Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Mwanachama ambaye hajafikisha miaka 10 kwenye chama hawezi kuwa mwenyekiti wa chama chetu Taifa
 
Mwanachama ambaye hajafikisha miaka 10 kwenye chama hawezi kuwa mwenyekiti wa chama chetu Taifa
Ni lazima anayetaka uenyekiti wa chama Taifa awe ameiva kiitikadi na aliyekulia ndani ya chama na anayejua miiko ya chama.
 
Kwakuwa CCM wanakereka Mbowe kuendelea kuiongoza CHADEMA na mimi nitaendelea kuwakera kwa kumpa nafasi Mbowe aendelee kuiongoza CHADEMA
Asante sana.Chadema haiwezi kuchaguliwa kiongozi na maaduu zake
 
Anaenda masomoni nje
Mpk sasa Mbowe siyo Mwenyekiti wa CHADEMA na kwa vyovyote vile Ubunge Jimbo la Hai (2020- 2025) hawezi kuupata. Watu tumemchoka.

Atakuwa mshauri wa chama na mjumbe wa CC !
 
""Lakini bahati nzuri ni kwamba wapinzani wote wa Freeman wanatoka nje ya chama hicho na akitokea mtu kujifanya anampinga Mbowe akiwa chini ya Chadema ni wazi ni kibaraka mwenye lengo la kuvuruga umoja ndani ya chama.""
===============

Hii nukuu ndio nimeilewa zaidi kwamba kwa sasa yeyote atakaechukua fomu kupambana na Mbowe moja kwa moja ni msaliti.

Na kwamba Lissu anafaa ila sio leo wala kesho siku za mbeleni huko...

Moja kwa moja ni kwamba Mbowe hatoki leo wala kesho...
 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa Fukuto la uchaguzi mkuu wa ndani kwa chama kikuu na tishio cha upinzani nchini limepamba moto.

Vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali vimepambwa na habari hizi lakini hususani nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama anayetarajiwa kuchaguliwa Decemba mwaka huu.Ni nafasi muhimu sana kwani ndiyo inayoamua hatma ya chama kwa miaka mingine mitano.

Freeman Mbowe jabali la kisiasa Tanzania na tajiri mwenye ukwasi mkubwa aliyeamua kuweka starehe pembeni na kuitikia wito wa kuwakomboa wananchi kupitia chama alichoshiriki kukiasisi cha CHADEMA amekitumikia chama hicho kwa awamu 3 sasa na akitarajiwa kupata ushindi mkubwa kuongoza awamu nyingine ya nne hapo December.

Mafanikio ya Freeman Mbowe ndani ya CHADEMA yanahitaji vitabu na vitabu kuviandika kwani tunaweza kusema ni Mwenyekiti aliyewezesha chama alichokiongoza kupata mafanikio makubwa zaidi kwa Tanzania tangu mfumo wa vyama vingi uanze 1992.

Freeman Mbowe anao wapinzani wake wanaotaka aondoke madarakani hata leo na asipewe nafasi nyingine kabisa ya kukiongoza chama hicho.Lakini bahati nzuri ni kwamba wapinzani wote wa Freeman wanatoka nje ya chama hicho na akitokea mtu kujifanya anampinga Mbowe akiwa chini ya Chadema ni wazi ni kibaraka mwenye lengo la kuvuruga umoja ndani ya chama.Tumeshuhudia hivi karibuni waasi wachache wabunge walioanza kumtukana Freeman na baada ya muda mchache wote wakaunga mkono juhudi na kujiunga na CCM.

Wengine tunajiuliza kwanini wasiomtaka Freeman watoke nje ya chama hicho? Kwamba wanaoipenda Chadema ni wanaCCM na vibaraka wao? Ili iweje??

Tutarajie kushuhudia makubwa zaidi kuelekea uchaguzi mkuu wa chama mwishoni mwa mwaka huu.Tusishangae kuona maadui wa Chadema wakitumia kila njia kutaka kuichagulia Chadema kiongozi.Na kila adui wa Chadema ombi lake ni moja Kwamba Mbowe Hafai na Asichaguliwe tena.Hiyo ndiyo kaulimbiu ya kila asiyeitakia mema Chadema.

Jambo la kumshukuru Mungu kwa sasa ndani ya Chadema wapo viongozi wengi watiifu kwa Katiba ya chama.Viongozi wengi wanaomtii na kumheshimu Freeman Mbowe kama Jabali la kisiasa Tanzania.Viongozi wanaoamini bila jitihada kubwa za Mbowe basi CDM ingekuwa katika kaburi la kisiasa leo hii kama CUF,NCCR,TLP na wengine.

Kati ya viongozi wengi wanaomtii na kumheshimu Mbowe nimtaje mmoja tu Tundu Antipas Mughwai Lissu.Hakuna asiyemjua jemedari huyu ambaye pamoja na usomi wake na umaarufu wake duniani kote Lakini kila azungumzapo hakosi kumtaja na kumpa heshima Freeman Mbowe kwamba ni Profesa wa upinzani Tanzania.

Kwamba kwa aliyopitia na heshima na uvumilivu wake kwa Chama chake basi anastahili siku moja kuvikwa Taji.Kwamba ni Hazina ndani ya Chadema.Kwamba ni Hazina ndani ya nchi.Kwamba siku moja miaka ijayo anafaa kabisa kuchukua mikoba.Kwamba anastahili kabisa kuwa mbadala wa Jabali la kisiasa Tanzania.Heshima nyingi zimwendee Tundu Lissu.

Nimalizie kwa kusema bado tunamhitaji Freeman Mbowe walau kwa miaka mingine mitano.

#Mbowe Tano Tena#

Mbowe achukue hata 100yrs again kama katiba inaruhusu lakini!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom