Pasco, heshima mbele mkuu. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar, nilikuwa nina umri wa miaka minne, na sitasahau siku ile ambapo tulila msituni na mamangu pamoja na dadangu katika harakati za kujificha kutokana na watu kuwa wanakimbia huku na kule. Sijawahi sahau hata siku moja. Wakati wa mapinduzi yale, watanganyika hawakuwepo, wala mapinduzi yale hayakufanyika ili baadaye tuje tuunde serikali ya muuungano? Tulifanya yale mapinduzi kwa maslahi ya watu wa zanzibar, na tulikuwa tunaitaka Zanzibar huru na si vinginevyo. Nikiwa kama mhanga wa adha za yale mapinduzi, siwezi kukubali damu ya wazanzibar iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa wazanzibar ipotee bure.
Wazanzibari hadi hivi sasa bado hatupo huru, kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya mambo yetu wenyewe. Wazanzibar tunaamuliwa mambo yetu na watanganyika ambao wanatudanganyishia nafasi za uwaziri na umakamu wa rais. Sisi hatuna shida na nafasi hizo, tunataka zanzibar huru. Tunataka uhuru tulioupigania wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964, utunufaishe wa zanzibar na iwe ni shukurani kwa mashujaa wetu waliopigania uhuru wetu.
Pasco, kwa nafasi yako, yawezekana hicho unachokisema ndo kinadhihirisha msimamo wa serikali ya Tanganyika. Sasa nasema wazanzibar hatujanyamaza katika hili. Tunaendelea na mikakati, wala msijeshangaa siku tutakapo iondoa serikali ya CCM madarakani na kuweka kiongozi mwingine atakayeitangaza Zanzibar kama nchi huru.