Free and Independent Zanzibar

Nawaonea huruma wanaojiita ni wazanzibar wazalendo, maskini ya Mungu wanaponzwa na wawakilishi wao waliopewa nyadhifa kubwa serikali ya Muungano.
Na ndo maana kila hoja inayoletwa ya kuuangalia Muundo wa muungano ili kuweza kuuboresha inapingwa kwa nguvu zote na wawakilishi kutoka Zanzibari. Nashindwa kuelewa nia ya hawa wawakilishi ni nini ? hasa ukitambua hisia na mamazo ya wananchi kuhusu muungano.

Kwa mwendo huu, Zanzibar litaendelea kuwa koloni la Tanganyika huku manung'uniko ya wananchi yakiendelea kuzimwa na hawa wachache.


Hatutegemei hao unaowaita wawakilishi hata kidogo.

Ukombozi wa Zanzibar utaletwa na Wazanzibari wenyewe na hilo haliko mbali
 
Waende tu UN. Hata Wairan wanaoishi Marekani huwa wanaenda kuandamana mbele ya UN pale Ahmedinajad anapokuja kuhutubia.
 
..msitusubiri wa-Tanganyika. kwetu sisi mgao wa umeme, na vita dhidi ya ufisadi, ndiyo priority zetu kwa sasa hivi and in the near future.

..njia ya uhakika na haraka ni wa-Zanzibari kutoshiriki ktk hii inayoitwa serikali ya muungano.

..pia wabunge wote walioko kwenye bunge la muungano watangaze kuachia nafasi zao.

..mkifanya hivyo muungano utakuwa umefikia tamati.

Hawawezi JokaKuu walivyo mafisadi labda wabunge wa CUF sio wa CCM wana tamaa mno!!!! Yote hii ni mikwala tu hakuna kitu.
 
Msema hovyo, itakuwa ulizaliwa baada ya mapinduzi matikufu ya Januari 64 ndio maana inasema hovyo. Uhuru gani huo unaouulizia. Zanzibar si ilipata uhuru wake Desemba 1963?, sasa uhuru gani tena mnaoutaka.

Muungano wetu ni ndoa ya ukweli ya mkeka iliyoongiwa kwa convenience. Ndoa ni ndoa hata ikiingiwa kwa hiari ni binding na haiwezi kuvunjika kwa hiari hata kama mmoja wa wanandoa hakuingia kwa hiyari na kesha ichoka ndoa yanyewe, bado haiwezi kuvunjika.

Ukiona mke amekuchoka na kuanza kukufanyia visa, ujue kesha pata bwana mwingine hivyo anafanya visa ili apewe talaka akajinafasi. Bara tumeshalibaini hilo, tena bwana mwenyewe ni mafuta ambayo hayajai hata kwenye kinibu!. Visa fanyeni, talaka kamwe hatutoi na ndoa itadumu daima. Muungano Milele!

Mungu ibariki Tanzania.

Pasco.
 
Lipeni kwanza deni la Bilioni 50 kwa kuwapatieni umeme, halafu mnasepa tu.

Na wao walipeni pound 600,000 walizoanzishia benki kuu ya Tanzania 1960s na US dollar zao zilizotumika katika vita vya kagera kutoka kwenye mauzo ya karafuu yaliyopita.

Dharau mkuu hazitaleta mwafaka wala kuelewana hekima na demokrasia ndio solution ya muungano huu. Serikali 3 au muungano kuvunjika kabisa kwa ustaarabu.
 
Zanzibar walikuwa na kiti UN wakaki surander kwa ridhaa yao wenyewe hivyo kwenye UN, Zanzibar doesn't exist anymore, so does Tanganyika, iliyopo ni Tanzania tuu. Hata waandamane na mabango mpaka mbinguni, it won't change a thing!.
 
Hakuna mwana JF anayewang'ang'ania kama Msema Hovyo anavyodai humu. Wengi wamekujibu na wanasema jiondoeni, nendeni nk. Sasa wewe unadai wanawang'ang'ania.

Si mmepata mwafaka na CCM? Sasa hapa si makao yao makuu. Hamkukutana humu. Maoni yetu wengi wetu ni chukueni nchi yenu, viongozi wenu wa CUF wamewaingiza mkenge, badala ya kuwabana mnakuja lia lia humu. Kwani hamjamsikia Lissu huko bungeni? Umeangukia humu lakini ulipojikwaa ni somewhere else. Please go and check.
 
Tatizo ni hao Baraza la Wawakilishi hawatataka kabisaaa kuondoka kwenye Muungano maana hawana uhakika kama kweli hizo keki za mafuta watafaidi au watakuja watu wengine na kuwafukuzilia mbali.

Hawa watu wa CCM huko Zanzibar ndiyo tatizo hasa na CCM Bara wanajua kuwavimbisha matumbo yao. Hebu kumbuka jinsi Dr. Hamad wa CUF alivyokuwa mkali wa POSHO na kutaka kuvunja sheria ili aanzishe Kambi ya upinzani isiyo Rasmi. Na mwisho malizilia huyu Maalim Seif aliyekula matapishi yake mwenyewe.



..msitusubiri wa-Tanganyika. kwetu sisi mgao wa umeme, na vita dhidi ya ufisadi, ndiyo priority zetu kwa sasa hivi and in the near future.

..njia ya uhakika na haraka ni wa-Zanzibari kutoshiriki ktk hii inayoitwa serikali ya muungano.

..pia wabunge wote walioko kwenye bunge la muungano watangaze kuachia nafasi zao.

..mkifanya hivyo muungano utakuwa umefikia tamati.
 
Last edited by a moderator:
Wale wote wenye wishful thinking muungano uvunjike, nawapa pole kwa vile hilo halitatokea. Wenye uwezo wa kulisukuma hilo mbele, wameshalambishwa asali hivyo wako bize kusikilizia utamu huku wakijiandaa kuchonga mizinga.
 
Sasa kama mmetuchoka mbona mnaendelea kutung'ang'ania? Mara ngapi wabunge wazanzibar wamelalamika kuhusu muungano, nyie mnawatishia wasiendelee kusema. Kama mngewapa uhuru wa kusema wanachokifikiria naamini kabisa wangewapa ukweli kwamba wazanzibar hatutaki muungano.

Hatujawachoka Msema Hovyo, tumechoka kuwabeba
 
Ukombozi wa zanzibar, if at all utatokea, utakuwa ndiyo ukombozi wa Tanganyika in disguise!! we are fed up with ungrateful zanzibaris!! Go away and disappear asap!!
 
hao wanao andamana wanamwakisha nani?
huu muungano ni tatizo la kudumu kama kila muhuni anaweza kuusemea
 
Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbili zilizoungana mwaka 1964 na kupatikana TANZANIA. Je, muungano huu unamanufaa kwa pande zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar?
 
Mimi nayashangaa haya maviongozi yetu kwa nini yana ng'ang'ania nchi ya watu. Visiwa vyenyewe vidogo kuliko hata wilaya yoyote iliyo ndogo kuliko zote hapa Tanganyika. Haya Mazanzibari tuyaache yakachinjane yenyewe kwa yenyewe kwa sababu hayo Mapemba na Maunguja hayatakaa meza moja. Hivi sasa yana kaa meza moja kwa sababu yako ndani ya Muungano. Natamani siku moja nione maneno haya: JAMHURI YA WATU WA TANGANYIKA!

Ewe Mwenyezi Mungu, kama ulivyomruhusu Simon amwone mtoto Yesu ndipo afariki dunia nami pia nijaalie nione taifa langu ndipo nilale mauti. Nimechoshwa vya kutosha na kelele za Wazanzibari!

images


Kwani ninyi kinachowazuia kuwa na hiyo serikali ya jamhuri ya watu wa Tanganyika ni nini? Kwanini msiamua kufanya hivyo ili wazanzibar tuwe huru. Tumechoka kukandamizwa na Tanganyika.
 
Back
Top Bottom