Free and Independent Zanzibar

Free and Independent Zanzibar

Babu yangu aliwahi kunihadithia.
Ukina mke wako anakusumbua sana kwa kutaka talaka kwa sababu ambazo hazina msingi-ujue kuna mume mwenzio pembeni.
Hii imekaaje wana JF Wazanzibari wachache wamekomalia kuataka kuvunja muungano, pamoja na kuwa waTanganyika tumechoka na hizi chokochoko zisizoisha , kuna msukumo toka nje?
 
Fine, lakini mkumbuke kwamba ni lazima iwe declared before international acts kwamba sasa imekuwa ni nchi halali. Ndiyo maana tunasema tunataka uhuru wetu. Mkubali kwamba mnatuacha tuishi na kujijenga kama nchi, mdeclare mbele ya sheria zote za kimataifa zitakazoitambua zanzibar kama nchi, na si kirahisi rahisi hivyo kusema eti tuachie madaraka tuende zetu! Halafu tukifanya hivyo? Nani atakayetutambua kwamba ni nchi?Mchakato uanze sasa, mturuhusu wananchi wa zanzibar tupige kura ya bila kampeni kama tunataka muungano or not? Hii kura ndiyo kitakuwa kigezo mhimu cha kuitangaza zanzibar kama nchi huru. Hivi sasa watanganyika mmejitahidi sana kuzuia mijadala yote inayohusu muungano kwa kuhofia kwamba zanzibar itajitenga. Lakini someni alama za nyakati. Tayari watanganyika wanachomewa maduka zanzibar na tayari makanisa, mabaa na mabucha ya nguruwe yanasambaratishwa kule. Ni dalili tosha kwamba hatuwahitaji wageni tena. Tunataka nchi yetu huru.
kwa hiyo na sisi tuwachomee maduka yenu huku bara?!
 
Mh umekosea sana wanawake na analogy hii. Kumbuka wanawake ni mama zetu, dada zetu , wapenzi wetu. Si vizuri kuwa tusi hivi.
 
Huo ni mfano tu. Bora wafe kibudu manake tumewachoka kwa kuendekeza udini nchi hii.
 
kuwa na adabu na heshima
kama zamani walikuwa taifa huru
wana haki ya kutaka kuwa huru tena

matusi yako yanaongeza hasira
nahisi umetumwa labda,kuwatukana na kuwachokoza wazanzibari
 
Ina maana wewe na akili zako zote unashindwa kuiona tofauti iliyopo kati ya bendera ya Tanganyika na Tanzania? Na bado unashindwa kuiona tofauti kwenye nembo hizo? Kuwa serious kidogo. Pengine ungeuliza kuna tofauti kwa kiwango gani? ngoja nikufafanulie tofauti zake ambazo ni kubwa sana ambazo zinazifanya bendera hizo na ngao zisifanane abadani ingawa zina rangi zinazokaribiana kama ilivyo kwa bendera ya Kenya na Sudani Kusini.Tofauti ya bendera ya Tanganyika na Tanzania ni kuwa ya Tanganyika haina rangi ya bluu halafu mistari yake imelala....Tofauti ya ngao ni kuwa ngao ya Tanganyika ndani yake ina bendera ya Tanganyika na ngao ya Tanzania ndani ina bendera ya Tanzania.Swali sasa. Hizo siyo tofauti? Ama ulitaka tofauti za kivipi kwa mfano?Idumu Tanganyika!
yakhee Weye acha ubishi yakhee hakuna kilichobadilika hapo, ni sawa na mwanamke labda mariam au amina kupaka wanja au poda but anabaki kuwa mariam au amina yule yule yakhee, Muulizeni karume vizuri mana ndio msomi wenu huyo yakhee.
 
Endeleeni kuomba uhuru tukiridhika basi tutawapa, klakini lazima muoneshe uwezo wa kujitegemea msije mkatufia
 
kuwa na adabu na heshimakama zamani walikuwa taifa huruwana haki ya kutaka kuwa huru tenamatusi yako yanaongeza hasiranahisi umetumwa labda,kuwatukana na kuwachokoza wazanzibari
wee nawe kwani hizi kero huzioni?hawa wanatulaumu sana wa bara,wanatubagua na kututenga wakijiita wazanzibar, hatuwalazishi kuwa nao kama vp wasepe tu.
 
I think we should get used to the idea that one day or next few years Zanzibar will be Independent from its ever meddling mainland partner: Tanganyika.

And become economically and socially dependent on Oman. We wish you the best of luck in your struggle.
 
Really? any particular reasons
U r an African and blood related to the Coastal People of Tanzania (though u call us vichogo and every bad names u know) even landwise! i suppose Zanzibar landmass was part of Pwani e.g. Bagamoyo and one day our ancestors from the mainland woke up and found a serious trench occupied with water and part of their land has disappeared with some of their brothers and sisters! They deviced a means to find them through boats and they continued with their brotherhood till when Arabs from Oman came and introduce Islamic religion plus their culture that indoctrinated a belief that u r related to them! These Arabs enslave most of u in the Islands till a day ur blood and race related brothers organized a coup to salvate you! But guess what after years of Freedom now you want to go back to ur slave master! Its a dangerous path you want to take my brother neither the US nor the EU will allow that since your motives has some elements of extremism and will distabilize the region to prove a point the EU+US have started to deal with your supporters first Egypt then now Libya and as a result Southern Sudan gain independence since no financial backers were there to help them financial on their war against the South as usually! Pls try to learn from fellow Africans from Southern Sudan, they later realized an African can never be an Arab by mere chance of just speaking their language and imitating their culture! a nigger will be a nigger!?
 
sipati picha siku muungano umevunjika jinsi wapemba watakavyojaa bandari wakisubiri vyombo kurudi ktk zanzibar iliyo huru, sa nyumba zao sijui zitauzwa? au zitafanywa gest? hivi watatosha kweli? watakao amua kubaki tanganyika itabidi waishi kwa permit, dah ulaji huo kwa uhamiaji maana hata hawajifichi.
 
Those in favour of independence say aye,,those opposed say nay. Coming soon at theatre near you.
 
Zanzibar will be free and independent once again. Sooner rather than later.

Cant wait to see their backs.

Zanzibar for Zanzibaris.
 
sipati picha siku muungano umevunjika jinsi wapemba watakavyojaa bandari wakisubiri vyombo kurudi ktk zanzibar iliyo huru, sa nyumba zao sijui zitauzwa? au zitafanywa gest? hivi watatosha kweli? watakao amua kubaki tanganyika itabidi waishi kwa permit, dah ulaji huo kwa uhamiaji maana hata hawajifichi.

Hilo ndilo mnalongojea. Majumba wajenge wengine, nyinyi mngojee muyapore na ya kufisidi.

Wapemba watarudi kwao wala hawakataliwi.

Lakini Wapemba wako katika nchi nyingi duniani na wala hatungana nazo.

Nawasikitikia nyinyi Watanganyika, mnaouza nchi yenu kwa magabachori.

Nchi tajiri, watu wake maskini kutokana na kuendekeza pombe na ufisadi
 
Nyie wazenji mkivunja muungano huu, haitawasaidia chochote isipokuwa kutengana wenyewe kati ya wapemba na waunguja. napita tu
 
Nyie wazenji mkivunja muungano huu, haitawasaidia chochote isipokuwa kutengana wenyewe kati ya wapemba na waunguja. napita tu

na hawa watu kinachowaunganisha ni huu muungano tu, lakini pale ni km chui na paka.
 
Pasco, heshima mbele mkuu. Siku ya mapinduzi ya Zanzibar, nilikuwa nina umri wa miaka minne, na sitasahau siku ile ambapo tulila msituni na mamangu pamoja na dadangu katika harakati za kujificha kutokana na watu kuwa wanakimbia huku na kule. Sijawahi sahau hata siku moja. Wakati wa mapinduzi yale, watanganyika hawakuwepo, wala mapinduzi yale hayakufanyika ili baadaye tuje tuunde serikali ya muuungano? Tulifanya yale mapinduzi kwa maslahi ya watu wa zanzibar, na tulikuwa tunaitaka Zanzibar huru na si vinginevyo. Nikiwa kama mhanga wa adha za yale mapinduzi, siwezi kukubali damu ya wazanzibar iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa wazanzibar ipotee bure.

Wazanzibari hadi hivi sasa bado hatupo huru, kwa kuwa hatuna uwezo wa kufanya mambo yetu wenyewe. Wazanzibar tunaamuliwa mambo yetu na watanganyika ambao wanatudanganyishia nafasi za uwaziri na umakamu wa rais. Sisi hatuna shida na nafasi hizo, tunataka zanzibar huru. Tunataka uhuru tulioupigania wakati wa mapinduzi ya mwaka 1964, utunufaishe wa zanzibar na iwe ni shukurani kwa mashujaa wetu waliopigania uhuru wetu.

Pasco, kwa nafasi yako, yawezekana hicho unachokisema ndo kinadhihirisha msimamo wa serikali ya Tanganyika. Sasa nasema wazanzibar hatujanyamaza katika hili. Tunaendelea na mikakati, wala msijeshangaa siku tutakapo iondoa serikali ya CCM madarakani na kuweka kiongozi mwingine atakayeitangaza Zanzibar kama nchi huru.
Msema hovyo, kwanza samahani kwa kuku under estimate kuwa huujui uhuru wa Zanzibar, pili nilipoona jina lako la Msema hovyo, nikadhania wewe ni msema hovyo kweli, kumbe ni jina tuu.

Pole kwa kuwa ni muhanga wa Mapinduzi yale sasa naomba tubishane kwa hoja based on facts na sio hisia tuu.

1. Kwanza tukubaliane, Zanzibar ilipata uhuru Desemba, 1963, that is a fact, you can't deny. Hivyo Zanzibar inachokitaka sasa sio uhuru, bali restoration ya its soverenity iliyoipoteza kwenye muungano na sio uhuru.

2. Pili, 'Umoja ni Nguvu', hivyo muungano wowote wenye nia ya kuleta umoja, ji jambo jema, ni jambo la kheri, licha ya kuwepo matatizo haya na yale. Hii inamaana, ukiondoa kero za muungano, muungano ni jambo la kheri.

3. Na tatu tukubaliane sababu zilizopelekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati ule zilikuwa valid na tena kwa nia njema ya usalama wa Zanzibar hata kama ghara yake ni ustawi hasi. Hebu ifikirie Zanzibar bila Muungano, ingekuwa Zanzibar gani?. Si mgeishia kuchinjana kila kukicha?. Just imagine, japo ulikuwa mdogo wa miaka 4 tuu wakati wa Mapinduzi, mimi nimesoma accont ya mlichowafanya Waarabu kwenye mapinduzi yale, hakuna aliyeandika wala unyama wa mapinduzi hayo haupaswi kuhadithiwa, itakuwa ni kujenga chuki na kutonyesha vidonda kwa waliofiliwa. Bila muungano, manowari ya Uingereza ilishatia nanga Mombasa, tayari kuvamia Zanzibar na kumrudisha Sultan Jamseed. Jee Sultan angerudi, unaweza kuimagine hatima ya wanamapinduzi?. Lazima mumshukuru sana Nyerere na Karume ndio maana wengine wenu mpaka leo mnaweza kukohoa kudai uhuru.

Nakubaliana nanyi kuwa sababu zilizopelekea muungano doesn't exist anymore na pia makubaliano yale ya msingi yameshakiukwa na kupindishwa na kuongezwa bila ridhaa ya upande wa pili kulikopelekea muungano huu kuzongwa na kero lukuki, dawa ya kero hizi ni kuzitatua na kuzirekebisha na sio kuuvunja muungano.

Kwa vile muungano iliingiwa kwa nia njema 'in good faith', naomba hata tunapojadili maslahi ya Zanzibar kwenye muungano huu, tudadili in good faith tukitanguliza utaifa mbele na kuacha hisia nyuma.

Nakuhakikishia wewe Msema hovyo na wengine wa aina yako, hata ikitokea muungano ukavunjika leo, kesho, Zanzibar hamtabaki salama kama mnavyojidhania, wale mliowachinjia baba zao na mama zao kwenye mapinduzi yale, na kuwabakia binti zao huku wengine mkijitwalia kuwafanya wake zunu, damu yao itawashukia na utafika muda, jambia zitatembea tena!.

Tukiuvunja muungano huu uliopo sasa, Wazanzibari ndio watakuwa the biggest loosers maana ni Zanzibar ndio ina gain the most ndani muunganu huu at the expense of sisi wabara!
 
Pasco, kuhusu uhuru nafikiri somewhere tumeargue pia na mwanakijiji. Wazanzibari tunaujua lakini hatuutambui uhuru wa 1963, ambao alikabidhiwa Sultani. Ule haukuwa uhuru wetu sisi, kwani wewe Pasco ulishawahi kuona Zanzibar wanasherehekea uhuru wa December 1963? Sisi uhuru kamili tuliupata 12/01/1964 pale tulipofanikiwa kuifanya nchi kuwa mali yetu wazanzibar weusi wazalendo. Nafikiri Pasco kama umefuatili kwa karibu historia ya Zanzibar utakuwa unajua kabisa ni namna gani ambavyo ushindi wa Chama cha ASP ulikuwa unaporwa na waarabu, hadi kufikia kuifanya ASP kutumia nguvu kurudisha utawala mikononi mwa wazanzibar. Kwetu sisi uhuru ni ule wa mapinduzi ya zanzibar na ndiyo maana tutayaenzi mapinduzi daima.

Naona umeongea sana kuhusu umoja ni nguvu na habari za sisi kuuana sisi kwa sisi. Nafikiri Pasco kuna kitu hapa umeamua kujifanya hukielewi au kwa makusudi umeamua kuupotosha umma wa watanzania kuhusu zanzibar. Hivyo visa na visasi vya mwaka 1964, kama vingeendelea kuwepo, kwa hakika tusingeshindwa kuuana hata kama tupo ndani ya muungano. Muungano umesaidia nini kuzuia watu wasilipane visasi vya mauaji yale? Na unafikiri muungano ukivunjika, nini kitasababisha watu wakumbuke machungu ya mapinduzi? Hapa Pasco sikubaliani na wewe hata kidogo.

Na kwa upande mwingine unaongelea habari ya umoja ni nguvu, yes hakuna anayekataa hilo, lakini hakuna haja ya kuwa katika umoja ambao hauna faida. Tunaweza kuvunja muungano, Zanzibar ikawa nchi huru na yet tukaungana kama federation. Wote tukawa washirika katika East Africa Federation. Kwanini nyinyi mnataka sisi tuwe nchi moja na nyie wakati mna mamlaka yenu na maamuzi yenu, ambayo mengi yao wazanzibar hatuhusishwi?

Na mwisho nataka ieleweke kwamba hakuna ushahidi wowote beyond reasonable doubt unaoonyesha kwamba Tanganyika inaibeba Zanzibar. Mna nini cha ziada nyie watanganyika ambacho zanzibar hatuna? Wakati tunaamua kuutafuta uhuru na hata kumpiga sultani tulijua kwamba tunaouwezo wa kujitegemea na tulijua kwamba tunaweza kuiendesha zanzibar huru kwa nguvu zetu wenyewe. Sasa kusema kwamba tunabebwa ni dharau kwa wazanzibar ambao walimwaga damu wakati wa mapinduzi ya 1964.

Umeongelea habari ya waingereza kutia nanga mombasa tayari kwa kuirudisha zanzibar kwa sultani wa oman. Nadhani katika hili pia umeamua kuupotosha umma. Ninakumbuka vizuri sana taarifa zilizoenea wakati huo juu ya kurudi kwa waingereza,tulikaa mafichoni kwa zaidi ya wiki kama tatu baada ya mapinduzi, tukila mtunda na madafu kwa kuhofia machafuko mengine yatokanayo na ujio mpya wa waingereza. Je unajua kwanini waingereza hawakuivamia Zanzibar ili kuirudisha kwa Sultani? Unaweza kuuhakikishia umma kwamba waingereza hawakuivamia zanzibar kwa sababu ya muungano? Mimi naomba nisiseme kitu juu ya hilo, manake naweza onekana mchochezi. Lakini kwa taarifa yako millions of Arabs were already dead. Huyo Sultan angerudi aje awaongoze akina nani? Fuatilia vizuri mkuu uelewe kwanini uvamizi wa waingereza hakufanyika. Kwamba hawakuvamia kwa kisingizio cha muungano, nafikiri tutakuwa tunapotosha.

Lakini pia nashukuru kwamba umenirekebisha mahali fulani kwamba kwa sababu tulishapata uhuru mara ya kwanza sasa tuombe restoration ya sovereignty ya wazanzibari na si uhuru. Hilo nakubaliana na wewe. Maana tayari tuna kila kitu kinachotupa haki ya kuwa nchi, isipokuwa uhuru wetu umebakwa na watanganyika. So turudishieni ule uhuru muliotuibia men.
 
swala la muungano huu wetu linatutafuna sana......

nimepata pdf hii toka CIA nimejua kuwa muungano ni batili kabisa.kweli nyerere alimzidi karume ujanja

http://www.foia.cia.gov/CPE/ESAU/esau-28.pdf

baada ya hii ntawaletea nyingine inayohusu utawala huu wa sasa

NB . chanzo cha muungano kipo page ya 118.....
 
Back
Top Bottom