Free talk: Mwanamke shtuka!

Free talk: Mwanamke shtuka!

Kuna demu juzi kati kamzingua dogo wangu hadi tukagoma kwenda kupeleka posa, wakati kamsaidia sana kwenye mambo ya shule hadi kamaliza chuo, jana ndio napata stori jamaa anaemzuzua anafanya kazi duka flani anaiba ela wanaenda kuzitumbua, dogo kalia sana ila ndio hivyo tumemwambia kuhusu habari ya huyo demu asituhusishe tena labda awe mwingine, ila kwa utajiri wa dogo aliokuanao (sema alkua hamuonyeshi huyo demu) demu kapishana na ela aisee, wanawake wazuri wana shida sana.
Poleni sana mkuu.

Dogo afanye mpango wa demu mwingine tuu maisha yaendelee ..hawa watu ndio shukrani zao hizi.



Cc Heaven Sent & espy
 
Noo...you took me wrong..

Huwezi kucompare sex na kumsomesha mtu...afu pia ujue Sex kuna mutual pleasure..kuna mutual benefit..

Sex kwani naenjoy mimi peke yangu..?

Vaa viatu vya mwanaume hebu;

Unapewa kitobo kweli, umesomesha mtu miaka 3 ama 4..kamaliza unataka kujenga nae future anakuja jamaa from nowhere binti bila kujali anasepa na msela mwingine..real..?

Sasa hapo ndio unajua kuwa uliingilia wajibu wa mtu..

Mimi hili nimeliona kwa macho yangu kwa marafiki zangu..! Wala sikusoma story..! I will never do it.
Safi kabisa never ever do it
 
Have ma" like babe-girlunajua nini umesema maneno maziiito mno mwenye kusikia na asikie,.japo KUPANGA NI KUCHAGUA hatuingiliani lifestyles lakini penye ukweli lazima tukumbushane...

Wadada tupunguze luxuries tofauti na vipato vyetu,.tuwe na kiasi na kuridhika..tukipata wenzetu hebu tupeane support sio kisa ni mbebe wako basi ndio akome kila dhiki unambebesha kaka wa watu looh tena ujue kwao wana japo mbuzi wa maziwa basi hali akashiba.,.ndio maana wengine miti mikavu hawanenepagi kwa kufyonzwa....tujue kufanya kazi zetu na kusave pia kwa ajili ya baadae,.kumtegemea mtu sana kwanza dhambi...

Yeremia 17:5-8 ukisoma utaona mtu anaye mtegemea mwanadamu anakuwaje...

Mungu akatubariki sawasawa na utajiri wake,kusukwa-sukwa hata kumwagika...!!!!
Ahsanteee
Naomba nikazie
 
Nikiwa binti, mara nyingi ijumaa tulikuwa na mikesha ya vijana, sio tu kuombeana ila nakukumbushana vitu mbalimbali. Namshukuru Mungu kwa ajili ya Pastor wetu, kuna muda alikuwa anatupa makavu hadi kanisani unapaona pachungu, Ila alitutengeneza tukawa watu fulani amazing sana.

He used to tell us young ladies; muda ambao hujaolewa ndo muda wa kufulfil your dreams; making an identity of your own. Once ukiolewa mara nyingi sana utatimiza ndoto/kutembea na vision ya mumeo. Majority tunaua ndoto zetu tukiingia ndoani (sad). So alitutaka tufanye kazi kwa bidii, adding values to our lives, sio tuspend kwenye unnecessary starehe kujifanya slay queens; waiting to get married and chop our hubby's money. Kuna wakati anamsimamisha kijana mdogo yupo high school (inspiration) ila tu ni anachakarika akikutajia assets zake, mimi limama lizima naona aibu na kupata tabu sana. Hakutaka kusikia kitu "I'm doing nothing". Kuna maisha zaidi ya kuolewa, what if usipoolewa, ndo utaishi ukiinvest kwenye kujiremba milele?

Hujapanga, unakaa home, make sure una vitu/assets zako. Sio kusubiri zawadi na vyombo vya send off ndo ukaanzie maisha, wewe binafsi unabeba nguo na viatu na mapochi.
Na alikuwa anatuambia kabisa, tusiende tukawe mizigo kwa waume zetu, hata chumvi ikiisha unasubiri baba atoke kazini. Wengine wanalia mume wangu ananinyanyasa sana, Ila wakati mwingine ni kwa sababu huna mchango wowote financially nyumbani, anakuchokaa. Afu pamoja na kuzaa, bado tuna wajibu wa kutimiza ndoto za watoto wetu. Watoto wako wasishindwe kutimiza ndoto zao kisa baba amekataa kuwahudumia au hayupo au tukasema ni kazi ya baba yao tu. Though sio kama kila mtu atafanikiwa kuinvest as we wish, ila kuwa na ile spirit ya kuthubutu/ kutaka kufika mahala fulani ni jambo zuri sana. Kwa sababu hata usipofanikiwa leo, you won't rest till you make it happen.

Na maisha yana ups and downs, hata ukiolewa na bilionea possibly kuna siku maisha yatashake kidogo, sasa ukiwa slay queen, hicho kipindi cha mpito kitapita salama? Usije ukamuua kwa presha mumeo kwa kutaka aendelee kukuhudumia as it was before, au utakimbia nyumba? au utatafuta sponsors ili uendelee kumaintain status?. Make your own identity lady. Mwanamke ana nguvu ya kumultiply, chochote kidogo kitakachopandwa kwake/kufanywa na yeye, atakitunza hadi kiongeze na vingine. (I missed magazeti mweeh)
Huu tunauita ukweli mchungu..barikiwa sana dada
 
Ok..positive

Kuwe na seminar nyingi ambazo zitakuwa zinalenga kumsaidia mwanamke kujitambua hasa kiuchumi.

Kuanzishwe vipindi vya redio na tv kwenye vituo mbalimbali, kumuelimisha mwanamke kujitambua na namna gani ya kujisogeza mbele na kuwekeza kwenye biashara, badala ya kutumia pesa nyingi kwenye urembo na starehe.

Apate elimu na mafunzo ya kutosha, endapo akipata pesa ni nini anatakiwa kufanya kujikwamua kiuchumi kwa sasa na baadae
Hizo seminar mbona ni nyingi sana..na hata redioni kuna vipindi vya uhamasishaji na uelimisha...elimu zinatolewa sana tu..ila nisisi tu wenyewe kutokuzifanyia kazi
 
Najua kwa sio wote..

Ila Mungu ni mwema , watu waliyopigwa changa la macho wanajitokeza hapa hapa kabla uzi haujafika mbali..

Tatizo No one can predict one's future..! So hatujui kama mtu atachange..!

To be safe bora mtu usijitose.
Teh ngoja na upande wetu, watakuja wengi tu waliochumia juani na watu, ila ulipofika muda wa kula kivulini wakatoswa
 
Kuna demu juzi kati kamzingua dogo wangu hadi tukagoma kwenda kupeleka posa, wakati kamsaidia sana kwenye mambo ya shule hadi kamaliza chuo, jana ndio napata stori jamaa anaemzuzua anafanya kazi duka flani anaiba ela wanaenda kuzitumbua, dogo kalia sana ila ndio hivyo tumemwambia kuhusu habari ya huyo demu asituhusishe tena labda awe mwingine, ila kwa utajiri wa dogo aliokuanao (sema alkua hamuonyeshi huyo demu) demu kapishana na ela aisee, wanawake wazuri wana shida sana.

Teh teh teh teh, hivi mwanaume mwenye hela zako unaanzaje kusumbuliwa na binti moja kweli ???
Unless huyo dogo wako hana pesa nyingi kivile, halafu pesa hata ufiche huwa inaonekana mazee yani huwezi ficha kabisa. Tukikuangalia tu tunafahamu kwamba hapa huyu jamaa kapigwa na upepo wa pesa. Sasa dogo lako lina hela halafu linasumbuliwa na kibinti cha hovyohovyo kweli ??? Bwahahaha, huyo dogo mumchangamshe kabisaa.
 
Poleni sana mkuu.

Dogo afanye mpango wa demu mwingine tuu maisha yaendelee ..hawa watu ndio shukrani zao hizi.



Cc Heaven Sent & espy
Mimi kuna moja hivi Braza alitafutia kazi na Scholarship ya PhD lakini alichokuja kufanywa, teh teh teh teh!
Nidyo maana mimi kama namsaidia mwanamke huwa namsaidia bure tu kwasababu nimeamua, lakini nje ya hapo huwa sitegemei sanaaaa kutoka kwao. Its a racket, kufanya betting ya maisha na mwanamke...
 
Back
Top Bottom