Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Kuna mambo yanajirudia kila wakati mpaka yanachosha. Unapokaribia uchaguzi ndani ya Chadema kuna maneno kuhusu Mbowe lazima uyasikie

– Mbowe anajilipa ruzuku yote. Kateka mali zote za chama. Mbowe anaendesha chama kama ofisi binafsi.n.k

Maneno haya yanajirudia kila msimu wa uchaguzi wa chama hicho.

Tuliyasikia wakati wa Chacha Wangwe. Wakati wa Zitto Kabwe. Sasa Kigogo wa ‘twita’ anayarudia kwa namna ileile. Kwa mwenye akili timamu hii inachosha.

Kama hizi ndiyo propaganda basi hizi ni za kipumbavu. Kichekesho zaidi ni wanaozitumia kushindwa kuelewa kuwa hazina mashiko. Uchaguzi wao ukiisha na haya maneno yanaisha.

Tuwekane sawa kwenye hili. Chama kinachopigania ukombozi au kutaka kushika dola, kikipata kiongozi imara hakimbadilishi ovyoovyo. Hii ni ‘prinsipo’. Yasser Arafat kafa akiwa kiongozi wa PLO kwa miaka mingi kule Palestina.

Dunia nzima, kiongozi wa namna hii huondolewa kwa kushindwa kustawisha chama na si vinginevyo. Huyu ndiye Mbowe.

Ukiwa na kiongozi asiye na msimamo mtaishia kuwa na vyama visivyosikika. Akili za Mbowe, msimamo wake, uchumi wake. Ndiyo yaliyopelekea akute chama kina wabunge watano na sasa wako sabini.

Unamuondoaje? Labda kama huna nia ya kushika dola. Propaganda za kula ruzuku lazima zife kibudu.

Kuna watu wakisikia shamba la Mbowe limeharibiwa na DC wanawaza matembele, nyanya chungu, sukuma wiki, kabeji na matuta ya viazi – wanalifananisha na mashamba ya bibi na babu zao huko Mpwapwa au Malinyi kama siyo Matombo.

Tunatakiwa kumshangaa Mbowe kuacha utajiri chekwa wa familia yake na kuja kuhangaika na siasa huku mitaani na kina Sugu.

Mwanzoni watu walikuwa ‘bize’ na Kigogo huko ‘twitani’. Kuna wakati akataka aniteke kiakili na mimi. Lakini kuanzia kwenye suala la ‘flash’ za ajali ya yule kigogo wa ukweli. Nikaanza kupata shaka. Ni sampuli ya watu wanaoamua kujipa nafuu ya nafsi zao kwa kuandika wanachojisikia.

Lowassa, aliitwa fisadi kila siku. Watu wakachoka kuona mtu mmoja anabebeshwa zigo lote la ufisadi. Kwanini hashtakiwi? Kwanini sasa hafungwi? Maswali yasiyo na jibu yalipelekea ageuke shujaa 2015.

Ndiyo Mbowe, shutuma anazopewa mbona Msajili wa vyama na CAG hawajawahi kusema lolote? Hata wapinzani wa Mbowe wamechoshwa nazo.

Tufanye siasa safi, zenye tija na manufaa kwa nchi. Hizi za ovyo ni upuuzi.

#Mbowe Tano Tena#
Umeona jinsi watu hawalali, kisa jembe lipo imara pamoja na swaga zao.
Chadema Isije ikafanya kosa kumtoa Mbowe pale, Kwasasa Mbowe anahitajika kuliko wakati wowote.
 
Umeona jinsi watu hawalali, kisa jembe lipo imara pamoja na swaga zao.
Chadema Isije ikafanya kosa kumtoa Mbowe pale, Kwasasa Mbowe anahitajika kuliko wakati wowote.
Usiwe na shaka mkuu.Tuko macho na hatutaruhusu hilo kutokea
 
Chadema mnafanya kosa lingine kubwa baada ya lile la kumpokea Lowasa 2015, kwa kuivuruga katiba yenu wenyewe ya chama!

Mkiendelea kukaza shingo na kulazimisha Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti wa maisha wa chama, ile dhana ya Demokrasia mnayotuhubiria itapoteza uelekeo! na hivyo mtatengeneza mazingira kwa wapinzani wenu kumfanya magufuli naye kuwa Rais wa maisha

Chonde chonde, fanyeni uchaguzi kwa mujibu wa katiba yenu ya chama. Msiifanye chadema kama TLP ya Mrema, CUF ya Lipumba, UDP ya Cheyo, DP ya marehemu Mtikila, nk. Mtaturudisha sana nyuma wapenda mabadiliko.
Hujitambui na hujui kutofautisha kati ya nchi na chsma cha siasa
 
Maandishi yako yanaonyesha wazi una chuki kubwa na CDM.Hatutadanganyika na porojo zako

Naona najadiliana na mtu mwenye mtazamo mdogo lakini uliyeshiba mahaba kwa Mbowe na sio chama. Pia naona unashindwa kutofautisha kati ya chama na cheo cha Mbowe. Sina popote nilipokituhumu chama au kuwa na chuki nacho, labda uweke wazi ni wapi, mjadala wetu hapa ni Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti, na sina popote nilipomtaja kwa chuki zaidi ya kusema muda wa yeye kukaa madarakani miaka 15 kunatosha ampishe mwingine. Je nikisema hili kwako ni chuki kubwa dhidi ya cdm au Mbowe? Uzuri nimeweka na sababu hasa ni kwanini sasa ampe mwingine kijiti, ukiachia muda mrefu aliokalia kiti.

Jitahidi usiwe na mahaba mazito kwa mtu badala ya chama, mpaka uanze kujenga hoja za kulazimisha ili kupotosha ukweli. Ww kunitaja mimi kuwa mwanaCCM au kunikejeli hakuboreshi hoja za utetezi wako dhidi ya Mbowe. Nina hoja za kutosha za kitaasisi kuwa sasa ni muda muafaka wa Mbowe kukaa pembeni iwapo kweli cdm ni taasisi, ni sidhani utetezi wa kuwa anayesema muda wa Mbowe kuhudumu kama mwenyekiti huyo ni ccm ni utetezi wa maana.
 
Kwa kifupi hakuna mjadala na hatutaruhusu mjadala wa uenyekiti CDM.Hilo hatuliruhusu Pole sana.

Labda tuweke hoja za nani wanaoweza kumsaidia Mbowe katika miaka yake mingine mitano ijayo.

Tutakuwa wakali kidogo kwenye hilo
 
Umeona jinsi watu hawalali, kisa jembe lipo imara pamoja na swaga zao.
Chadema Isije ikafanya kosa kumtoa Mbowe pale, Kwasasa Mbowe anahitajika kuliko wakati wowote.

Bila shaka muda si mrefu tutakuwa na CHADEMA ya Mbowe, TLP ya Mrema, CUF ya Lipumba, UDP ya Cheyo, ACT Wazalendo ya Zitto, CCM ya Magufuli, nk. Kweli siasa za Tanzania ni ujasiriamali tosha.
 
Bila shaka muda si mrefu tutakuwa na CHADEMA ya Mbowe, TLP ya Mrema, CUF ya Lipumba, UDP ya Cheyo, ACT Wazalendo ya Zitto, Ccm ya Magufuli, nk. Kweli siasa za Tanzania ni ujasiriamali tosha.
Songa ugali ule upumzike.Siasa waachie wenye uwezo nazo.

Mbowe Tano Tena
 
Kwa kifupi hakuna mjadala na hatutaruhusu mjadala wa uenyekiti CDM.Hilo hatuliruhusu Pole sana.

Labda tuweke hoja za nani wanaoweza kumsaidia Mbowe katika miaka yake mingine mitano ijayo.

Tutakuwa wakali kidogo kwenye hilo

Kama hamruhusu mjadala wa uenyekiti wa cdm hukupaswa hata kuuleta huu mjadala hapa jukwaani, mngeendelea tu na utekelezaji. Lakini ukweli uko hivi, sio ww, Mbowe au mwanacdm yoyote anayeweza kujenga hoja kwanini Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa cdm, huku akiwa ameshakuwa kwenye nafasi hiyo kwa miaka 10+. Tena hivi karibuni akiwa amefanya kosa kubwa na kuokota mgombea toka ccm aliyekuja kusaka madaraka, na baada ya kuyakosa akarudi tena huko huko ccm. Ni kichekesho kusema Mbowe au cdm inapambana na ccm huku hata mgombea wa urais tunaenda kuokoteza huko ccm, achia mbali wanaccm wengine waliokuja na kupewa nafasi bila kukitumikia chama.
 
Wanachama wengi katika dodoso langu nililozunguka nalo mikoani nchi nzima wanapendekeza walau Mbowe apewe miaka mingine 15 kisha ndiyo chama kifanye tathmini nyingine.

Ndiyo maana nikakuambia suala la uenyekiti wa Mbowe kwa sasa halina mjadala labda mpaka 2034
 
Mbowe Tano Tena

Ni kweli usemayo, ila atakuwa anaongoza cdm yenye nguvu kiasi gani hapo ndio mjadala ulipo. Naiona cdm niliyoikubali ikufubaa kwa kukosa hoja mbele ya umma. Molemo wala usijali, acha Mbowe awe mwenyekiti, halafu baada ya uchaguzi wa serekali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020 kama cdm bado itakuwa hii.
 
Kama ilivyofubaa tangu Mbowe achukue Uenyekiti
 
Mimi naona tuige mambo mazuri ya Chadema, JPM tumuongeezee muhula agombee bila kikomo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom