Freeman Mbowe: Misimamo ya Serikali kuhusu Corona inaathiri wengi

Freeman Mbowe: Misimamo ya Serikali kuhusu Corona inaathiri wengi

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,541
Reaction score
139,848
​
D603F3C8-D024-4619-9AC0-6784B568B4B7.jpeg

Yetu macho

====
Alichokiandika Mbowe

Msimamo wa JPM na Serikali yake kuhusu #COVID19 ni aibu na jinai kubwa dhidi ya ubinadamu yenye athari kwa maisha & uchumi. Corona Tz ipo tele. Waso-hatia wanakufa. Woga & ukimya ni ujinga. Madaktari na wauguzi mna kiapo. Semeni ukweli. Kataeni uharamia huu. #Tanzanialivesmatter
 
Mimi namshauri Freema Alkael Mbowe aiache serikali ifanye kazi, maana yeye na chama chake wametuchelewesha sana.

KUWATETEA WATANZANIA NI KUJITAFUTIA MATATIZO YASIYO YA LAZIMA.

Yaache yafe mkuu. Corona imeondolewa kwa maombi ya mtakatifu Jiwe.

MITANO TENA JAMANI.
 
Kwa kuzingatia maambukizi ya corona kwenye nchi zilizoendelea, tahadhari zilizochukuliwa na mafanikio ya tahadhari hizo, idadi ya wagonjwa na idadi ya vifo vya corona kwenye nchi hizo Mbowe aje na ushauri nini kifanyike.

Wakati tunatoa lawama tuwe na solutions pia, ziwe zile zilizofaulu kupambana na hii corona bila kuiathiri jamii na kupelekea watu kufa kwa presha, sukari kupanda, njaa na upweke
 
Mbowe sema ukweli, hali ingekuwa kama unavyodhani basi watanzania leo wangekuwa wanaongelea hadithi nyingine.

Muheshimiwa unaisemea hii Covid19 inayosumbua dunia au unaongelea ugonjwa ambao unafanana na Malaria kwamba Malaria ipo na watu kila siku ukienda hospital unakuta wanaumwa Malaria.

Ahhhhh, siasa isiwe siasani mzee.
 
Covid 19 ipo sana, bado wataalam wa afya hawajabaini njia sahihi za kukabiliana nao.

Tuendelee na tahadhari zilizokwisha tolewa na wataalamu.

Magufuli anabeza wavaa barakoa mara nyingi, hii ni hatari sana. Aambiwe!
 
Back
Top Bottom