Free talk: Mwanamke shtuka!

Free talk: Mwanamke shtuka!

Akuu! "Sijengi gari wala sinunui nyumba" wala kiwanja sijui biashara wala nini. Ukishakuwa na vitu hivi wanaume wazuri wazuri wanajiuliza mara mbili mbili; wewe unakuwa unagombaniwa na marioo hadi wanakwendea kwa vigagula. Mpaka uje umpate mwanaume mnayelingana au anayekuzidi siyo leo na kuoa hutaki na ukitaka kuolewa basi u-pretend kujishusha. Kwa maisha yenye urefu gani?

Ila haka kaujumbe ka Espy kanawafaa wanawake wote wa kike na wa kiume. Kadunia kameharibika haka!
Hahahaaaaa! NANDERA nilikumisimo jamani.
Heaven Sent njoo huku.

Nyakati zimebadilika ujue, naona mabadiliko makubwa hata kwao wanaume. Soon marioo watajikuta wamegeuka tunagombania nao wanaume maana hakutakuwa na mwanamke mfuga marioo.
 
Kuna wale wake za watu kabisa. Mtu anakaa anapewa kila kitu anaona maisha ndo kayamaliza. Nimeshawahi kuona mmama anaishi kwa aibu baada ya mume wake kufa ambae alikua anampa kila kitu. Hata mwanaume akupe kila kitu usipotafuta chako ipo siku utaumbuka.
Ni kweli mama, ukishajizoesha kutafuta unaunga tela tu, ila kama haujazoea ndio unaanza upyaaaa. Mtoto alikuwa feza unamrudisha kidumu na mfagio. Hadi mambo yaje yakae sawa umeisoma namba vya kutosha.
 
Na kuna wanaume nao wanapenda kutegemewa ili wamuendeshe mwanamke. Anajua hata akufanyie nini hutapata uwezo wa kuondoka. Nawaambiaga rafiki zangu hata kama unapewa mpaka hela ya pad jifunze kutafuta chako ili siku kupewa kukikata ujue kujisimamia.
Mwanaume mzigo huyo, mawazo mgando kabisa hayo. Fanya nafasi yako kama mwanaume nawe utaheshimika tu, haina haja ya kumnyanyasa mtu kwa kigezo cha "kuheshimiwa".
 
Mimi ndo maana natafutaga changu maana akili yangu kubadilika ni dakika moja. Sijawahi kumnyenyekea mwanaume kisa naishi kwa hisani yake. Na nilijifunza ukitaka maisha ya tabu ishi kwa kutegemea kila kitu kwa bwana. Mwanaume anakwambia usisome usifanye kazi usifanye biashara na wewe unakaa unafurahia tu. Mwanaume anaweza akatoa kila kitu alicho nacho kwa mwanamke wake ila siku za kuishi kwa binadamu ni chache sana. Kesho mwanaume hayuko mwanamke wake aliemfanya kilema ataishije? Maana hata aache Mali atazitapanya ziishe zote
Umenifanya nimekumbuka kuna story ililetwa humu na mtu ambae kaka yake aliwasomesha wao alafu alipokufa wakasahau familia yake. Watoto na mama yao wakapigwa na maisha hatari. Na ni kwasababu hakumuandaa mkewe kwa maisha ya kesho.
 
Kuna watu ujue hawatoi zaka,fungu la 10 wala sadaka ya kuteketeza wala ya kawaida si kanisani wala msikitini...lakini kumpa hata mtu pipi tuu ya 150 anaona dhambi,.basi hata uonge napo 0 jomoniii....mfyuuuu
Hahahaaaa!! Kutotoa sadaka haoni kama ni dhambi ila kukupa mpenzi wake ndio anaona dhambi.
 
Back
Top Bottom