Umenena vyema Espy, kwa kweli ni wanawake wachache sana kwasasa wanaofikiria maendeleo kwa jitihada zao wenyewe pasipo kuwepo mkono wa mwanaume.
Unakuta dada kaajiriwa (binafsi/serikali) na ana muda hata wa zaidi ya miaka mitatu kazini lakini hana lolote alilowekeza zaidi ya kuhangaika na fashion kila siku... Wengi hatukumbuki kuwa nafasi na muda tulionao sasa baadaye tunaweza tusiupate, nyakati zinabadilika uchumi nao unakuwa sio rafiki.. Siku utakayoingiwa na akili ya kufanya kitu angalau kikaonekana cha manufaa kwako na kwa yeyote ajaye (mume/watoto) ndo utakapo ng'amua kuwa huna tena uwezo wa kufanya hivyo na ndipo itabaki tu simulizi kuwa yule dada enzi zake alikuwa yuko vizuri kiuchumi...Muda huo akili unayo lakini huna vitendea kazi.
Mambo mengine tuwe tunayaacha yanatupita, si lazima kuyumbishwa na dunia, kushoto upo, huku upo , kule upo yaani kila kinachokuja umo....
Tujaribu pia kuangalia na aina ya marafiki wa kuambatana nao, wao kila siku wazungumzia fashion mpya tu na kutambiana madanga, wafikiri lini utapata wazo la kusema uinvest kwenye kitu cha maana???
Nimewahi kuwa na rafiki, alinizidi kwa umri (miaka 6) lakini sioni alichokuwa akinifaidisha zaidi ya kunipa stori tu za kupelekana maduka ya mikoba + nguo + viatu + stori za madanga aliyonayo...
Nikimshauri mawazo mazuri utasikia maisha yenyewe hayaeleweki, tutumie....Nikaona hili BOX halinifai...
*Kama una uwezo na nafasi ya kufanya kitu fanya, huyo mume endapo utajaaliwa aje akute angalau una pa kuegemea...Mkiunganisha nguvu pamoja angalau mnakuwa mmejisogeza sogeza....