Gari yako imegoma kuwaka? Sababu zinazopelekea gari kupata ugumu wa kuwaka...

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Siku ikiwa imeanza na tukiendelea na ujengaji wa uchumi wetu na nchi kwa ujumla. Leo ningependa kuelezea kitu ambacho watu wengi huwa tunakumbana nacho na mara nyingi hiki kitu ubaya wake hutokea ghafla. Ishawahi kukutokea umeendesha gari ukaenda kuiegesha ukaingia sehem labda saluni au kwenye ofisi fulani unarudi jua limekupiga na gari ndani ni joto unapiga hesabu hapa nawasha naweka kiyoyozi full alaf unapiga start kitu oyaaaaaa..... Gari haiwaki kila ukipiga haiwaki. Hapo ndo unajiuliza jaman si nilizima ikiwa sawa kabisa?

Kitu kimoja kuhusu gari kumbuka ni mashine iliyotengenezwa na binadamu kama wewe hata kama unaithamin kiasi gani ugonjwa au fault hutokea tena bila hodi na ndo maana ukiwa na gari unatakiwa ujiandae kwa lolote litalotokea hapo basi huja kauli ya kama huna kitu mfukoni basi usiendeshe gari maana likija tokea la kutokea hutokua na la kufanya zaidi ya kupiga piga simu na hapo ni mpaka uwe na airtime

Mojawapo ya matatizo ya gari ni kushindwa kuwaka yani kiufup hata kama umetoka kuinunua gari dakika tano zilizopita pale showroom hili tatzo linaweza kutokea na inaweza kuwa kubwa au dogo tu mfano terminal zimelegea tu ni kiasi cha kukaza hata na kidolr gari ikawaka lakin ndo hujui sasa. Tusipige kelele sana ndugu yangu naomba nielezee sababu kadhaa ambazo zinasababisha gari yako ishindwe kuwaka au endapo ikikutokea tu basi angalia haya mambo kwanza kabla hujafkiria vinginevyo.

1. Kulegea kwa terminal za betri.
Honestly hii ni sababu kubwa sana ambayo inapelekea gari yako kushindwa kuwaka. Kumbuka betri ya gari yako ndiyo chanzo kikuu cha umeme kwenye gari yako lakin pia ndiyo chanzo cha dharura cha umeme kwenye gari yako so hata gari umetoka kununua zero km leo kama betrii ni kipengele basi jua hapo una gofu.

Tunapopeleka magari yetu garage au labda unataka kum boost mtu ndipo betri husauliwa sana kwenye kurudishiwa. Hakikisha unapofanya shughuli inayohusu betrii basi unairudishia na kuikaza inavyotakiwa kwani ikilegea kidogo inaweza kusababisha kutotoa volt husika za kufanya gari iwake kama sikosei ni 12.6 hivi. Lakini kingine ni kuota kutu kwenye terminal ikitokea kitu kama hiki basi hakikisha unaitoa hiyo kutu.

Nitajuaje shida ni betrii? Endapo unawasha gari yako na starter haizungushi yani hailiii ule mlio wa kuwasha gari basi jua shida inaweza kuwa ni betrii na mara nyingi huleta mlio wa triiiiiii triiiii basi hebu kagua betrii yako kwanza.

2. Mafuta kuwa machache.
Ili gari iwake na mashine ifanye kazi inahitaji mafuta ya either petroli au dizeli hivo mafuta yanapokua machache pump inakosa cha kupeleka mafuta na engine kukosa kitu cha kuchoma hivo gari haitoweza kuwaka. Tofauti yake na sababu ya kwanza hapo juu ni kwamba hapa gari itakua starter inazungushaa njiiiinjinjinjinji lakin haiwez kupokewa na engine lakini hili halihitaji maelezo mengi sana sababu tayari gari yako ina guage ya mafuta so jibu utakuwa nalo mwenyewe.

3. Tatizo la starter.
Kazi ya starter ya gari yako ni kupeleka mshindo kwenye engine ili iweze kuruhusu piston zifanye kazi yake na hatua nyingine zifate mpaka kupelekea gari yako kuwaka hivo basi starter ni kama switch ya kuruhusu engine iwake hivo inapokuwa mbovu basi gari yako haitawaka ila wacha nikupe ujuzi wa emergence endapo shida ndo kwanza inaanza maana ugonjwa ukiwa mkubwa hutofanya lolote mpaka uibadili. Starter nyingi ugonjwa huanza taratiibu sasa kumbuka njia pekee ya kutibu ni kuipeleka kwa fundi itengenezwe au ununue mpya.
For emergency unaweza acha gari ipoe kwa masaa kadhaa then ujaribu kuiwasha itakubali au unaweza chukua nondo au kitu uigonge gonge then ukiipiga itawaka lakin hii ni kwa emergency.

4. Kuharibika kwa switch ya starter
Hapa tunaongelea ile sehemu ya kuingiza funguo na kuwasha gari. Kutokana na matumizi yake kuwa ni ya mara kwa mara huwa inatokea switch hii kuharibika na pindi inapoharibika hutoweza kuwasha gari na solution kubwa ya tatzo hili ni kubadilisha tu switch na kuweka nyingine. Endapo utaigusa na kuhisi joto kali kwenye switch basi jua kutakuwa na tatzo kwenye wiring yake kwenye gari hivo unahitaji fundi umeme kuifuatilia. Lakini kuna elimu ningependa upate.

Kumekuwa na tabia ya watu kuweka funguo ya gari na funguo nyinginezo yani unakuta ile holder ina funguo nyingi sana so unapochomeka kwenye switch zinakua zinaning'inia hakika hili linasababisha kuharibu switch ya gari yako jitahidi holder ya funguo ya gari iwe na funguo ya gari tu kwa usalama wa gari yako.


5. Kukata kwa fuse
Binafsi hii ishawahi nikuta. Nakumbuka nili park gari usiku vema tu then asubuh nimekuja kuwasha gari holaaaa!! Jaribu sana lakin wapi. Nakumbuka kipindi hiko sikuwa na uelewa wowote kuhusu magari basi gari ilikaa siku nzima hadi jion kuna jamaa yangu ni fundi akaja kucheki tu akachomoa fuse bahati nlikua na fuse za akiba basi akaipachika gari ikawaka.

Kiufupi fuse imetengenezwa kukata endapi kutakuwa na kuongezeka kwa nguvu ya umeme au kama kutakua na shida ya ki umeme ya kifaa husika ambacho kinalindwa na fuse hiyo na ndo maana kunakuwa na fuse nyingi sana kwenye fusebox ya gari yako na kila fuse ina kifaa chake inalinda hivo basi endapo fuse ya labda tuseme fuel pump imekata basi jua fuel pump haitafanya kazi na kama haitafanya kazi basi jua mafuta hayatapelekwa kwenye engine na kama hayatapelekwa jua gari haitawaka maisha mpaka utakapobadili fuse na hivo hivo kwa vifaa vingine.

Ushauri wangu kama ilivo una fuse za akiba kwenye nyumba yako kwaajili ya vifaa mbali mbali basi hata kwenye gari yako jitahid kuwa na fuse za akiba hakika itakusaidia.

Makala hii imeandikwa na Hamis Mgaya

IMG-20230611-WA0010.jpg
 
Ishu nyingine ambayo umeisahau ni ishu ya alarm ukajisahau ukabonyeza basi gari haitawaka hadi uitegue
 
Back
Top Bottom