full vikombe sasa, hiki chajileta City centa, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

full vikombe sasa, hiki chajileta City centa,

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Nov 11, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  [h=3]full vikombe sasa, hiki chajileta City centa,[/h]

  [​IMG]
  Huu ni mwaka wa kuoteshwa Vikombe Bongo, cha sasa kimekuja kisasa zaidi, chachemshiwa katika jiko la gesi, chagharimu 1000, wanjwa mara mbili kwa wiki mbili baaaasi, mapaparazi wanakuwa wakwanza kuonjeshwa, mtindo ndo ule ule, Uandikishwi, uulizwi ugonjwa wala historia, no kurudia wala maswali. Kwa hisani ya Mo Blog
  [​IMG]
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  "MWAKA WA VIKOMBE" BONGO  [​IMG]Margreth Mutalemwa au Bibi akiombea kikombe kabla ya kumpa mgonjwa, huko Uzuguni Tabora, Huu ni mwaka wa miujiza au vikombe?


  Kikombe cha Babu - 78% wamepona by Utafiti.
  Juzi niliweka post hapa kujaribu kutafuta ushuhuda wa wale ambao walienda Loliondo Samunge kwa Babu kupata kikombe ili kujua kama kuna yeyote ambaye hakika kupitia kikombe amepata uponyaji, hakuna aliyejitokeza mpaka sasa.
  Leo hii Synovate wamekuja na utafiti unaoonyesha kuwa asilimia 78 wamepona.


  [​IMG]
  ASILIMIA 78 ya watu waliotibiwa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila, walipona magonjwa yao.
  Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Synovate kuanzia Mei 2 hadi 19, mwaka huu na kuwahoji watu 1,994 wenye umri zaidi ya miaka 18 maeneo mbalimbali nchini.Utafiti huo uliotolewa na Synovate kwa gazeti hili jana, unaeleza kuwa ni asilimia saba waliosema hawakupona wakati asilimia 15 walisema hawajui.
  “Asilimia 78 ya waliotibiwa kwa kikombe cha Babu wa Loliondo, walisema wamepona magonjwa yaliyokuwa yanawakabili,” inaeleza sehemu ya ripoti hiyo ya utafiti.
  Utafiti wa Synovate umekuja wakati ambapo utafiti wa awali uliofanywa na serikali juu ya dawa hiyo ya Babu kuinyesha kuwa ina uwezo wa kutibu magonjwa sugu kama vile kisukari, saratani, moyo na Ukimwi.
  Serikali ilisema bado inaendelea na utafiti zaidi juu ya dawa hiyo, ambao unaweza kuchukua muda wa hadi miaka mitatu ikizingatia kuwachunguza waliotibiwa na kiwango cha dozi, kulingana na aina ya ugonjwa.
  [​IMG]
  Ripoti ya Synovate inaonyesha ingawa ni watu wengi wanaotamani kuponyeshwa dawa ya Babu, ni Watanzania wachache wenye uwezo wa kumudu gharama za kwenda Loliondo.
  Asilimia 83 walisema ni vigumu kupata dawa ya mchungaji huyo maarufu kama Kikombe, huku asilimia 17 wakaonyesha hakuna tatizo la kumfikia.Hata hivyo, kati ya waliokwenda asilimia 25 hawakuwa tayari kutaja magonjwa waliyokwenda kutibiwa, wakati asilimia 24 walisema ni kisukari.
  Magonjwa mengine na asilimia ya watu walioenda kutibiwa kwenye mabano ni moyo (22), Ukimwi (13), saratani (12), vidonda vya tumbo (7), pumu (5), magonjwa ya ngozi (4), maumivu ya miguu (4), kifua kikuu (3), maumivu ya tumbo (3), maumivu ya uti wa mgongo (2), maumivu ya kifua (2), macho (1) na waliokwenda bila tatizo maalumu (3).
  Mchungaji Masapila alijijenga umaarufu mkubwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu baada ya watu kutoka sehemu mbalimbali nchini na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kupata tiba hiyo.
  Hali hiyo ilisababisha baadhi ya ndugu kuwachukuwa wagonjwa wao waliolazwa hospitalini kuelekea kwa Babu, yapata kilomita 400 kutoka mjini Arusha.
  Misururu mirefu ya magari ilijipanga kwenda kwa babu na kufanya watu kutumia hadi siku saba kupanga foleni ya kupata dawa.
  Pia, utafiti wa Synovate ulizingatia kuwa kulikuwa na waganga wa jadi waliojitokeza kutoa tiba sawa na Masapila, lakini licha ya hali hiyo, asilimia 60 walikiamini Kikombe cha Babu.
  [​IMG]
  Wengine waliojitokeza na asilimia za kuaminika kwa watu kwenye mabano ni Dogo Jafferi wa Mbeya (9), Magret maarufu kama Bibi wa Tabora (8), Subira Ali (4), Majimarefu (2), Sinkala wa Mbuyuni (2) na babu wa Moma Mtwara (2).  source: Mwanachi
  Picha: ©Emmanuel Herman
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtajakufa kabla ya siku zenu! Mtanyweshwa mpaka mafuta ya transfoma, kwa uroho wenu.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  haahahah mkuu na mimi natak kuanzisha kikombe changu nitakiita kikombe cha Jamii forums uta ni sapoti Mkuu?
   
 5. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Synovate imeripoti kwamba:
  Asilimia 78 wamesema wamepona, 7 wamesema hawajapona na 15 wamesema hawajui.
  Ila haijasema78 wamepona, 7 hawajapona na 15 hawajui.
  Umeona tofauti hapo?
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Mie ntakubishia hadi ukome! Hiyo 75%ya synovate haijawapitia nnaowafahamu mimi? Manake hakuna hata mmoja ya jamaa zangu ambae alipona.
   
 7. k

  kamimbi Senior Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nami nipo njiani kuleta kikombe, just wiki ijayo, mahalim pa huduma patakuwa jangwani dsm, bei ni tsh.200/= tu pamoja na shillingi kushuka thamani dhidi ya dolla, mnasemaje washikaji? naomba kampani yenu na muwajulishe na masela wengine pia, au siyo watu wangu, aminia sana.
   
 8. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watu wasipoangalia watapewa mpaka vikombe vya kimpumu.
   
 9. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Noma ipo wapi kama wagonjwa watapona?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  kwanini unibishie si kikombe cha jamii forums upande wa Thread ya J.F Doctor?
   
Loading...