Mwandishi J kwayu ni mwehu, leo ujinga wake ukatumike kufundishia? La saba mwenyewe alifeli akaenda kusoma private
Kama alifeli akaenda kusoma private shida iko wapi?! Hakumaliza masomo?! Hakupata qualification?! Huenda ana mafanikio kuzidi waliofaulu na kumtangulia mwanzo
 
Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Mbona kama hawajiamini hivyo wamekaa kimchongo sana kama wanaoga nje
 
Ilitakiwa pia kijumuishe mauaji ya kinyama na mateso dhidi ya waandishi wa habari, wanaharakati na wanasiasa wa mlengwa wa kushoto yaliyotekelezwa na uongozi wake
 
Kwa kweli hakuna kitabu Bora kama hicho. Ili kuimarisha uzalendo, nashauri kitabu hicho kitumike kufundishia mashuleni elimu ya historia. Hakika watoto watakua wakielewa mambo mengi kwa kina.

Hongereni watunzi
Kuuhusisha uzalendo na awamu ya 5, kunatia mushkeli wa ukweli wa unachoongea.
 
Kwa kweli hakuna kitabu Bora kama hicho. Ili kuimarisha uzalendo, nashauri kitabu hicho kitumike kufundishia mashuleni elimu ya historia. Hakika watoto watakua wakielewa mambo mengi kwa kina.

Hongereni watunzi
Wewe masikini mwenzangu endelea kuhubiri uzalendo wakati wenzetu wanaendelea kulamba asali kupitia uzalendo wangu na wa kwako.
 
Kwa mamlaka nisiyonayo naagiza kitabu hiki kitumike mashuleni tuachane na kina Ngoswe walopitwa na wakati....
Lissu alisema "tumepata kiongo-zi wa ajabu haijawahi kutokea" mafurukuzenze hayakuelewa namengine Hadi Leo hayaelewi/yanajidai hayaelewi
Ndugu usilalamike sana kuhusu Magu,najua alikutumbua na vyeti vyako fake,Mama kasema wote wenye vyeti fake anawarudisha tena kazini na ma fake yenu ili muendeleze tena usanii wenu wa upigaji!!
 
Historian ndo kitu gani? Huko Chato hakuna watu? Hayo maendeleo alopeleka hawastahili? Hebu kuweni na akili sometimes.
Umenikumbusha kitu,zamani wakati ATM machine zinaanza kupelekwa nje ya mji Kama kule Mbagala kuna baadhi ya watu walikua wanashangaa sana,eti watu wa Mbagala na ATM machine wapi na wapi!? Leo hii ATM machine zipo kila mahali, na hayo ndiyo maendeleo yenyewe!!
 
Si naona unajiliza sana uhuni wa dhalimu ukiwekwa hadharani.
Ndio hisia zako zinavyokwambia hivyo? Halafu mie nilidhani huo uhuni wake ulikuwa hadharani kila mtanzania na dunia inajua kumbe sivyo, sasa mnamdananisha vp na Idd Amini na Hitler?
 
Yaliyojificha uwekezaji wa Hayati Dk Magufuli Chato yawekwa vitabuni​

Ijumaa, Aprili 14, 2023
magufuli-pic.jpg

Dar es Salaam. Ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kupoteza maisha Machi 17, 2021 akiwa madarakani, waandishi wakongwe wanne wamezindua kitabu kinachoonyesha sura ya kiongozi huyo na uwekezaji mkubwa alioupeleka wilayani Chato.

Absalom Kibanda, Ansbert Ngurumo, Neville Meena na Jesse Kwayu ndio waandishi walioandika kitabu hicho chenye jina 'I am the State' ikiwa na maana Mimi ndio Dola.

Kitabu hicho linaonyesha hali ilivyo sasa wilayani Chato alipozaliwa kiongozi huyo mkuu wa nchi baada ya miradi mikubwa ya maendeleo
Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa katika kitabu hicho ni wanyama waliopelekwa Chato enzi ya utawala wa Rais Dk Magufuli, ujenzi wa kiwanja cha ndege, uboreshaji mkubwa wa miundombinu, wananchi kukimbilia kununua viwanja, ujenzi wa masoko na miradi mingineyo.

Pia kitabu hicho kimeangazia fedha zilizopelekwa wilayani huko zitarejeshwaje, mpango wa wilaya hiyo kuandaliwa kuwa mkoa uko uliishia wapi.

Kabla ya uzinduzi wa kitabu hicho Ansbert Ngurumo amesema jina la kitabu limetokana na hofu iliyoshuhudiwa baada ya utawala wa hayati Dk Magufuli tangu mwaka 2015-2021 kuelekeza miradi mingi eneo alikozaliwa bila kuwepo mtu aliyehoji.

Amesema kilichofanyika ndani ya utawala wa Dk Magufuli ilikuwa ni historia ya kipekee kwani awamu zote za viongozi waliopita hapa nchini hakukuwa na kiongozi aliyefanya uwekezaji mkubwa eneo alilotoka.

Mbali na uwekezaji walioutaja kuwa na dalili zote za ubinafsi alioufanya kiongozi huyo, amesema upo ukandamizaji mkubwa alioufanya kwenye jamii na kutoa kauli zenye vitisho kuonyesha hakuna aliye juu yake.

"Kama mnafikiri mpo huru kiasi hicho watch it,"Kauli hayati Dk Magufuli enzi ya uhai wake ambaye imeleta tafsiri kwenye kitabu hicho namna ambavyo uongozi wake haukutetereshwa na kitu chochote.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
Ukiuliza kwanini fedha nyingi zilipelekwa Chato utajibiwa kwani Chato ipo Sudan.

Matendo ya Magufuli na kauli zake za kifedhuli ikiwemo ile aliyoitoa kwa Waanga wa tetemeko la ardhi Bukoba ni sababu tosha ya kutengeneza Katiba mpya.

Katika kipindi cha miaka 5 Magufuli alipendelea Wilaya yake ya Chato kuliko kitu chochote.
 
..hakuna haja ya kufurumusha matusi.

..watetezi wa Magufuli nao waandike kitabu.

..waandishi wote waliokuwa wakimsifu na kumpamba Magufuli wakati akiwa hai wako wapi?

..Musiba, Kabudi, Makonda, etc wanasubiri nini kunyanyua kalamu zao kuandika kuhusu Magufuli?
Upo sahihi kabisa. Wasomaji tupo. Tutavinunua vyote na kuvisoma
 
Back
Top Bottom