Fumanizi hili Guest house Iringa

Fumanizi hili Guest house Iringa

Mwanamke ameamua kutumia mwili wake kwa manufaa yake..kwa nini umpige? Afadhali kama mwanamke angekuwa na uwezo wa kuiba dudu ya mwanaume na kuitumia kwa rafiki yake wa kike ndio jamaa angempiga kwa kosa la wizi wa ndude..

Kupiga mwanamke ni ujinga.. na tunaendeleza ujinga!!!.. Kuna maandiko ya dini fulani yanasema kabla hujamuhukumu mwenzako basi kwanza jihukumu mwenyewe......Anyway..Adhabu kubwa ilikuwa ni kuachana nae kwa amani kila mtu ashike hamsini zake..
 
Sikubali kupigwa by any means...TRY ME watu8 lol

Mwanamke waonekana mtata sana wewe...ninye ndio huwa mwajifunga vibwebwe na kuvaa vitaiti wakati wa kusutana
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke waonekana mtata sana wewe...ninye ndio huwa mwajifunga vibwebwe na kuvaa vitaiti wakati wa kusutana
Umenichekesha sana wallahi...laiti ungelijua wala sipo hivo...sikubali tu kuonewa bila sababu!
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Hata kama kamfumania, hakutakiwa kumpiga, TGNP na TAMWA waingilie kati, unyanyasaji wa kijinsia huu.
Anaweza kufa kwa kipigo hiki, nani anajua kama hapata madhara makubwa ya ndani?

Ndg yangu Kongosho, kwani hao TGNP na TAMWA walimutuma huyo dada akafanye uzinzi asb yote hii. Mbona mnazibambikia hizi taasisi majukumu mengine ambayo yako nje ama mbali na majukumu yao. Siiungi mkono sana mwanandoa yeyote kumpiga mwenzake lakini lipokuja swala mahususi kama hilo lolote linaweza kutokea ikiwemo kupigwa na hata kufikia kupoteza maisha/uhai wa mhusika.

Wapo watu waliwaua wagoni wao, kisheria ni kosa kujichukulia sheria mkononi, lakini mahakama ziliwaachia huru kutokana na aina ya tukio lilivyotokea na huyo mhusika alivyorespond kwalo, hebu mara nyingi tujaribu kuuvaa uhusika, imagine kama ungekuwa wewe ungefanya nini.

Eti TGNP, TAMWA, nk, kumbe basi watu wanaweza kuamua kufanya upuuzi ndani ya ndoa zao kwa kujua ama kutambua kuwa hizo taasisi zipo kwa ajili ya yao na kutetea upuuzi wao. Nitazishangaa hizo taasisi za namna hiyo ambazo zitaacha mambo ya msingi kama ya mirathi ya wajane, utumikishwaji wa watoto wadogo nk, na kwenda kushughulikia mambo ya kujitakia kama hayo.
 
Last edited by a moderator:
wamezidi nao00000000 rudixha kwao hafai huyo n mke mbuzi kla m2 analamba 2
 
Umenichekesha sana wallahi...laiti ungelijua wala sipo hivo...sikubali tu kuonewa bila sababu!

Suala la kushikwa ugoni bado tu waliona kama ni 'kuonewa bila sababu"?
 
Suala la kushikwa ugoni bado tu waliona kama ni 'kuonewa bila sababu"?
Ndio ni uonevu hahitaji kupigwa mtu hapo...huyo unaongea nae tu na kama hamuwezani kila mtu anashika hamsini zake!
 
Mwanmme anapozini anapigwa na nani?

Kuna mama alipigwa na mmewe, akapata majeraha kwa ndani bila wao kujua na alikuwa na ujauzito mdogo. Baada ya wiki mbili ujauzito ukatoka, she didn't make it sababu hakuna aliyemjali.

Basi watoto wakaishia kupoteza mama, mume alioa mwingine.

TGNP na TAMWA ndio walimtolea mahari huyo bwana?...acha mtu apewe mkong'oto kidogo maana hakuna taasisi inayoshughulikia mafumanizi
 
I dont condone violence against women but in this case "I understand". Mke mzinzi ni janga kwa familia na taifa kwa ujumla.
 
sikubali kipigo na sitaruhusu kufumaniwa wala kufumania
 
Safi kabisa...Tia mbata tu,haiwezekani mtu asubuhi na mapema muda wa kuijenga Tanzania we unawaza ngono..Hao TAMWA nao watakua vilaza kama wanatetea huu umburukenge..!
 
Mwanmme anapozini anapigwa na nani?
Mwanaume apigwe na mkewe...

cc: mimi49

Kuna mama alipigwa na mmewe, akapata majeraha kwa ndani bila wao kujua na alikuwa na ujauzito mdogo.
Baada ya wiki mbili ujauzito ukatoka, she didn't make it sababu hakuna aliyemjali.
Basi watoto wakaishia kupoteza mama, mume alioa mwingine.

Huyo mama alitoka nje ya ndoa au alifumaniwa?
 
Last edited by a moderator:
Uzinzi ni A, kuchukua sheria mkononi ni B
Havichangamani! Kama ameumia sana, angempa talaka tu maana hata kisheria inaruhusiwa kumwacha kwa kuwa na mahusiano nje ya ndoa.

Mwanamme anayepiga mkewe kwa sababu yeyote ni 'WEAK', period!

Duh, huyo mwanamke naye mkali asubuhi yote hii, au alilala huko jamani, maana kama saa tatu tukio limetokea, it means around saa mbili alikuwa eneo la tukio already hata hiyo guest house huenda hawajaanza usafi maana wateja wengi unakuta wamelala bado.

Sidhani kama baada ya hapo kuna ndoa tena, na kama ipo sijui kama imani itakuja kurejea baina ya hao wanandoa, na hata yule bwana aliyeachwa aende zake kisa eti hana kosa, sijui kama huko aliko anapumua salama.

Unzinzi ni dhambi, lakini unapoufanya kwa mke wa mtu ama mume wa mtu nadhani ni dhambi maradufu, tutafakari zaidi kabla ya kufanya uamuzi ya kishetani.

Huyo dada kwa jinsi alivyokamatwa, na muda huo, hakika kwa mwanaume yeyote anaipenda ndoa yake kipigo kwa huyo dada hakiepukiki, japo nimeona wengine sijui wanasema TGNP, TAMWA nk, as if hizo taasisi zipo kuwatetea wanzizi ama ndizo zimemtuma kuzini tena asb yote hii. Kwenye ndoa tu muda kama kama hakuna sababu za msingi sana huwezi kuta wanandoa wanafanya mapenzi japo kwao ni halali kabisa na hawana kizuizi cha muda sasa wewe na wizi wako unajihimu kana kwamba ndio kazi yako, hapina wakupige tu wewe.
 
Ndio ni uonevu hahitaji kupigwa mtu hapo...huyo unaongea nae tu na kama hamuwezani kila mtu anashika hamsini zake!

Wewe wasema...ikiwa hata sheria inatoa mwanya kwa mgoni kuuawa (kutegemeana na mazingira), wewe unashangaa adhabu ndogo tu hii ya mkong'oto
 
Back
Top Bottom