Program Manager
JF-Expert Member
- Aug 6, 2018
- 2,517
- 3,441
Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi kwa wadhamini, viongozi, wadau, wachezaji, wanachama na mashabiki wa Wananchi Young Africans SC kwa mchakato, uwekezaji na mafanikio waliyoyavuna kwa misimu miwili mfululizo na kutwaa vikombe:
- Ngao ya jamii x2
- Ubingwa wa ligi kuu NBC X2
- Azam sports federation cup x2
- Kucheza fainali ya CAFCC na kushinda ugenini dhidi ya USMA ambao wametwaa Ubingwa kikanuni tu.
Baada ya hayo yote waliyoyapanda na kuvuna hatimaye kocha mkuu Nabi na baadhi ya staff wa technical benchi wamepata soko kwenye vilabu vingine ambavyo vimehitaji huduma zao, sawa mpira ni biashara wacha waende na ni wakati sahihi kwao kutafuta changamoto sehemu nyingine kwani wameshatengeneza mazingira ya kufanya hivyo, a good dancer must know when to leave the stage.
Kilichonipush kuandika uzi huu ni baada ya kusikia kutoka vyanzo vya kuaminika vya Yanga kuwa siku moja baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Nesredine Nabi kuondoka klabuni hapo wamepokea maombi ya kazi kutoka kwa makocha zaidi ya 1000 duniani na wenye CV kubwa wakiwemo.
Pia kuna tetesi zinazidi kusambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya kuaminika vya habari vikiihusisha klabu ya Yanga kuwa kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa Al Ahly ya Misri kocha wa soka mwenye daraja ya juu kabisa barani Afrika naye si mwingine bali ni Pitso John Hamilton Mosimane ambaye hivi karibuni pia amevunja mkataba wake na timu aliyokuwa akiitumikia ya Al ahli Saudi ya Saudi Arabia kutokana na mgogoro wa kimaslahi.
Kabla sijataka kujiridhisha usahihi wa tetesi hizi imenibidi kwanza kuipa rank ya juu kabisa klabu ya yanga kwa sababu mbili.
1. Kuhusishwa kuwa na mazungumzo ya kimkataba na kocha Mosimane, kocha mwenye daraja ya juu kwa sasa Afrika. Klabu kubwa itahusishwa na wachezaji na makocha wenye profile kubwa.
Kama ni kweli na watafanikiwa kupata huduma ya Mosimane basi yanga watakuwa wamelamba dume na siyo garasa. Pitso ni bingwa mara kadhaa kwenye Ligi ya Mabingwa barani afrika na ndoto ya Yanga ni kufanya vizuri kwenye ligi ya mabingwa.
2. Njia waliyoipitia yanga na mafanikio waliyoyapata inafanya kuwa moja ya klabu yenye uzani wa juu kwa sasa Afrika, ukweli usemwe kuwa yanga imejitambulisha vyema msimu huu ulioisha na sasa kuelekea msimu wa 23/24 timu itasomeka kama moja ya giants na siyo underdog tena, wameprove kwenye shirikisho sasa kazi imebaki kwenye klabu bingwa.
Nb:si mbeya City, Mtibwa, Mbao, wala klabu yoyote ya uzani wa chini inayohusishwa na kocha mkubwa bali ni vigogo wakuu Dar Young Africans SC daima mbele nyuma mwiko pekee, kwanini? Kwa sababu kwa sasa ni one of the most Giant football clubs in Africa.
MWISHO.