Hawa jamaa miyeyusho sana,tatizo lao kubwa ni kukimbia maswali magumu.
Maswali yangu huwa hawayajibu sasa sijui ni ya kipuuzi hayana maana au magumu sana.
Ila tu nawakumbusha hawa jamaa Elimu haiongopi na huo msamiati wao mara Esoteric Knowledge mara Exoteric Knowledge mara Chakra (Internal Energy/Spiritual Energy) ni mambo madogo sana ambayo yote hukomea kwenye uongo,uoga na wasi wasi tele. Sasa msingi wa maswali yangu huwa nataka wawe wana yajibu ili tuwapeleke huko wanakotaka wao.
Asili ya hizo waziitazo hidden doctrines ni ujinga na mwisho wake huwapelekea kwenye ushirikina.
Hizi lugha zao huwa wanazitumia kwa maslahi yao binafsi ili kuja kuwapiga watu wasio jishughulisha na elimu,ilo waweke matabaka yaliyo asisiwa katika uongo na ujinga,ili wawafanye watu fulani waonekane bora kuliko wengine kisa eti wana elimu zilizofichikana/elimu za siri/hidden doctrines/علم الباطن.
Hakuna binadamu katika uso huu wa dunia anaejua elimu ya mambo yaliyofichikana,Elimu hii hata mitume na manabii hawakupewa seuze hawa wasio jua kwanini kuna usiku na mchana au wasio jua ni zipi lazi za nyota.
Nimewakumbusha tu.