Wasalaam
Nilipata nafasi ya kusafiri na abiria wangu,tumepumzika kituo cha kwanza nataka kuwasha gari tuendelee na safari kukidhi ombi la abiria wangu...gari ikagoma[emoji20]
Tukagusanisha nyaya zote wapi hata cheche hamna
Hali hii iliniacha kwebye fedheha na simanzi, japo abiria wangu aliomba kushuka huku akijitahidi kukwepa kunilaumu dereva wake,nadhani alinihurumia pia...na kuniambia nisihofu tutapata wasaa mwingine wa kusafiri tena...lakini hali hii imeniumiza sana...gari limekuja kuwaka asubuhi nikiwa peke angu
Wasafiri wenzangu naomba mawazo yenu...mnatumia njia gani kuwash gari na kuwaka punde tuu mnapokua mlilizima kwa mapumziko ya muda mfupi
Asanteni naomba kuwasilisha