoa huitwa mnafiki!... kwa serikali na utawala wa CCM huu utaitwa unafiki...
kwa hiyo angesema akiwa Bongo angekuwa mnafiki na akisema akiwa USA bado ni mnafiki kwa sababu ndoa haitavunjika na tutaanza kuhoji kwa nini aseme leo baada ya..