Freeman Mbowe aungwe mkono uchaguzi ndani CHADEMA

Mbowe mitano tena! Magufuli mitano 2020, mitano tena 2025, mitano tena 2030, mitano tena ...!
Hapa Tunazungumzia ya Mbowe na CDM.Hayo mengine anzishie uzi wake kama Katiba inaruhusu
 
ujinga kabisa..... eti mbowe kawakomboa wananchi??? ujinga kabisa........ mbowe kajikomboa yeye na familia yake na siyo wewe.....
Mtu wa CCM utaandika nini zaidi ya hiki?
 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa Fukuto la uchaguzi mkuu wa ndani kwa chama kikuu na tishio cha upinzani nchini limepamba moto.

Vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali vimepambwa na habari hizi lakini hususani nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama anayetarajiwa kuchaguliwa Decemba mwaka huu.Ni nafasi muhimu sana kwani ndiyo inayoamua hatma ya chama kwa miaka mingine mitano.

Freeman Mbowe jabali la kisiasa Tanzania na tajiri mwenye ukwasi mkubwa aliyeamua kuweka starehe pembeni na kuitikia wito wa kuwakomboa wananchi kupitia chama alichoshiriki kukiasisi cha CHADEMA amekitumikia chama hicho kwa awamu 3 sasa na akitarajiwa kupata ushindi mkubwa kuongoza awamu nyingine ya nne hapo December.

Mafanikio ya Freeman Mbowe ndani ya CHADEMA yanahitaji vitabu na vitabu kuviandika kwani tunaweza kusema ni Mwenyekiti aliyewezesha chama alichokiongoza kupata mafanikio makubwa zaidi kwa Tanzania tangu mfumo wa vyama vingi uanze 1992.

Freeman Mbowe anao wapinzani wake wanaotaka aondoke madarakani hata leo na asipewe nafasi nyingine kabisa ya kukiongoza chama hicho.Lakini bahati nzuri ni kwamba wapinzani wote wa Freeman wanatoka nje ya chama hicho na akitokea mtu kujifanya anampinga Mbowe akiwa chini ya Chadema ni wazi ni kibaraka mwenye lengo la kuvuruga umoja ndani ya chama.Tumeshuhudia hivi karibuni waasi wachache wabunge walioanza kumtukana Freeman na baada ya muda mchache wote wakaunga mkono juhudi na kujiunga na CCM.

Wengine tunajiuliza kwanini wasiomtaka Freeman watoke nje ya chama hicho? Kwamba wanaoipenda Chadema ni wanaCCM na vibaraka wao? Ili iweje??

Tutarajie kushuhudia makubwa zaidi kuelekea uchaguzi mkuu wa chama mwishoni mwa mwaka huu.Tusishangae kuona maadui wa Chadema wakitumia kila njia kutaka kuichagulia Chadema kiongozi.Na kila adui wa Chadema ombi lake ni moja Kwamba Mbowe Hafai na Asichaguliwe tena.Hiyo ndiyo kaulimbiu ya kila asiyeitakia mema Chadema.

Jambo la kumshukuru Mungu kwa sasa ndani ya Chadema wapo viongozi wengi watiifu kwa Katiba ya chama.Viongozi wengi wanaomtii na kumheshimu Freeman Mbowe kama Jabali la kisiasa Tanzania.Viongozi wanaoamini bila jitihada kubwa za Mbowe basi CDM ingekuwa katika kaburi la kisiasa leo hii kama CUF,NCCR,TLP na wengine.

Kati ya viongozi wengi wanaomtii na kumheshimu Mbowe nimtaje mmoja tu Tundu Antipas Mughwai Lissu.Hakuna asiyemjua jemedari huyu ambaye pamoja na usomi wake na umaarufu wake duniani kote Lakini kila azungumzapo hakosi kumtaja na kumpa heshima Freeman Mbowe kwamba ni Profesa wa upinzani Tanzania.

Kwamba kwa aliyopitia na heshima na uvumilivu wake kwa Chama chake basi anastahili siku moja kuvikwa Taji.Kwamba ni Hazina ndani ya Chadema.Kwamba ni Hazina ndani ya nchi.Kwamba siku moja miaka ijayo anafaa kabisa kuchukua mikoba.Kwamba anastahili kabisa kuwa mbadala wa Jabali la kisiasa Tanzania.Heshima nyingi zimwendee Tundu Lissu.

Nimalizie kwa kusema bado tunamhitaji Freeman Mbowe walau kwa miaka mingine mitano.

#Mbowe Tano Tena#
Kumbe anatakiwa mtu anae mtii Mbowe? Kama ndio hivyo basi Mbowe ataeendelea kuongoza.
 
Historia ni mwalimu mzuri.... Hakuna aliewahi kujaribu kumpinga Mbowe akabaki salama.

Kama Mbowe anakubalika hofu ya nini kuitisha uchaguzi.?
Hakuna hofu yoyote. Uchaguzi utafanyika.

Swali kwanini ccm inakataa tume huru na kuwawania maded wasimamie Uchaguzi?
 
Hapo kisu kimeingia mfupani.Hawatakujibu
 
Hata 2050+ ni sawa tu.
Cha msingi Mbowe Tano Tena
Mimi ya Mbowe tano tena hainisumbui. Hata ingekuwa "mia tena". Kwangu sawa tu. Mimi niko concerned na 2030+ ya Rais Magufuli. Kama Franklin Delano Roosevelt. Remember?
 
Na mimi hayo hayanihusu kabisa.
Kwangu ni CDM Kwanza na Mbowe Kwanza
 
Ni dhahiri kuwa kwa sasa Fukuto la uchaguzi mkuu wa ndani kwa chama kikuu na tishio cha upinzani nchini limepamba moto.

Vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali vimepambwa na habari hizi lakini hususani nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama anayetarajiwa kuchaguliwa Decemba mwaka huu.Ni nafasi muhimu sana kwani ndiyo inayoamua hatma ya chama kwa miaka mingine mitano.

Freeman Mbowe jabali la kisiasa Tanzania na tajiri mwenye ukwasi mkubwa aliyeamua kuweka starehe pembeni na kuitikia wito wa kuwakomboa wananchi kupitia chama alichoshiriki kukiasisi cha CHADEMA amekitumikia chama hicho kwa awamu 3 sasa na akitarajiwa kupata ushindi mkubwa kuongoza awamu nyingine ya nne hapo December.

Mafanikio ya Freeman Mbowe ndani ya CHADEMA yanahitaji vitabu na vitabu kuviandika kwani tunaweza kusema ni Mwenyekiti aliyewezesha chama alichokiongoza kupata mafanikio makubwa zaidi kwa Tanzania tangu mfumo wa vyama vingi uanze 1992.

Freeman Mbowe anao wapinzani wake wanaotaka aondoke madarakani hata leo na asipewe nafasi nyingine kabisa ya kukiongoza chama hicho.Lakini bahati nzuri ni kwamba wapinzani wote wa Freeman wanatoka nje ya chama hicho na akitokea mtu kujifanya anampinga Mbowe akiwa chini ya Chadema ni wazi ni kibaraka mwenye lengo la kuvuruga umoja ndani ya chama.Tumeshuhudia hivi karibuni waasi wachache wabunge walioanza kumtukana Freeman na baada ya muda mchache wote wakaunga mkono juhudi na kujiunga na CCM.

Wengine tunajiuliza kwanini wasiomtaka Freeman watoke nje ya chama hicho? Kwamba wanaoipenda Chadema ni wanaCCM na vibaraka wao? Ili iweje??

Tutarajie kushuhudia makubwa zaidi kuelekea uchaguzi mkuu wa chama mwishoni mwa mwaka huu.Tusishangae kuona maadui wa Chadema wakitumia kila njia kutaka kuichagulia Chadema kiongozi.Na kila adui wa Chadema ombi lake ni moja Kwamba Mbowe Hafai na Asichaguliwe tena.Hiyo ndiyo kaulimbiu ya kila asiyeitakia mema Chadema.

Jambo la kumshukuru Mungu kwa sasa ndani ya Chadema wapo viongozi wengi watiifu kwa Katiba ya chama.Viongozi wengi wanaomtii na kumheshimu Freeman Mbowe kama Jabali la kisiasa Tanzania.Viongozi wanaoamini bila jitihada kubwa za Mbowe basi CDM ingekuwa katika kaburi la kisiasa leo hii kama CUF,NCCR,TLP na wengine.

Kati ya viongozi wengi wanaomtii na kumheshimu Mbowe nimtaje mmoja tu Tundu Antipas Mughwai Lissu.Hakuna asiyemjua jemedari huyu ambaye pamoja na usomi wake na umaarufu wake duniani kote Lakini kila azungumzapo hakosi kumtaja na kumpa heshima Freeman Mbowe kwamba ni Profesa wa upinzani Tanzania.

Kwamba kwa aliyopitia na heshima na uvumilivu wake kwa Chama chake basi anastahili siku moja kuvikwa Taji.Kwamba ni Hazina ndani ya Chadema.Kwamba ni Hazina ndani ya nchi.Kwamba siku moja miaka ijayo anafaa kabisa kuchukua mikoba.Kwamba anastahili kabisa kuwa mbadala wa Jabali la kisiasa Tanzania.Heshima nyingi zimwendee Tundu Lissu.

Nimalizie kwa kusema bado tunamhitaji Freeman Mbowe walau kwa miaka mingine mitano.

#Mbowe Tano Tena#
Kwa hali hii,
CCM TUTAENDELEA KUN'ARA.....
 
Back
Top Bottom