Habari.
Kwa masikitiko makubwa nimepewa taarifa kutoka ndani ya Chadema kwamba ,baada ya msajili wa vyama vya siasa kuiandikia Chadema ijieleze kwa nini hawafanyi uchaguzi wa mwenyekiti wa chama kinyume na katiba ya chama ,sasa Mbowe ameanza kuhaha!!
Kinyume kabisa na katiba ya chama na ni uvunjwaji mkubwa wa katiba ya chama kinachojiita cha kidemocrasia nchini ,sasa Freeman Mbowe amesambaza vijana mitandaoni wanaoendesha kampeni ya ## mbowe 5 tena#, Lengo kubwa la kampeni hii ni kumfanya Mbowe aonekane anakubalika sana ndani ya chama na awe mwenyekiti wa milele !!
Ukweli ni kwamba Mbowe tangu alipokiuza chama kwa Lowasa hakubaliki tena ndani ya chadema kwa sasa ndiyo maana kuna kundi la wabunge wamekataa kuchangia chama kila mwezi.
Vijana mliosambazwa mitandaoni mkae mjiulize je Mbowe ndiyo ana akili pekee ya kuiongoza chadema hamna mwingine? Na kama jibu ni ndiyo basi ili kukamilisha huo udikteta ondoeni neno democrasia kwenye chama chenu.
View attachment 1225084
Tunataka mabadilikooo ndiyo maana wabunge wa chadema wamekataa kuchangia chamaEtwege nina maswali au ushauri 2 kwako
1. Kama kuna kitu mnatakiwa kushukuru sana ni Mbowe kuendelea kuwa madarakani. Mbowe amekuwa na siasa za ukimya sana na hadi kufikia hatua ya kulaumiwa na watu wake kwanini anajishusha sana na kuendekeza 'Busara' kwenye maamuzio yake. Wamekuwa wanaomba wapatiwe mtu kichaa ambae anaweza simama kusema kesho vijana wa chadema nchi nzima waingie barabarani! Amini usiamini mnatakiwa mshukuru sana uwepo wa Mbowe na sio kumbeza kwa mustakabali wa CCM na nchi yetu kwa ujumla. Msiamini sana kuwa mna nguvu ya dola na Polisi, vinashindwaga hivi vitu sometimes!
2. Mbowe alikiuza chama kwa Lowasa kama usemavyo, kwa sasa Lowasa karudi CCM na alipokelewa kwa shangwe na mwenyekiti wako, ni pia CCM imeuzwa kwa Lowasa? Nadhani baada ya Lowasa kurudi CCM mlitakiwa mfute kabisa hizi kauli zenu kuwa kuna kununua chama. Mchukulieni Lowasa kama malaya' wa kisiasa kama walivyo wengine tu ambao wanaangalia maslahi yao kwanza
3. Tuchukulie ni kweli kuwa MBowe anahamasisha vijana kuonesha bado anahitajika. Lakini si ndio mambo ya uchaguzi yalivyo mkuu. Mmekuwa mnalilia sana ufanyike uchaguzi Chadema, sasa katiba yao inaruhusu Mbowe kugombea na kufanya kampeni kwanini inakuwa dhambi akifanya mikakati yake. Nadhani tuwaache waamue jinsi wanavyotaka wao,wanachama wakiona hafai hawatamchagua na wakiona anafaa watamchagua tu.
Mimi sina chama wala upenzi wa siasa ni mtanzania kwa kuzaliwa baba na mama!
Angalia haya mabadiliko yanaweza kuja na ugumu kwenu mkuu!Tunataka mabadilikooo ndiyo maana wabunge wa chadema wamekataa kuchangia chama
Barikiwa sana.Umeongea kwa Hekima kubwa sanaKama mwiba kwa ccm mh Mbowe baki. Tundu Lissu ni makini ila kwa sasa msimsumbue yuko kwenye mapito hivyo Mbowe hata ukifungwa endelea kuongoza CDM kwani uwepo wako hai bado tutakungoja tu
Hayo yenu hayatusumbui.Mnayo haki hiyo.Ila kwa Chadema ni Mbowe Tano TenaCHADEMA mmekuwa vipofu sana, ikiwa Mbowe ataongoza miaka yote kama mwenyekiti wenu, na sisi CCM tunaanza mchakato Mh. JPM abakie madarakani kwa miaka 20 ijayo.. Sbb sisi wananchi ndio tunaamua na sbb wananchi wengi ni CCM, tutaamua Mh. JPM aendelee kwa miaka walau 20 yaani mihula 4..
Mabadiliko haya ni takwa la katiba ya chama siyo hisani ya mtuAngalia haya mabadiliko yanaweza kuja na ugumu kwenu mkuu!
Sijakuelewa mkuuDah propaganda awamu hii imekuwa Kama hoja ya mgombea binafsi
Kwa hiyo wewe ni mke wa nani?Akili zenu ninyi wake wa Mbowe mnazijua wenyewe.
Haiwezekani kila mwanachama anayetaka kugombea uenyekiti mnamuundia zengwe la kutumika na Ccm.
Ina maana hamuwapiki makamanda wenu vizuri wakaiva?
Kwa nn kila wakati wao tu ndo hununuliwa?
Mbowe achia nafasi kwa ajili ya heshima yako uliyojiwekea
Kwakuwa CCM wanakereka Mbowe kuendelea kuiongoza CHADEMA na mimi nitaendelea kuwakera kwa kumpa nafasi Mbowe aendelee kuiongoza CHADEMA
Mabadiliko hayo kwa mujibu wa takwa hilo la katiba ni kuwa haruhusiwi kugombea tena?Mabadiliko haya ni takwa la katiba ya chama siyo hisani ya mtu