Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Kuna mambo yanajirudia kila wakati mpaka yanachosha. Unapokaribia uchaguzi ndani ya Chadema kuna maneno kuhusu Mbowe lazima uyasikie

– Mbowe anajilipa ruzuku yote. Kateka mali zote za chama. Mbowe anaendesha chama kama ofisi binafsi.n.k

Maneno haya yanajirudia kila msimu wa uchaguzi wa chama hicho.

Tuliyasikia wakati wa Chacha Wangwe. Wakati wa Zitto Kabwe. Sasa Kigogo wa ‘twita’ anayarudia kwa namna ileile. Kwa mwenye akili timamu hii inachosha.

Kama hizi ndiyo propaganda basi hizi ni za kipumbavu. Kichekesho zaidi ni wanaozitumia kushindwa kuelewa kuwa hazina mashiko. Uchaguzi wao ukiisha na haya maneno yanaisha.

Tuwekane sawa kwenye hili. Chama kinachopigania ukombozi au kutaka kushika dola, kikipata kiongozi imara hakimbadilishi ovyoovyo. Hii ni ‘prinsipo’. Yasser Arafat kafa akiwa kiongozi wa PLO kwa miaka mingi kule Palestina.

Dunia nzima, kiongozi wa namna hii huondolewa kwa kushindwa kustawisha chama na si vinginevyo. Huyu ndiye Mbowe.

Ukiwa na kiongozi asiye na msimamo mtaishia kuwa na vyama visivyosikika. Akili za Mbowe, msimamo wake, uchumi wake. Ndiyo yaliyopelekea akute chama kina wabunge watano na sasa wako sabini.

Unamuondoaje? Labda kama huna nia ya kushika dola. Propaganda za kula ruzuku lazima zife kibudu.

Kuna watu wakisikia shamba la Mbowe limeharibiwa na DC wanawaza matembele, nyanya chungu, sukuma wiki, kabeji na matuta ya viazi – wanalifananisha na mashamba ya bibi na babu zao huko Mpwapwa au Malinyi kama siyo Matombo.

Tunatakiwa kumshangaa Mbowe kuacha utajiri chekwa wa familia yake na kuja kuhangaika na siasa huku mitaani na kina Sugu.

Mwanzoni watu walikuwa ‘bize’ na Kigogo huko ‘twitani’. Kuna wakati akataka aniteke kiakili na mimi. Lakini kuanzia kwenye suala la ‘flash’ za ajali ya yule kigogo wa ukweli. Nikaanza kupata shaka. Ni sampuli ya watu wanaoamua kujipa nafuu ya nafsi zao kwa kuandika wanachojisikia.

Lowassa, aliitwa fisadi kila siku. Watu wakachoka kuona mtu mmoja anabebeshwa zigo lote la ufisadi. Kwanini hashtakiwi? Kwanini sasa hafungwi? Maswali yasiyo na jibu yalipelekea ageuke shujaa 2015.

Ndiyo Mbowe, shutuma anazopewa mbona Msajili wa vyama na CAG hawajawahi kusema lolote? Hata wapinzani wa Mbowe wamechoshwa nazo.

Tufanye siasa safi, zenye tija na manufaa kwa nchi. Hizi za ovyo ni upuuzi.

#Mbowe Tano Tena#
Mungu mbariki Freeman Mbowe , Jabali la kisiasa , mwamba usiotikisika , Hakuna kinyangarika chochote kutoka ccm anayeweza kupambana na mtu huyu , msaada wao mkubwa ni polisi .
 
nakumbuka Majimarefu na Mwinyi walisema kwa kuwa utendaji kazi wa Rais ni mzuri na ni wa kizalendo, ikiwezekana aendelee kuongoza miaka kumi zaidi baada ya mda wake kuisha..

nakumbuka wanaCHADEMA walilaani sana hizo kauli na wakasema huo utakua ni UDIKTETA.

Kama hili la Rais kuongezewa muda lilionekana ni UDIKTETA, hili la MBOWE tuliitaje?

Kama hili la Rais ni gumu kutekelezeka basi na hili la MBOWE kuongezewa muda nalo lisitekelezeke.

CHADEMA wanachukulia advantage chuki ya wananchi dhidi ya CCM, kwahio wanajiposition kama wakombozi wa nchi.

Kwa mimi nnavojua, mwanaume akimchoka mwanamke anatafuta mwanamke bora zaidi ya huyu aliemchoka..
sasa kama mwanamke aliedhaniwa ndio atakua mrithi wa nafasi ya mwenzake na yeye anaanza kuonyesha tabia chafu, ni mara mia mwanaume abaki kwa huyu alie nae.

Unafiki unatutafuna sana waTz.
 
Mimi naona tuige mambo mazuri ya Chadema, JPM tumuongeezee muhula agombee bila kikomo
Ni kweli kabisa kama chama cha mapinduzi kikiiga CDM kumuongezea Mwenyekiti wake muda wa kuongoza chama.Ni jambo jema sana
 
nakumbuka Majimarefu na Mwinyi walisema kwa kuwa utendaji kazi wa Rais ni mzuri na ni wa kizalendo, ikiwezekana aendelee kuongoza miaka kumi zaidi baada ya mda wake kuisha..

nakumbuka wanaCHADEMA walilaani sana hizo kauli na wakasema huo utakua ni UDIKTETA.

Kama hili la Rais kuongezewa muda lilionekana ni UDIKTETA, hili la MBOWE tuliitaje?

Kama hili la Rais ni gumu kutekelezeka basi na hili la MBOWE kuongezewa muda nalo lisitekelezeke.

CHADEMA wanachukulia advantage chuki ya wananchi dhidi ya CCM, kwahio wanajiposition kama wakombozi wa nchi.

Kwa mimi nnavojua, mwanaume akimchoka mwanamke anatafuta mwanamke bora zaidi ya huyu aliemchoka..
sasa kama mwanamke aliedhaniwa ndio atakua mrithi wa nafasi ya mwenzake na yeye anaanza kuonyesha tabia chafu, ni mara mia mwanaume abaki kwa huyu alie nae.

Unafiki unatutafuna sana waTz.
Chadema haina nafasi wala uwezo wa kukiamulia chama cha Mapinduzi kuhusu viongozi wake.Mwenyekiti wa CCM hata akiongoza chama chake miaka 20 ni sawa tu
 
Chadema haina nafasi wala uwezo wa kukiamulia chama cha Mapinduzi kuhusu viongozi wake.Mwenyekiti wa CCM hata akiongoza chama chake miaka 20 ni sawa tu
point ni kwamba kuendelea kuwa madarakani angali mda wa uongozi umeisha ni ishara ya UDIKTETA.

kama ni sawa MBOWE kuendelea kuwa Mwenyekiti basi ni sawa hata sisi waTz tukiamua Rais aendelee tu.

huu ung'ang'anizi wa madaraka mnaoutetea kwenye ngazi ya chama hata mkipata nchi mtauendeleza tu.
 
Mungu mbariki Freeman Mbowe , Jabali la kisiasa , mwamba usiotikisika , Hakuna kinyangarika chochote kutoka ccm anayeweza kupambana na mtu huyu , msaada wao mkubwa ni polisi .
Mbowe ni Jabali la kisiasa Tanzania
 
point ni kwamba kuendelea kuwa madarakani angali mda wa kiongizi umeisha ni ishara ya UDIKTETA.

kama ni sawa MBOWE kuendelea kuwa Mwenyekiti basi ni sawa hata sisi waTz tukiamua Rais aendelee tu.

huu ung'ang'anizi wa madaraka mnaoutetea kwenye ngazi ya chama hata mkipata nchi mtauendeleza tu.
Nafasi ya Mbowe ni sawa na Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM.Mbowe si Rais wa nchi hivyo siwezi kulinganisha nafasi yake na ya Urais.Ni vitu viwili tofauti.Ni sawa na mbingu na ardhi
 
Mbona hatujawahi kuwasikia mnamuuliza Lyatonga kwamba uchaguzi wanafanya lini?

vilivyokufa huwa haviuliziwi

mbowe akiwa chairman miaka 5 ijayo no one will care asking kuhusu chadema

nitakukumbusha
 
vilivyokufa huwa haviuliziwi

mbowe akiwa chairman miaka 5 ijayo no one will care asking kuhusu chadema

nitakukumbusha
Na hatuhitaji mwanaccm yeyote kuulizia mambo ya Chadema.Yanawahusu nini labda?
 
Uwezo wa Mbowe kutuongoza umekwisha na hivyo ni bora kuwa na kichwa kingine
 
Kinakuuma nini? Mbona wewe uko kupata mkate wako kutoka CCM.?

sio kweli

unathibitisha my hypothesis

pambana njaa mbaya

sina chama tangu nilipoondoka chenu 2006'kwa kumbukumbu hizi hizi
 
sio kweli

unathibitisha my hypothesis

pambana njaa mbaya

sina chama tangu nilipoondoka chenu 2006'kwa kumbukumbu hizi hizi
Na tangu ulipoanza kutukana kuchafua na kukashifu CDM tangu 2006 umefanikiwa nini?

Kila uchaguzi wa CDM si umekuwa ukitabiri CDM itakufa ikimchagua Mbowe?

Haya mwenzetu mjuaji na hypothesis zako feki CDM imekufa kwa kumchagua Mbowe tangu 2006?

Usiwe kama Kanga anayeficha kichwa huku mwili wote ukiwa nje
 
Kwa mlivyo na usongo na husuda na cdm naamini dua zenu ni kuona cdm inazikwa hata leo kama alivyo oteshwa Dada yenu Tulia kule mbeya
vilivyokufa huwa haviuliziwi

mbowe akiwa chairman miaka 5 ijayo no one will care asking kuhusu chadema

nitakukumbusha
tapatalk_1569129196473.jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom