Kwanini aliweza kugundua kuwa mwanaume aliyemfumania na mkewe hana hatia kama alikuwa katika hali hiyo?
Huko ndio tunaita kuchanganyikiwa sasa, kwa akili ya kawaida asingeweza kusema hilo alilolisema kama kweli alilisema. Ni kweli mke anaweza kuwa ni mkosaji namba moja maana yeye alitongozwa (kitu ambacho hutokea mara nyingi kwa wanawake wengi), kosa linakuja pale yeye alipokubali, lakini hiyo haimuondelii mkosaji wa pili kosa, huyo mgoni wa kuime. Kumbe basi katika hali ya kawaida yule ndg anayetuhumiwa kwa kosa la ugoni naye ana makosa, lakini huenda kwa akili kutokuwa katika hari ya kawaida huyu jamaa anamuona hana kosa, kitu ambacho ni illogical.