Furssa ya ajira fundi pikipiki

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
610
733
Abraar Education Centre tunahitaji fundi pikipiki mzoefu ambae ana uwezo wa kutatua matatizo yote ya kiufundi kwa pikipiki zilizozoeleka Tanzania.

Tunaanzisha kituo kipya cha mafunzo ya ufundi pikipiki kwa vitendo.

Fundi awe na uzoefu wa kutosha kufanya kazi zake bila kusimamiwa.

Kutatolewa mafunzo ya mara kwa mwara kwa fundi ili kuhakikisha anaelewa na anafata vigezo vya ufundi bora, anafata maadili ya ufundi bora, nidhamu za ufundi bora, na anaielewa miiko ya ufundi bora.

Malipo ni ubia wa kugawana faida kati ya Abraar Education Cebtre, Mwekezaji wa mtaji na Fundi. Pia tunahakikisha tunagharamia, sehemu ya makazi kuishi fundi au kwa kumpatia nyumba zetu za wafanya kazi au kumkodishia nyumba ya kuishi., Bima ya afya msingi pia itatolewa kwa yeyote ataebahatika kujiunga nasi.

Awe tayari kuishi karibu na eneo la "workshop" lilipo.

Tupo, mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu, Wilaya ya Kibaha mji, Mkoa wa Pwani, Tanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605 au 0656399856.
 
Back
Top Bottom