Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Mbowe must go...!
Kuna mambo yanajirudia kila wakati mpaka yanachosha. Unapokaribia uchaguzi ndani ya Chadema kuna maneno kuhusu Mbowe lazima uyasikie

– Mbowe anajilipa ruzuku yote. Kateka mali zote za chama. Mbowe anaendesha chama kama ofisi binafsi.n.k

Maneno haya yanajirudia kila msimu wa uchaguzi wa chama hicho.

Tuliyasikia wakati wa Chacha Wangwe. Wakati wa Zitto Kabwe. Sasa Kigogo wa ‘twita’ anayarudia kwa namna ileile. Kwa mwenye akili timamu hii inachosha.

Kama hizi ndiyo propaganda basi hizi ni za kipumbavu. Kichekesho zaidi ni wanaozitumia kushindwa kuelewa kuwa hazina mashiko. Uchaguzi wao ukiisha na haya maneno yanaisha.

Tuwekane sawa kwenye hili. Chama kinachopigania ukombozi au kutaka kushika dola, kikipata kiongozi imara hakimbadilishi ovyoovyo. Hii ni ‘prinsipo’. Yasser Arafat kafa akiwa kiongozi wa PLO kwa miaka mingi kule Palestina.

Dunia nzima, kiongozi wa namna hii huondolewa kwa kushindwa kustawisha chama na si vinginevyo. Huyu ndiye Mbowe.

Ukiwa na kiongozi asiye na msimamo mtaishia kuwa na vyama visivyosikika. Akili za Mbowe, msimamo wake, uchumi wake. Ndiyo yaliyopelekea akute chama kina wabunge watano na sasa wako sabini.

Unamuondoaje? Labda kama huna nia ya kushika dola. Propaganda za kula ruzuku lazima zife kibudu.

Kuna watu wakisikia shamba la Mbowe limeharibiwa na DC wanawaza matembele, nyanya chungu, sukuma wiki, kabeji na matuta ya viazi – wanalifananisha na mashamba ya bibi na babu zao huko Mpwapwa au Malinyi kama siyo Matombo.

Tunatakiwa kumshangaa Mbowe kuacha utajiri chekwa wa familia yake na kuja kuhangaika na siasa huku mitaani na kina Sugu.

Mwanzoni watu walikuwa ‘bize’ na Kigogo huko ‘twitani’. Kuna wakati akataka aniteke kiakili na mimi. Lakini kuanzia kwenye suala la ‘flash’ za ajali ya yule kigogo wa ukweli. Nikaanza kupata shaka. Ni sampuli ya watu wanaoamua kujipa nafuu ya nafsi zao kwa kuandika wanachojisikia.

Lowassa, aliitwa fisadi kila siku. Watu wakachoka kuona mtu mmoja anabebeshwa zigo lote la ufisadi. Kwanini hashtakiwi? Kwanini sasa hafungwi? Maswali yasiyo na jibu yalipelekea ageuke shujaa 2015.

Ndiyo Mbowe, shutuma anazopewa mbona Msajili wa vyama na CAG hawajawahi kusema lolote? Hata wapinzani wa Mbowe wamechoshwa nazo.

Tufanye siasa safi, zenye tija na manufaa kwa nchi. Hizi za ovyo ni upuuzi.

#Mbowe Tano Tena#
 
Sawa sina access na kura na nyie wenye nayo ni beneficiaries kwa mbowe kuendelea kuwa chair na mko mfukoni mwake na kwamba yeyote anayepinga ni lumumba. This time huo upuuzi hautafanikiwa, rest assured nyie wote wenye access kuwa this time mwenyekiti wa cdm ni Tundu Lissu
[/QUOTE]
Nimeshakuonya tena mbinu mnayodhani mnaweza kumtenga Mbowe na Lissu mnajidanganya sana.Lissu anajua waliomwokoa na waliotaka kumtoa uhai
 
Sawa mh Mbowe kwa kujifagilia!!

Kwa hiyo kwa wanachama woooote wa CDM Mbowe pekee ndiye mwenye uwezo wa kuongoza na kukuza chama. Hakuna mwanachama hata m1 mwenye uwezo km wa Mbowe au hata zaidi ya Mbowe ktk wanachama wote wa CDM?

Huoni kama hayo ni matusi na dharau kwa wana CDM ambao ni wengi na wapo wenye elimu zaid ya Mbowe?

Elewa hata hao viongozi wa ukombozi uliyowatolea mfano waliongoza vyama vyao kwa mda mrefu wakati nchi zao zina wasomi wachache. Je kwa CDM unaweza kusema wasomi ni wachache?

ACHA HAYO MATUSI YA REJA REJA
Kwa akili yako ndogo unadhani kuwa na elimu kubwa ndiyo kuwa kiongozi bora.

Mbowe hana mbadala kwa sasa ndani ya chama.
 
Sasa hapa hoja yako ni nini? Km we ni paid troll wa mbowe basi mbowe hana tofauti na chakubanga based on types of trolls they recruit, low iq bots. By the way chakubanga aweza pia kuwa mwenyekiti wa cdm km ambapo lowassa amekuwa mgombea uraisi wa cdm baadaya kukatwa kule na chakubanga.
Eti na wewe unaweka vijimaneno vya kimombo uonekane unajua...

Ha Ha Haaa
 
Tatizo la chadema linaanzia kwa wanachama wenyewe hadi kwa viongozi wao, mfano mbowe angeweza shauriwa na miongoni mwa wanachama akae pembeni awapishe wengine huku yeye akiendelea kuwa mshauri Mkuu Wa ndani ya chama, kiukweli kwa mtazamo wangu chadema inahitaji reform ya ndani, nadeclare interest sio mshabiki Wa chama chochote ila napenda changes kwenye nchi yetu pendwa.
Huna lolote wewe.Tukana CDM mkono uende kinywani
 
Achana na majuha ya lumumba sisi Kama chama [taasisi] Hatuna muda wa kuhangaika na walioshindwa kwanini wasihangaike na mambo ambayo yanamasilah kwao Mali zetu watanzania zinasombewa Chato wao na chadema tu
 
Kwanini usitake mwenyekiti wa chama chako akae pembeni badala yake unataka mkiti wa chama kingine usichokipenda akae pembeni?

Siko cdm kwa bahati mbaya, na sina maslahi binafsi na kiongozi bali chama. Ccm nimeiona toka nikiwa mtoto na wala sijawahi kuitamani, isitoshe mimi sio wa hizo siasa za maneno ya rejareja kwamba nikiweka wazi msimamo wangu basi ni ccm, kana kwamba kila aliye cdm lazima atake Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti.

Narudia tena, jitahidi kuijenga cdm kama taasisi na sio cdm kama mali ya Mbowe. Nimekuwekea mpaka mifano ya wazi kuwa Mbowe kukaa madarakani miaka 15 kunatosha, na sasa chama hakipandi tena bali kimesimama kwa sababu ya hujuma za rais, huku yeye akiwa amegota kwenye mbinu za kujinasua. Sana sana ninachokiona kwenye uongozi wake toka sasa, ni chama kushuka kilipokuwa badala ya kupanda. Ww weka ushabiki wa kijinga kisa unafaidika na cheo cha Mbowe, lakini kwa hujuma za wazi wazi za rais dhidi ya cdm sioni cdm ikipata viti vingi vya uwakilishi, kwani hata hizo hujuma za mpaka sasa tumeshindwa kwenda mahakamani, na nguvu ya umma iliyokuwa tegemeo letu nayo imeingia woga, na ikithubutu ndio kama yale yaliyopelekea kifo cha Akwillina na viongozi wetu ndio wenye kesi!
 
IMG-20190928-WA0027.jpg
IMG-20190928-WA0025.jpg
 

Attachments

  • VID-20190922-WA0020.mp4
    4.8 MB
Naunga mkono hoja aungwe mkono hadi 2020 ipite ili tupate ona kuwa nguvu bado au imepungua kwa idadi ya wabunge atakaosaidia kuingia bungeni kutoka hawa 70 kwenda mbele au kushuka toka 70 kurudi nyuma...
Apewe nafasi baada ya uchaguzi anaweza kujiuzuru...
 
Siko cdm kwa bahati mbaya, na sina maslahi binafsi na kiongozi bali chama. Ccm nimeiona toka nikiwa mtoto na wala sijawahi kuitamani, isitoshe mimi sio wa hizo siasa za maneno ya rejareja kwamba nikiweka wazi msimamo wangu basi ni ccm, kana kwamba kila aliye cdm lazima atake Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti.

Narudia tena, jitahidi kuijenga cdm kama taasisi na sio cdm kama mali ya Mbowe. Nimekuwekea mpaka mifano ya wazi kuwa Mbowe kukaa madarakani miaka 15 kunatosha, na sasa chama hakipandi tena bali kimesimama kwa sababu ya hujuma za rais, huku yeye akiwa amegota kwenye mbinu za kujinasua. Sana sana ninachokiona kwenye uongozi wake toka sasa, ni chama kushuka kilipokuwa badala ya kupanda. Ww weka ushabiki wa kijinga kisa unafaidika na cheo cha Mbowe, lakini kwa hujuma za wazi wazi za rais dhidi ya cdm sioni cdm ikipata viti vingi vya uwakilishi, kwani hata hizo hujuma za mpaka sasa tumeshindwa kwenda mahakamani, na nguvu ya umma iliyokuwa tegemeo letu nayo imeingia woga, na ikithubutu ndio kama yale yaliyopelekea kifo cha Akwillina na viongozi wetu ndio wenye kesi!
Maandishi yako yanaonyesha wazi una chuki kubwa na CDM.Hatutadanganyika na porojo zako
 
Chadema mnafanya kosa lingine kubwa baada ya lile la kumpokea Lowasa 2015, kwa kuivuruga katiba yenu wenyewe ya chama!

Mkiendelea kukaza shingo na kulazimisha Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti wa maisha wa chama, ile dhana ya Demokrasia mnayotuhubiria itapoteza uelekeo! na hivyo mtatengeneza mazingira kwa wapinzani wenu kumfanya magufuli naye kuwa Rais wa maisha

Chonde chonde, fanyeni uchaguzi kwa mujibu wa katiba yenu ya chama. Msiifanye chadema kama TLP ya Mrema, CUF ya Lipumba, UDP ya Cheyo, DP ya marehemu Mtikila, nk. Mtaturudisha sana nyuma wapenda mabadiliko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom