Free talk: Mwanamke shtuka!

Kuna wale wake za watu kabisa. Mtu anakaa anapewa kila kitu anaona maisha ndo kayamaliza. Nimeshawahi kuona mmama anaishi kwa aibu baada ya mume wake kufa ambae alikua anampa kila kitu. Hata mwanaume akupe kila kitu usipotafuta chako ipo siku utaumbuka.
Wanawake walio wengi huolewa ili kupata sifa mtaani kuwa kaolewa pasipo kujua kuwa kuna mambo anatakiwa kuyazingatia na kuyafanya yeye kama mke...Neno msaidizi lina maana kubwa ambayo wanawake walio wengi wanafikiri ni kuingia katika ndoa kwa lengo la kuzaa na kulea watoto, kupika, kufua...Hapana!!!!

Yakiwemo yote hayo, mke anatakiwa asaidizane na mumewe kutimiza malengo yao, kwa ushauri na utendaji. Mwanamke aliye bora ni yule mwenye mawazo mazuri ya maendeleo, asiye na mtazamo wa kufanyiwa kila kitu na mumewe, msimamizi wa maendeleo, mtetezi wa haki ya familia yake na mwenye kiu ya kutimiza ndoto zake pamoja na ndoto za familia yake (mume na watoto).

Kama mwanamke umeingia ndoani bila kujua nini unakwenda kufanya tofauti na kuzaa basi daima utakuwa mzigo kwa mumeo... Tafsiri ya MSAIDIZI itageuka na kuwa jeraha kwa mumeo.. Hatakuwa na mshauri wa karibu, hatakuwa na msimamizi wa maendeleo ya familia yake na vilevile anaweza fikia hatua ya kujuta kwanini aliamua kukuweka ndani..
 
Ngoja nijifunze kitu leo, ila umejua kumisika agemate wangu. Mada nzuri sana ngoja nisubiri michango ya wadau

Mada nzuri sana! wanawake wengi wa hivyo bahati mbaya mume akitangulie mbele yahaki wanazirika.Kwa kweli kila mtu aishi akijua kuna leo na kesho tusiwe tegemezi kwa kila kitu tuweze kusimama hata kama mume hayupo.
 
Shit happens though, hata wanawake unamsaidia boyfriend weeh afu akifanikiwa hakujui au mume anakwambia wewe sio wa hadhi yang
.
Mmh sex ni mutual benefits, ila nyie mkinyimwaga ndo wa mnaongoza kulia lia lol. Na laiti tungejua; hawa wapenzi ni bora tungewapa hela hata kama watatukimbia; kuliko kuwapa "raha za ndoa zetu" tunazoziacha kwenye vitanda tunavyolalia na watu wasio na ndoa na sisi

Jamani khaah
 
Wanawake walio wengi huolewa ili kupata sifa mtaani kuwa kaolewa pasipo kujua kuwa kuna mambo anatakiwa kuyazingatia na kuyafanya yeye kama mke...Neno msaidizi lina maana kubwa ambayo wanawake walio wengi wanafikiri ni kuingia katika ndoa kwa lengo la kuzaa na kulea watoto, kupika, kufua...Hapana!!!!

Yakiwemo yote hayo, mke anatakiwa asaidizane na mumewe kufikisha malengo yao, kwa ushauri na utendaji. Mwanamke aliye bora ni yule mwenye mawazo mazuri ya maendeleo, asiye na mtazamo wa kufanyiwa kila kitu na mumewe, msimamizi wa maendeleo, mtetezi wa haki ya familia yake na mwenye kiu ya kutimiza ndoto zake pamoja na ndoto za familia yake (mume na watoto).

Kama mwanamke umeingia ndoani bila kujua nini unakwenda kufanya tofauti na kuzaa basi daima utakuwa mzigo kwa mumeo... Tafsiri ya MSAIDIZI itageuka na kuwa jeraha kwa mumeo.. Hatakuwa na mshauri wa karibu, hatakuwa na msimamizi wa maendeleo ya familia yake na vilevile anaweza fikia hatua ya kujuta kwanini aliamua kukuweka ndani..
Na kuna wanaume nao wanapenda kutegemewa ili wamuendeshe mwanamke. Anajua hata akufanyie nini hutapata uwezo wa kuondoka. Nawaambiaga rafiki zangu hata kama unapewa mpaka hela ya pad jifunze kutafuta chako ili siku kupewa kukikata ujue kujisimamia.
 
Habari wana MMU.

Kuna hili jambo ningependa tujadiliane ama tushirikishane kidogo.

Hakuna asiejua kuwa kila mwanamke kabla hatujavurugwa na dunia huwa matamanio yetu ni siku moja kuolewa na kutengeneza familia na mwanaume fulani hivi amazing(fantancy vs reality).

Sasa tatizo linakuja kuwa huwa wanawake wengi wana mentality kuwa maandalizi ya familia ya baadae haswa kwa mambo yanayohusu assets na gharama zingine ni majukumu ya mwanaume na sio mwanamke.
Hivyo unaweza kukuta binti ana kazi nzuri tu ila hata kujiwekeza kununua hata kiwanja walaaa hawazi au hata kufungua biashara. Anawekeza kwenye mikoba,mawigi,simu za bei ghali,viatu nk. Vitu ambavyo ukivipigia mahesabu unakuta ana viwanja vitano vikubwa tu huku kijijini kwetu.

Hebu fikiria unaolewa ukiwa angalau umejiwekeza kiasi fulani hivyo mkiunganisha nguvu na mwenza wako angalau mnapiga hatua kadhaa kwa haraka kuliko kusubiria mwanaume afanye kila kitu.

Wakati mwingine unakuta binti anadate mwanaume mwenye expossure ya kutosha na mfanyabiashara mzuri, hata kuomba basi hata aelekezwe abc's za biashara, hata kuunganishwa kibiashara nehiiii.
Au unadate mwanaume mwenye uwezo mkubwa kifedha hivyo kazi yake ni kuomba kununuliwa simu ya milioni 2 nk, vitu vya anasa ambavyo kwa kiasi kikubwa havikuongezei lolote la maana zaidi ya sifa za kijinga. Ni kwanini usimuombe mtu wa aina hiyo hata business idea, au angalau uanze jambo lako ie biashara,ujenzi nk kisha umuombe akuongezee kiasi fulani cha pesa? Kwa mwanaume mwenye upeo atakuona una akili na anaweza kukusogeza mahali pazuri.

Mwingine unakuta ni mama kabisa ila hata haiwazii kesho ya mtoto wake ambae anamlea peke yake, yuko busy na starehe na kutumbua pesa za child support, kesho na keshokutwa baba hayupo mtu anaanza kuhaha wakati nafasi ilikuwepo akaichezea

Maisha yamebadilika sana jamani basi nasi wanawake tubadilike in a positive way, tuyaishi maisha halisi na sio ya kuigiza ili angalau tunapoingia kwenye maisha ya ndoa angalau tuwe na cha kuongeza sio ndio ukiolewa umtwishe mwanaume majukumu ya familia mnayoijenga,familia ya kwao na ya kwenu pia. No wonder wanakufa mapema hawa watu.

Tuzitumie fursa vizuri pale zinapopatikana kabla haijawa too late.
Jamani hapa simchagulii mtu maisha ila hakikisha hautokuwa na majuto baadae kuwa "laiti ningejua"!!! Maana hakuna anaependa kesho yake iwe ya kuunga unga.

Nawasilisha.
Naomba uniruhusu nije nikupose.. maana nahisi Duniani umebaki wewe tu
 
Na kuna wanaume nao wanapenda kutegemewa ili wamuendeshe mwanamke. Anajua hata akufanyie nini hutapata uwezo wa kuondoka. Nawaambiaga rafiki zangu hata kama unapewa mpaka hela ya pad jifunze kutafuta chako ili siku kupewa kukikata ujue kujisimamia.
Ndio wapo, wanapenda kunyenyekewa, na wanafanya hivyo sio kama wanakupenda sana, la hasha! Hapo ni kukulemaza na kukufanya mtumwa siku zote ndoani, ataamua lolote kwako kwasababu anajua huna ujanja wa kujiendesha mwenyewe na kwa namna yoyote ile hutakuwa na jeuri ya kuishi nje ya yeye....

Just imagine wewe wamtegemea mwanaume kila kitu, kuanzia vocha mpaka kula yako, utakuwa na ujanja gani kwake??? Hata akutende vibaya mara kibao bado utaendelea kumvumilia kwasababu ya UOGA wa maisha aliokutengenezea mwenyewe..
 
Ndio wapo, wanapenda kunyenyekewa, na wanafanya hivyo sio kama wanakupenda sana, la hasha! Hapo ni kukulemaza na kukufanya mtumwa siku zote ndoani, ataamua lolote kwako kwasababu anajua huna ujanja kujiendesha mwenyewe na kwa namna yoyote ile hutakuwa na jeuri ya kuishi nje ya yeye....

Just imagine wewe wamtegemea mwanaume kila kitu, kuanzia vocha mpaka kula yako, utakuwa na ujanja gani kwake??? Hata akutende vibaya mara kibao bado utaendelea kumvumilia kwasababu ya UOGA wa maisha aliokutengenezea mwenyewe..
Mimi ndo maana natafutaga changu maana akili yangu kubadilika ni dakika moja. Sijawahi kumnyenyekea mwanaume kisa naishi kwa hisani yake. Na nilijifunza ukitaka maisha ya tabu ishi kwa kutegemea kila kitu kwa bwana. Mwanaume anakwambia usisome usifanye kazi usifanye biashara na wewe unakaa unafurahia tu. Mwanaume anaweza akatoa kila kitu alicho nacho kwa mwanamke wake ila siku za kuishi kwa binadamu ni chache sana. Kesho mwanaume hayuko mwanamke wake aliemfanya kilema ataishije? Maana hata aache Mali atazitapanya ziishe zote
 
Have ma" like babe-girlunajua nini umesema maneno maziiito mno mwenye kusikia na asikie,.japo KUPANGA NI KUCHAGUA hatuingiliani lifestyles lakini penye ukweli lazima tukumbushane...

Wadada tupunguze luxuries tofauti na vipato vyetu,.tuwe na kiasi na kuridhika..tukipata wenzetu hebu tupeane support sio kisa ni mbebe wako basi ndio akome kila dhiki unambebesha kaka wa watu looh tena ujue kwao wana japo mbuzi wa maziwa basi hali akashiba.,.ndio maana wengine miti mikavu hawanenepagi kwa kufyonzwa....tujue kufanya kazi zetu na kusave pia kwa ajili ya baadae,.kumtegemea mtu sana kwanza dhambi...

Yeremia 17:5-8 ukisoma utaona mtu anaye mtegemea mwanadamu anakuwaje...

Mungu akatubariki sawasawa na utajiri wake,kusukwa-sukwa hata kumwagika...!!!!
Mumu laiti wadada wote wangekusikia na kuku elewa. Basi kizazi hiki kinge change. Ila sasa shida ni kuwa wadada wengi kwa sasa wanambebesha kila kitu boy wake.

Yes kuhudumia ni kazi ya mwanaume lakin waangalie situation zenyewe. Unakuta dada kwao wana uwezo kabisa au ana kazi, lakin boi wake anabebeshwa majukumu mpaka ya baba mzazi.
Ndio hapa mtu anakimbia unaanza kuuliza umemkosea nn.
 
Ni hulka tuu mbaya,..ila kama mwanaume unacho pia na unawiwa kumpa mpenzio MPE,..sio basi na nyie ndio heee!!!!kisa tunaweza okoteza senti mbili tatu ndio hamtununlii hata pipi ivory sio Poa,...
 
Huo uchoyo sasa. Kwanza ili upate zaidi unatakiwa uonyeshe shukrani japo kwa zawadi ya boxer tuu.
Kuna watu ujue hawatoi zaka,fungu la 10 wala sadaka ya kuteketeza wala ya kawaida si kanisani wala msikitini...lakini kumpa hata mtu pipi tuu ya 150 anaona dhambi,.basi hata uonge napo 0 jomoniii....mfyuuuu
 
Hahaha, bata langu la ujana silijutii kabisa.
Sikutaka kukimbilia majukumu mpaka pale nilipokaa sawia.
Sasa vijana siku hizi akipata tu 1 or 2 M, baada ya chuo basi anavuta na kademu kake gheto kabisa.
Mimi kuna dogo langu juzi nimelifanyia mnasaha wa nguvu, eti anahudumia vibinti kama yeye ndiyo baba.
Tabia mbaya tu, hii kampeni ya kutunyima fursa kwanini lakini
 
Back
Top Bottom