Natafuta Coil Original ya Pikipiki Cc110 na Fundi Mzuri na Mwaminifu wa Pikipiki

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
Wataalam Habari zenu

Mdogo wenu kiukweli nakutana na changamoto ya kwenda kwa fundi Kila baada ya muda Kwa tatizo la kuungua Kwa coil.. pikipiki yangu ni private siifanyii Biashara.

1. Coil ya Kwanza iliyokuja na Pikipiki iliungua MFUMO wa Taa yaani Taa zilikuwa ukiwasha baada ya muda zinafifia hivyo mwanga hakuna nikabadilisha coil.

2. Coil ya pili Siku moja natoka masafa yangu bagamoyo nafika maeneo ya bunju pikipiki ikazima kuja kuangalia ni kwamba jiko moja la coil likipata Moto Sana inafanya pikipiki izime.. hivyo nikawa nikiendesha na ikizima huwa naisubilia ipoe kisha niendelee (ilinitesa Sana hii hali) nikabadilisha coil

3. Coil ya tatu nimeenda zangu Kigamboni vizuri nikafanya mizunguko yangu (kwenye mizunguko nilitumia usafiri mwingine pikipiki nilipaki sehemu) nilivyo rudi pikipiki ikawaka vizuri Ila niliacha ichemke kidogo kama Dakika 2 ghafla ikazima ndo haikuwaka tena.. kesho yake fundi kuja kakuta imeungua coil jino la kuwashia.. nikabadilisha

4. Coil ya nne Juzi mvua kubwa ilinjesha Dar sasa sehemu niliyoenda kujikinga kiukweli pikipiki haingii kiukwel pikipiki ilinyeshewa na mvua, mvua ilivyokata nikawasha nikaendelea na mizunguko yangu.. nikafika sehemu nikapaki, baadaye nikawasha ili niende sehemu eeh ile kuwaka na kutembea kama Mita 100 ikazima ghafla Tu.. nikamuita fundi wangu kuja kuangalia sehemu ya coil maji yaliingia ya mvua.. sasa nikamuuliza maji yanaingiaje wakati pamezibwa naye Hana majibu.. hivyo coil ikaungua ikabidi anibadilishie.

Mpaka sasa natumia Coil ya Tano, na hii ndo Coil ya kichina nawaza ZILE Safar zangu za mbali itaweza kweli?

Katika masafa yangu ya mbali yote Tanga, Dodoma coil haijawai kuungua ila nikiwa mjini Tu yaani ndo shida.

Sasa wataalam naomba Msaada wapi naweza kupata Coil Original ya Pikipiki yangu hapa Dar es Salaam pia wapi kuna mfundi mzuri na mwaminifu hapa Dar maana nishaona huyu fundi naye mwamini ananizingua tu coil zinaungua ovyo na yeye ajui shida iko wapi.

Naomba Msaada Wenu pikipiki nzima kabisa ila Coil ndo Mchawi.

PICHA: Mfano wa Coil Yangu
images%20-%202023-01-15T082725.926.jpg
 
Nenda mitaa ya Fire kuna Duka lipo pembezoni na Jengo la Fire linaitwa Bike Point au kama unaenda Gerezani upande mbele ya Duka la Toyota kuna maduka ya vifaa vya pikipiki.
 
Asante sana Mkuu
Ni pikipiki gani hiyo mkuu, huyo fundi aliyesema maji yaliingia kwenye magneto coil bila sababu au cover la engine linatundu. Ignition coil au nyaya za kutoka kwenye magneto zitakuwa zipo loose zinasababisha short
 
Ni pikipiki gani hiyo mkuu, huyo fundi aliyesema maji yaliingia kwenye magneto coil bila sababu au cover la engine linatundu. Ignition coil au nyaya za kutoka kwenye magneto zitakuwa zipo loose zinasababisha short
Hii Mkuu inaitwa Lifo 110cc.. itakuwa ni tundu ila natafuta coil original mapaka sasa naogopa kwenda Safari ya mbali (adventure) sababu inaweza ikanizimikia tu ghafla
images%20-%202023-01-15T190802.100.jpg
 
Hizo mbona spare zipo si wana dealer wao kabisa. Kama tundu umeliona mpe fundi azibe na hardite au waunge na aluminium
Ameziba na Mpira flan hivi wa waya WA Coil ila nawaza inaweza isiwe mvua pikipiki ikazima Tu kisa Coil nawaza Sana
 
Back
Top Bottom