Fumanizi hili Guest house Iringa

Fumanizi hili Guest house Iringa

Ndo mana kuna wanamuziki walishaimba kwamba "Hii kitu hi kitu hii tu hii, Hii kitu hii, Hii kitu hii..... inagombanisha watu hii kitu hii, inagombanisha hata ndugu hi kitu hii, watu wakatana mapanga shauri ya kitu hii, watu wanakuwa chongo shauri ya kitu hii, watu wanakuwa vilema shauri ya kitu hii, wengine wanakufa shauri ya kitu hii..." NOMA.
 
piga kabisa huyo!!!!

halafu mianamke ya siku hizi inakera!!!! yani unaenda kut*wa saa mbili asubuhi??

ina maana na huyo mwanaume alikuwa wapi?? hakulala kwake ama vipi?
 
hivi kuna watu wanaoweza kugawa kisago hadi mtu akapoteza fahamu? wapi wanatoa mafunzo haya?
 
Umenichekesha sana wallahi...laiti ungelijua wala sipo hivo...sikubali tu kuonewa bila sababu!
sababu si kufumaniwa ...asingefumaniwa asingepigwa......
cc.... watu8
 
Last edited by a moderator:
Hasira hasara.

Hiyo ni tabia ya ubinafsi na umiliki...kama ameamua kumpa talaka kwa nini anampiga? Kwa sababu ana nguvu kuliko mke wake? Kama ana nguvu si apigane na wanaume wenzake? Na ukute hata yeye hakulala nyumbani ila kwa kuwa ni mwanaume ...

Nimetoka kuangalia movie moja baba alikuwa anatoka kuwachukua watoto shule wakawa wanalalamika wana njaa.. akawambia wabaki kwenye gari yeye avuke barabara aende kuwachukulia chakula fast food. Mtoto mdogo si akafungua mlango kumfuata. Akagongwa na gari. In short walipomkimbiza hospital ikatakiwa aongezewe damu na doctor ni rafiki wa familia hakuchukua muda kugundua mtoto si wa rafiki yake. Ilikuwa balaa. Ile movie ilianza kama vile ndoa ya jamaa ni nzuri kupita maelezo. Mke alijifungua last born wao akapewa funguo za gari kama zawadi...leo hii mtoto last but one ni wa nje.

Jamaa kaenda kumbana mkewe aseme baba ni nani ili mtoto asije akafa kwa kuwa damu inahitajika. Kumtaja baba mume kachanganyikiwa. Ni best friend wake...lakini source ya cheating ilikuwa mume. Alikuwa anampiga sana mkewe na kumfukuza ndani (kabla ya kubadili tabia) Akimfukuza best friend wake na mkewe wanampa hifadhi. Na mkewe ni mzuri hasa. Kama hujuavyo wanawake ni rahisi sana ku fall kwa mtu anayejali. Wakajikuta wana fall. Alipopata mimba akafanya juu chini akarudi kwa mumewe.

Kibaya zaidi yule doctor akamshauri wawapime watoto wote DNA. Wakakuta mtoto wa kwanza nae si wa mume (walikuwa na watoto 4; walibaki 3 baada ya 1 kufa)...by then alikuwa ameshamtimua mkewe....baada ya kushauriwa na huyo doctor wakaamua wamtafute huyo mwanamke awambie ukweli na huyo mtoto ni wa nani...

Jibu ni wa mdogo wa mume wake...soon baada ya kufunga ndoa mwanaume alikuwa kiguu na njia...business trips, mara UK, mara US. Mke anasema naogopa kukaa peke yangu nyumbani...kaletewa shemeji akae nae...haya shemeji kuna siku ikatokea situation wakavunja amri ya sita...ndio huyo first born...

Mwishi wa siku baada ya kushauriwa na mama yake na wazee alimsamehe mkewe kwa sababu walimuhoji alikuwa wapi mpaka mkewe akawa anazaa nje...

Ni ngumu na ni movie ila kuna wanaume wana busara na hawafikirii kwa ushabiki...wanasamehe na jamii (including mimi na wewe) tunakuwa hatuamini kama mwanaume wa hivyo ana akili sawa....kuna tofauti kati ya mwanamke alochiti sababu ya situation na anayemuaga mmewe daily anaenda night shift kumbe muhongo na hana mpango wa kuacha uzinzi.

Wanawake wengine wanazaa nje sababu ya waume zao...wana wa frustrate...wakipata a shoulder to cry on...inakuwa real shoulder...
 
hivi kuna watu wanaoweza kugawa kisago hadi mtu akapoteza fahamu? wapi wanatoa mafunzo haya?
Hizi ni mbinu za akina KASEJA mashambulizi yakizidi..unajivunja kiaina.... hapo kapunguza mashambulizi....mpaka wafike nyumbani
 
Na watu humu wanachangia mada kwa ushabiki...huyu angekuwa, binti yako, dada yako au mama yako ungekubali apigwe hata kama ana kosa gani?????

Muwe mnajaribu kuvaa uhusika...kosa amefanya lakini hiyo adhabu si sahihi...hakuna binadamu anastahili kupigwa...siku hizi hata wanyama kwenye nchi za wenzetu wanalindwa. Na huku kwetu wanafunzi tu wameacha kupigwa...upori pori at work

Huyu angekuwa dada yangu huyo mwanaume ndio angejua kama kuoa si kununua...tungemfunza adabu nyumba nzima.Lol Kama wameshindwana amrudishe kwao
 
Mimi siku zote huwa najitaidi sana kumfanya mtu wangu asitoke njee kwa kuhakikisha majukumu yangu kama mwanaume nayatimiza kila idara. Hata akitoka nikajua sitompiga, tachunguza madhaifu yangu kwanza. Nitaongea naye, tufike muhafaka yaishe siku hiyo hiyo. ile dhana ya mwanaume ndio mwenye haki ya kwenda nyumba ya kando, mwanamke ikitokea imepitwa na wakati. kabla ya kutoa hukumu, jiulize wewe upo vyema. Tutazungumza mara ya kwanza, ya pili ya tatu. Asipo nisikia, namwambia mama kwa heri ya kuonana. Si dhani kama ni vyema kumpiga alafu usiku kitandani unamwambia sogea huku.

mkuu na maradhi yote haya ujifanye mwema kiasi? lol
 
Hata kama kamfumania, hakutakiwa kumpiga, TGNP na TAMWA waingilie kati, unyanyasaji wa kijinsia huu.
Anaweza kufa kwa kipigo hiki, nani anajua kama hapata madhara makubwa ya ndani?

Nyie ndo mnalea uzinzi duniani hapa, madhara ukimwi na magonjwa ya zinaa.
 
Baada ya kumpiga wife wake jamaaa kapata faida gn? kupiga sio dawa!
 
piga kabisa huyo!!!!

halafu mianamke ya siku hizi inakera!!!! yani unaenda kut*wa saa mbili asubuhi??

ina maana na huyo mwanaume alikuwa wapi?? hakulala kwake ama vipi?

Ndugu yangu mwanaume alijihimu kugema ulanzi.
 
Na watu humu wanachangia mada kwa ushabiki...huyu angekuwa, binti yako, dada yako au mama yako ungekubali apigwe hata kama ana kosa gani?????

Muwe mnajaribu kuvaa uhusika...kosa amefanya lakini hiyo adhabu si sahihi...hakuna binadamu anastahili kupigwa...siku hizi hata wanyama kwenye nchi za wenzetu wanalindwa. Na huku kwetu wanafunzi tu wameacha kupigwa...upori pori at work

Huyu angekuwa dada yangu huyo mwanaume ndio angejua kama kuoa si kununua...tungemfunza adabu nyumba nzima.Lol Kama wameshindwana amrudishe kwao

Mi hata angekuwa mama angu mzazi provided mdingi kamfumania apigwe tu
 
Amseme tu kisha amsamehe,na kama hawezi kufanya hivyo amuache!!

Kumegewa mke halali wa ndoa umempiga pamba soap soap, lips stick, saloon alafu jamaa linakuja kujibebea kiulaini.
 
Duh! Anaukika kama jamaa alikua hatambui huyo ke ni Mke wa watu?
Adabu na fundisho zuri lingepatikana kwa kuwahukumu wote!!

muongo, aliogopa kipigo toka kwa hilo dume. akamalizia hasira kwa mkewe.
 
Hivi kama fumanizi ilikuwa saa 2 asubuhi, ina maana amelala hapo na mumewe amemfuata asubuhi? Au huyu bibie ametoka Mwembetogwa hiyo asubuhi kwenda Mwangata alikofumaniwa? Na huko kumbeba kwenda nae Mwembetogwa toka Mwangata mbona kazi? tujulishe shuhuda uliyeleta hii habari.
 
Ushamba na uncivilized kupiga mwanamke!!! Ukimfumania piga chini. Tafuta mwingine. Unaeza piga mtu ana maradhi yake au ndiyo siku zimefika ukaambulia murder case! Keko panakuwa bedrum yako!!!
Ukaishia kukosa vyote!!!! Tusifanye vitu kwa hasira pasipo tumia akili. Hasira hasara always!!!
 
Back
Top Bottom