Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA, Mbunge wa Jimbo la HAI,,na Kiongozi wa kambi RAsmi bungeni MH FREEMAN MBOWE ameendeleza juhudi zake katika kuokoa maisha wa watu wa jimbo lake ambapo wiki hii ametoa ambulances kwa ajili ya watu wa jimbo lake....

Kutolewa kwa ambulance hiyo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa HAI jimbo ambalo limetawaliwa na mito na mabonde mbalimbali ambapo litatumika kuwawaisha wagonjwa hospitali za teule ya Machame na ile ya Wilaya.

Kufuatia kutolewa kwa ambulance hiyo mkazi mmoja wa kata ya Machame Mashariki(LYAMUNGO KATI) amesema itakuwa ni msaada mkubwa sana kwao maana itarahisisha kupeleka wagonjwa kutoka Kituo cha afya Lyamungo Hadi hospitali teule ya Machame.

Baadhi ya wakazi wa Masama(Masama Bweera) wameonekana kufurahia na wengine kudiriki kusema kama FREEMAN MBOWE atagombea tena watampa ushiindi wa kishindo kutokana na mheshimiwa Mbowe kutoa Ahadi zake bila kupendelea upande wowote.

10933724_345578208967134_2984157386036978574_n.jpg
Hongera Sana kaka umewanyamazisha wale wanaobeza harakati zako. Big up sana
 
Freeman Mbowe amefanya jambo kzuri sana na la kupigiwa mfano. Ila mimi kama shabiki wa cdm sifurahishwi sana na hali hii ya kutoa mambo ya maendeleo haswa mwaka wa uchaguzi. Kwa kiasi kikubwa hali hii tunaipigia kelele huko ccm kwani ikifika wakati wa uchaguzi ndio unawaona viongozi wao wakianza kurekebisha miundo mbinu kama ya maji, barabara, umeme nk. Lakini wakishapata kura huwaoni tena jimboni. Kama amewahi kutoa misaada mingine yenye tija katika jimbo lake kabla ya mwaka huu ni sawa lakini kama ni sasa naona tunaanza kutumia mbinu zilezile za kiccm.

Kwa mtu anayeangalia ukweli hapa anaweza kupata shida na dhamira ya mtoaji. Ni kweli kwamba ni muwajibikaji ama ndi walewale wanaotumia uelewa finyu wa wananchi kuwapiga bao? Nasema hivo huku nikizingatia wajibu mkubwa sana wa mbunge ni kuisimamia na kuiwajibisha serekali na wala sio mfadhili, lakini hazuiwi kutoa msaada kutoka kwenye mfuko wake au kuhamisisha watu waliokaribu naye kusaidia kutatua kero zilizo jimboni mwake na taifa kwa ujumla. Ila hali hii isisubiri tu mwaka wa kampeni maana kuna uwezekano wa kuwa ni walewale. Watanzania tuwe makini ili tusirudie kosa.
Naomba nikueleweshe hayo magari ndio yamefika mwaka huu ulitaka awagawie mwaka kesho?
 
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?

Kukosekana Kwa Madaktari Na Madawa Ni Kwa Sababu Ya Utawala Legelege Wa CCM.. VIVA CHADEMA
 
Magari yapo pale Arusha Art yaliuzwa kwa Muhindi.

Kwatarifa kwako na wengine hayo si magari yaliyotolewa msaada wala hakuna kitu kama hicho umepewa habari za kupikwa.. naomba nikulize na mimi jee ulivyotengeneza yale mabango yakumchafua Lema ulikua na Maana gani kwenye serekali za mitaa?
 
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?

Sasa madawa mtayapata wapi wakati MICCM hailipi hela za MSD? Madaktari mnawapiga na kuwapeleka mabwepande watatokea wapi wa kutosha? hovyo kabisa nyie
 
Kwatarifa kwako na wengine hayo si magari yaliyotolewa msaada wala hakuna kitu kama hicho umepewa habari za kupikwa.. naomba nikulize na mimi jee ulivyotengeneza yale mabango yakumchafua Lema ulikua na Maana gani kwenye serekali za mitaa?

Labda ungetuambia zile Ambulance mbili Lema alizopewa na meya wa jiji la London kwa ajili ya wana Arusha ziko wapi?
 
Labda ungetuambia zile Ambulance mbili Lema alizopewa na meya wa jiji la London kwa ajili ya wana Arusha ziko wapi?

Nafikiri nimekujibu hapo juu hakuna Ambulance yoyote zilizotolewa sasa nijibu swali langu la mabandiko
 
Back
Top Bottom