Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Kwani aliyekuambia ambulance inakomea Hospitali ya wilaya pekee ni nani? Inaweza kumkimbiza mgonjwa kwenda KCMC au Arusha akili yako iko kwenye kupinga tu...ifike wakati uwe unapongeza...sawa East African
 
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?

Nani kakudanganya kuna shida ya madaktari?? Machame Hospital kuna chuo cha uganga sasa hiyo shida inatokea wapi?? Na hilo suala la dawa ni ujinga unaojaribu kuwadanganya wajinga wenzako. Hakuna hiyo shida kabisa..
 
Congrats Mwenyekiti wangu Kamanda wa anga Mh. Freeman Mbowe kwa kuwajali wapiga kura wako.

Mwenyekiti wa ccm aliahidi bajaji mwaka 2010 lakini hadi leo hii bado hajatekeleza ahadi yake. Lakini Mwenyekiti wa CHADEMA aliahidi ambulance na leo ametekeleza ahadi yake.

Tukiwapima ninyi wenyeviti wawili wa vyama vikubwa hapa nchini tunabaini bila shaka yoyote kuwa Kamanda Mbowe unatenda unachokizungumza wakati Le profeseri Kikwete anatenda kinyume na anachozungumza.
 
Nafikiri nimekujibu hapo juu hakuna Ambulance yoyote zilizotolewa sasa nijibu swali langu la mabandiko
Miccm haiwezagi kujenga hoja, yenyewe ni kushambulia tu.Haumuoni Nape mwehu mwenzao yule? Ndiyo sample za sahihi za magamba.
 
Naomba nikueleweshe hayo magari ndio yamefika mwaka huu ulitaka awagawie mwaka kesho?

Sipingi hilo unalolisema na ndio maana nimesema ni mfano wa kuigwa. Ila ukumbuke sisi washabiki na wanachama wa cdm tunaikataa ccm kwa matendo yao na sio kwa rangi yao. Isije ikawa tunapinga matendo yanayofanywa na ccm wakati huo huo tukawa mabubu wanapofanya cdm. Kama ni kweli limekuja mwaka huu na amelitoa kwa dhamira nzuri well and good. Nadhani wewe na mimi sio wageni wa miundo mbinu kama barabara, maji na umeme kuboreshwa mwaka wa uchaguzi na ccm ili waendelee kubaki madakani, sisi tutumie mbinu ya kweli ya kuwaletea maendeleo wananchi wakati wote na sio kipindi fulani tu ili kupata kura baada ya hapo tunaingia mitini. Rekodi ya Mh. F.Mbowe ya miradi ya maendeleo kipindi chote alipokuwa mbunge ndiyo itakayombeba na sio kuvuta shuka asubuhi. Ukweli utatuweka huru kama taifa na wote tunapaswa kusimamia hili ili tutembee kifua mbele pindi tunapotumia majimbo ya wabunge wetu kama mfano. Ila kama tutatumia approach zilezile za kiccm mbona itakuwa majanga huko mbeleni tukipata madaraka.
 
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?

ni kweli mkuu
kuna siku nilimshauri mbowe
_vijiji vya kyeri,uraa na uswaa kigeografia vipo pamoja kwani vimetenganishwa na mto marire na kikafu,kuna zahanati ipo centre inaitwa "kishibwe"
angeiboresha na ingekuwa msaada sana kwa vijiji husika
 
Nimekuelewa sana Fanya reserch ndogo tu ya madiwani na wabubge wa chadema mara kwa mara wako na wananchi kwenye swala la maendeleo na hila zote wanavyofanyiwa na mkoloni mweusi yani ccm
 
Profesa maji marefu anatoa ambulance za ungo

Kwi kwi kwi kwi! Labda kwa hilo mkuu, maana hawa magamba kwa ushirikina hawajambo.

CC; Change,Mzee wa vijisent alitia unga kwenye kiti cha Mwakyembe kule mjengoni.
 
Nimekuelewa sana Fanya reserch ndogo tu ya madiwani na wabubge wa chadema mara kwa mara wako na wananchi kwenye swala la maendeleo na hila zote wanavyofanyiwa na mkoloni mweusi yani ccm

Hilo ninakubali kwani nina ushahidi nalo. Ila angalizo langu kama mbuge ama diwani wetu alizembea hapo nyumba wakati wa miaka yake mitano akianza madoido lala salama hii hatujengei picha nzuri kwa umma. Ni vyema hawa madiwani au wabunge wetu wachache tulionao tukiingia wakati wa kampeni tuwatumie kama mifano halisi ya nini chama chetu kimefanya. Hali hii itajenga imani kwa wananchi kwani watukuwa na uhakika wakitupa madaraka wametoka kimaisha. Lakini kama mtu alikuwa miguu juu kwenye muda wote leo tuanze kumuona sijui kwenye misiba, mara anawanunulia mapool table vijana, sijui kununua jezi za mpira ndungu hizo mbinu zimepitwa na wakati. Tuendelee kutiana moyo na hasa kuonyana bila haya kwa faida ya chama chetu na hatima ya taifa letu.
 
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?

ulitakaje we kibalaka
huyo wa kwako si alete angalao (panado)
wa kwako aliahidi ataleta (ambulensi) za bajaji je zimefika kijijini kwenu??
 
ni kweli mkuu
kuna siku nilimshauri mbowe
_vijiji vya kyeri,uraa na uswaa kigeografia vipo pamoja kwani vimetenganishwa na mto marire na kikafu,kuna zahanati ipo centre inaitwa "kishibwe"
angeiboresha na ingekuwa msaada sana kwa vijiji husika

Tayari suala la Zahanati ya Kishibwe lipo mezani na linashugulikiwa vizuri sana na mh mbowe...si Muda mrefu kutoka sasa utaona mabadiliko makubwa hapo......
 
Back
Top Bottom