Free talk: Mwanamke shtuka!

Free talk: Mwanamke shtuka!

José mwenyewe mtoto tuu huoni alivyokuwa ananisumbua?
Nadhani sasahivi nitafute mzee mwenzangu hawa watoto watanipa jaka la moyo.

Au nielekeze akili yangu kwenye kujikwamua kimaisha kwa kuendeleza biashara zangu kuliko kupambana na hawa watoto kama ulivyotushauri kwenye bandiko lako au wewe unasemaje?
Haya mambo unayasema hadharani kabisaa? Yaani mimi mtoto? Biashara zako unafanya kimyakimya hata hunishirikishi
 
Mwanamke ununue kiwanja ni mwanaume gani huyo ambaye hana akili sawa sawa atajenga hapo......labda kununua fenicha za ndani na vikolokolo......nyumba hujengwa na mwanaume ili mkewe aje kuingia na kuisimamia hatimaye kuimiliki....
Kumbe anaimiliki ukishajenga, basi haina haja jenga tu kwenye chake.
 
hapa naona kuna mada mbili tofauti
1.matarajio ya wanawake kwa wanaume wa kuwaoa"kabla hawajavurugwa na dunia according to mtoa mada"(fantasy vs reality)
2.wanawake kujikwamua kiuchumi kabla na baada ya kuolewa
Ila naona hapa wengi wao wamebase kwenye hiyo ya pili, ya kwanza wameiacha sijui kwanini
Hiyo ya kwanza ilikuwa kibwagizo tu, haikuwa mada. Moderator sijui ni Jamii forum ndio wameiweka kama mada kwa kubadili heading.
 
Habari wana MMU.

Kuna hili jambo ningependa tujadiliane ama tushirikishane kidogo.

Hakuna asiejua kuwa kila mwanamke kabla hatujavurugwa na dunia huwa matamanio yetu ni siku moja kuolewa na kutengeneza familia na mwanaume fulani hivi amazing(fantancy vs reality).

Sasa tatizo linakuja kuwa huwa wanawake wengi wana mentality kuwa maandalizi ya familia ya baadae haswa kwa mambo yanayohusu assets na gharama zingine ni majukumu ya mwanaume na sio mwanamke.
Hivyo unaweza kukuta binti ana kazi nzuri tu ila hata kujiwekeza kununua hata kiwanja walaaa hawazi au hata kufungua biashara. Anawekeza kwenye mikoba,mawigi,simu za bei ghali,viatu nk. Vitu ambavyo ukivipigia mahesabu unakuta ana viwanja vitano vikubwa tu huku kijijini kwetu.

Hebu fikiria unaolewa ukiwa angalau umejiwekeza kiasi fulani hivyo mkiunganisha nguvu na mwenza wako angalau mnapiga hatua kadhaa kwa haraka kuliko kusubiria mwanaume afanye kila kitu.

Wakati mwingine unakuta binti anadate mwanaume mwenye expossure ya kutosha na mfanyabiashara mzuri, hata kuomba basi hata aelekezwe abc's za biashara, hata kuunganishwa kibiashara nehiiii.

Au unadate mwanaume mwenye uwezo mkubwa kifedha hivyo kazi yake ni kuomba kununuliwa simu ya milioni 2 nk, vitu vya anasa ambavyo kwa kiasi kikubwa havikuongezei lolote la maana zaidi ya sifa za kijinga. Ni kwanini usimuombe mtu wa aina hiyo hata business idea, au angalau uanze jambo lako ie biashara,ujenzi nk kisha umuombe akuongezee kiasi fulani cha pesa? Kwa mwanaume mwenye upeo atakuona una akili na anaweza kukusogeza mahali pazuri.

Mwingine unakuta ni mama kabisa ila hata haiwazii kesho ya mtoto wake ambae anamlea peke yake, yuko busy na starehe na kutumbua pesa za child support, kesho na keshokutwa baba hayupo mtu anaanza kuhaha wakati nafasi ilikuwepo akaichezea

Maisha yamebadilika sana jamani basi nasi wanawake tubadilike in a positive way, tuyaishi maisha halisi na sio ya kuigiza ili angalau tunapoingia kwenye maisha ya ndoa angalau tuwe na cha kuongeza sio ndio ukiolewa umtwishe mwanaume majukumu ya familia mnayoijenga,familia ya kwao na ya kwenu pia. No wonder wanakufa mapema hawa watu.

Tuzitumie fursa vizuri pale zinapopatikana kabla haijawa too late.

Jamani hapa simchagulii mtu maisha ila hakikisha hautokuwa na majuto baadae kuwa "laiti ningejua"!!! Maana hakuna anaependa kesho yake iwe ya kuunga unga.

Nawasilisha.

Dada hilo jimbo lina mtu au tunaruhusiwa kugombeamo maana "you have speak my mind" hebu nitafuta kule chumbani tuyajenge
 
Back
Top Bottom