Nikiwa binti, mara nyingi ijumaa tulikuwa na mikesha ya vijana, sio tu kuombeana ila nakukumbushana vitu mbalimbali. Namshukuru Mungu kwa ajili ya Pastor wetu, kuna muda alikuwa anatupa makavu hadi kanisani unapaona pachungu, Ila alitutengeneza tukawa watu fulani amazing sana.
He used to tell us young ladies; muda ambao hujaolewa ndo muda wa kufulfil your dreams; making an identity of your own. Once ukiolewa mara nyingi sana utatimiza ndoto/kutembea na vision ya mumeo. Majority tunaua ndoto zetu tukiingia ndoani (sad). So alitutaka tufanye kazi kwa bidii, adding values to our lives, sio tuspend kwenye unnecessary starehe kujifanya slay queens; waiting to get married and chop our hubby's money. Kuna wakati anamsimamisha kijana mdogo yupo high school (inspiration) ila tu ni anachakarika akikutajia assets zake, mimi limama lizima naona aibu na kupata tabu sana. Hakutaka kusikia kitu "I'm doing nothing". Kuna maisha zaidi ya kuolewa, what if usipoolewa, ndo utaishi ukiinvest kwenye kujiremba milele?
Hujapanga, unakaa home, make sure una vitu/assets zako. Sio kusubiri zawadi na vyombo vya send off ndo ukaanzie maisha, wewe binafsi unabeba nguo na viatu na mapochi.
Na alikuwa anatuambia kabisa, tusiende tukawe mizigo kwa waume zetu, hata chumvi ikiisha unasubiri baba atoke kazini. Wengine wanalia mume wangu ananinyanyasa sana, Ila wakati mwingine ni kwa sababu huna mchango wowote financially nyumbani, anakuchokaa. Afu pamoja na kuzaa, bado tuna wajibu wa kutimiza ndoto za watoto wetu. Watoto wako wasishindwe kutimiza ndoto zao kisa baba amekataa kuwahudumia au hayupo au tukasema ni kazi ya baba yao tu. Though sio kama kila mtu atafanikiwa kuinvest as we wish, ila kuwa na ile spirit ya kuthubutu/ kutaka kufika mahala fulani ni jambo zuri sana. Kwa sababu hata usipofanikiwa leo, you won't rest till you make it happen.
Na maisha yana ups and downs, hata ukiolewa na bilionea possibly kuna siku maisha yatashake kidogo, sasa ukiwa slay queen, hicho kipindi cha mpito kitapita salama? Usije ukamuua kwa presha mumeo kwa kutaka aendelee kukuhudumia as it was before, au utakimbia nyumba? au utatafuta sponsors ili uendelee kumaintain status?. Make your own identity lady. Mwanamke ana nguvu ya kumultiply, chochote kidogo kitakachopandwa kwake/kufanywa na yeye, atakitunza hadi kiongeze na vingine. (I missed magazeti mweeh)