Nmekuelewa mkuuMwanadamu ana hali ya kuabudu. Ipo katika utu wake akiwa mzima wa akili.
Kukiwapo ombwe, maswali au wasiwasi huzuka.
Wasiwasi juu ya kifo na hali nyingine za maisha huongezeka.
Hatma ya uwepo wake hapa, hujaza fikra zake.
Katika mahangaiko yake kutafuta majibu, ndipo anaangukia katika dhana za dini, sayansi, consipiracy.
Akihisi kapata majibu, hufikiri wengine wote hawajui au wanakosea.
Kuhusu mada:
System ni nani? Kama ni watu je wao pia ni waathirika au ni tofauti na wengine.
Je ni viumbe tofauti?
Je ni maumbile kama dunia.
Faida na hasara ni kwao 'system' ni ipi?
Kama ni wanadamu basi ni ujanja tu na haudumu. Hakuna cha mwanadamu kilichodumu zama nyingi.
Kwa vyovyote vile hilo kuwepo au kutokuwepo kwa system hatuondelei kifo.
Ambacho kuna wanaopanga, lakini kinatuchagua.
Twendeje, Turuhusu fikra zetu zifanye mazuri sasa. Maana wanadamu wote kwa namna zao huukiri wema huwaletea furaha.
Miaka michache itumike vizuri.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app