Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Standalone

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2014
Posts
676
Reaction score
576
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA, Mbunge wa Jimbo la HAI,,na Kiongozi wa kambi RAsmi bungeni MH FREEMAN MBOWE ameendeleza juhudi zake katika kuokoa maisha wa watu wa jimbo lake ambapo wiki hii ametoa ambulances kwa ajili ya watu wa jimbo lake....

Kutolewa kwa ambulance hiyo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa HAI jimbo ambalo limetawaliwa na mito na mabonde mbalimbali ambapo litatumika kuwawaisha wagonjwa hospitali za teule ya Machame na ile ya Wilaya.

Kufuatia kutolewa kwa ambulance hiyo mkazi mmoja wa kata ya Machame Mashariki(LYAMUNGO KATI) amesema itakuwa ni msaada mkubwa sana kwao maana itarahisisha kupeleka wagonjwa kutoka Kituo cha afya Lyamungo Hadi hospitali teule ya Machame.

Baadhi ya wakazi wa Masama(Masama Bweera) wameonekana kufurahia na wengine kudiriki kusema kama FREEMAN MBOWE atagombea tena watampa ushiindi wa kishindo kutokana na mheshimiwa Mbowe kutoa Ahadi zake bila kupendelea upande wowote.

10933724_345578208967134_2984157386036978574_n.jpg
 
Chadema ndicho chama kinachoweza kutenda na wananchi wakakiamini.

Huyu ndiye Freeman Mbowe
Hawa ndiyo wabunge wa Chadema.
Hii ndiyo Chadema
 
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?
 
Dah huu ndio mfano wa kuigwa wa kiongozi wa watu. Hongera sana kamanda wa anga, Freeman Aikael MBOWE
 
Ametoa magari au gari?

Bora huyu amejitahidi, mwenzake Godbless J Lema yeye alipewa msaada na bado akayauza.

Leo maji yamekufika shingoni ukakubali kilaini hivyo mkuu msalani. Kweli chadema kinakubalika na watu wengi sana hadi ccm sema ni ioga tu kusema waziwazi kuwa hichi chama kipo makini.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la Hai sio ambulance ni ukosefu wa madatari na madawa hospitalini.Sasa hiyo ambulance itakuwa inawakimbiza watu kuwapeleke mahali kusiko na madawa na madaktari?

Ccm imefanya nn kwa miaka 50? Si ni afadhari alotoa ambulance inaweza ata kuwakimbiza wagonjwa hosp ya Rufaa kuliko mkuu wa kaya anotumia pesa za umma kusafiri ka Vasco da Gama
 
Freeman Mbowe amefanya jambo zuri sana na la kupigiwa mfano. Ila mimi kama shabiki wa cdm sifurahishwi sana na hali hii ya kutoa mambo ya maendeleo haswa mwaka wa uchaguzi. Kwa kiasi kikubwa hali hii tunaipigia kelele huko ccm kwani ikifika wakati wa uchaguzi ndio unawaona viongozi wao wakianza kurekebisha miundo mbinu kama ya maji, barabara, umeme nk. Lakini wakishapata kura huwaoni tena jimboni. Kama amewahi kutoa misaada mingine yenye tija katika jimbo lake kabla ya mwaka huu ni sawa lakini kama ni sasa naona tunaanza kutumia mbinu zilezile za kiccm.

Kwa mtu anayeangalia ukweli hapa anaweza kupata shida na dhamira ya mtoaji. Ni kweli kwamba ni muwajibikaji ama ndi walewale wanaotumia uelewa finyu wa wananchi kuwapiga bao? Nasema hivo huku nikizingatia wajibu mkubwa sana wa mbunge ni kuisimamia na kuiwajibisha serekali na wala sio mfadhili, lakini hazuiwi kutoa msaada kutoka kwenye mfuko wake au kuhamisisha watu waliokaribu naye kusaidia kutatua kero zilizo jimboni mwake na taifa kwa ujumla. Ila hali hii isisubiri tu mwaka wa kampeni maana kuna uwezekano wa kuwa ni walewale. Watanzania tuwe makini ili tusirudie kosa.
 
Ametoa magari au gari?

Bora huyu amejitahidi, mwenzake Godbless J Lema yeye alipewa msaada na bado akayauza.
Huo ushaidi upo wapi kua aliuza? Ndio yale mabandiko yako yakumchafua ulitengeneza kwenye serekali za mitaa badala yake tukawachapa vilivyo?
 
Last edited by a moderator:
Kudos Mbowe,sio hao mafisadi wa ccm wanaenda kuficah pesa nje ya nchi
 
Back
Top Bottom