Foleni za magari ni maisha bora - Kikwete

Njia za kupunguza foleni ni

3) Makosa ya usalama barabarani yasilipishwe faini, askari wa usalama barabarani wakae na marungu, kosa dogo wavunje endiketa, linalozidi taa za mbele, kosa kubwa kioo na kuendelea. Na ukivunjiwa taa, askari wa mbele unakokwenda akikushika, anakuvunjia nyingine.

.

Hapo naamini unatania ndugu yangu - maana hilo likitendeka tutaendeleza utawala wa kiimla.
 
Njia za kupunguza foleni ni
1) Kuuchora mpaya mji, na maafa yake ni kuwa wengi itabidi wabomolewe majumba. Mfano Dubai.

2) Kuboresha usafiri wa jamii, bus, trains na kuzuia magari kuingia katikati ya mji kwa kutoza toll za kuingilia mjini na parking za mjini zizidishwe bei. Mfano, London.

3) Makosa ya usalama barabarani yasilipishwe faini, askari wa usalama barabarani wakae na marungu, kosa dogo wavunje endiketa, linalozidi taa za mbele, kosa kubwa kioo na kuendelea. Na ukivunjiwa taa, askari wa mbele unakokwenda akikushika, anakuvunjia nyingine.

4) Kuzuwia magari yenye umri wa zaidi ya miaka 5 toka yaundwe yasiingizwe nchini.

4) Kudhibiti wanaotowa na kupokea rushwa jeshi la polisi, hususan askari wa usalama barabarani. Anaekamatwa kutoa au kupokea rushwa auliwe kwa kupigwa risasi hadharani.
Hiyo njia ya tatu aisee!! Hiyo ya mwisho ingetumika kwa watu wote nadhani tutakuwa na heshima!
 
Jamani pia ujenzi wa maghorofa marefu katikati ya jiji ungepigwa marufuku mara moja. Kila ghorofa refu jipya linasababisha magari tele kuja katikati ya jiji. Mji usambae kuelekea pembeni sio kwenda juu.
 
Hilo alilolisema, kuna nchi wanalitumia na linafanyika kwa ufanisi mkubwa sana sana.

Mkuu, kama kweli ni wazo lako basi HONGERA sana kwa kuliona hilo bila ya KUSOMA.

Kwenye Traffic Engineering kuna utaratibu kama huo. Na hali halisi huwa inakuwa hivi:

1. Kunakuwa na LANE special kwa Mabasi yaendayo kasi na huko huwa wanaruhusu TAXI na Mabasi tu.

2. Kama ikionekana Mabasi na Taxi ziko chache na kuna nafasi kidogo kwenye hiyo Lane, basi wanaweza kuruhusu mtu yeyote mwenye gari na abiria kuanzia 5 kwenda juu (hao abiria lazima wawemo ndani), gari hilo linaweza kuingia kwenye lane ya MABASI na kuwahi MJINI au NYUMBANI haraka.

3. Ili kuleta ULINZI wa mwenye GARI na Abiria, kunakuwa na DATABASE kwenye ofisi fulani hata kama zitakuwa za mitaani na mtu mwenye gari anakwenda kujiandikisha hapo na kila mwenye kuhitaji usafiri wa LIFT kwa mtu na yeye anakwenda kujiandikisha hapo. Sasa ikifika asubuhi, kila mtu anafahamu wapi akasubiri LIFT yake. Gari linakuja na unachukua abiria wako (nafikiri zaidi watakuwa wanafunzi) na kuwabeba mjini kwa kupita LANE iliyotengwa kwa mabasi.

Mwenye gari anakuwa ANAWAHITAJI abiria hao ili ndani kuwe na watu 5 na abiria wanakuwa na LIFT haraka kwenda mjini au kurudi nyumbani. Magari badala ya kutembea TUPU, yanakuwa yanatumika yote.

Ni kutumia kidogo tulichonacho/mlichonacho katika efficients ya juu kabisa.........

Dubai-Have-Exclusive.jpg
C_67_article_2049764_body_articleblock_0_bodyimage.jpg

siebuslane.jpeg

Hapa chini, muangalie jinsi MAGARI yanavyochukua nafasi kubwa barabarani. Ndiyo maana nchi kubwa zote, mijini wanatumia Trains, Trams, Metro za juu na chini, mabasi yenye LANES special (angalia juu picha)........

tampa_capacity.jpg

The same 40 people
. . . (1) in their cars,
. . . (2) seated at car spacing,
. . . (3) seated at bus passenger spacing,
. . . (4) as pedestrians and bicyclists.
(From: TreeHugger Forums • View topic - Imagine Your City Without Cars.). Angalia hiyo PAGE kwa faida zaidi.
 
kila m2 ana mawazo yake jamani! nami hilo ndo wazo langu so sijalazimisha kila m2 akubaliane nalo!! i know what im talking, sio lazima wa2 wawapakie watu wengine bt kama familia inaweza tumia gari moja instead of magari sita incase wako sita. Preta wewe ndo unachekesha
vipi kwa sasa tanzania hatuna hizo fly overs? au tuanze tu kupaa angani? fikiri kabla
Kama hao ndugu hawaendi sehemu moja inakuwaje?
 
mfano mkubwa pale unapokuwa ndani ya bus, ukiangalia pembeni utaona private cars zikiwa na m2 mmoja mmoja, sasa nikakaaa na kufikiria, iwekwe sheria ni marufuku kuendesha gari ukiwa pekeako atleast wawepo wa2 watatu na kuendelea, najua kwa wenye private cars itakua ni tatizo lkn kwa sisi watumia public transport nadhani tutachekelea pia wadosi watajifunza kutoa lift kwa majirani au familia kutumia gari moja badala ya baba na gari yake, mama yake, na kila mtoto yake. hapo mnaonaje wana JF?
Mkuu hapo kwenye blue hakuna mdosi anaekaa Kimala, Yombo, Gogolamboto, Kwa mtogole, Chanika, Vingunguti, Jet
 
Ofisi za wizara na taasisi mbalimbali zijengwe pembezoni mwa jiji. Itapunguza foleni. Nina mfano hai ambao niliufanyia research. Katika wizara moja iliyopo jirani na Jk kuna watu wasiopungua 20 wote wana magari na wanapita barabara moja kila asubuhi wanapoenda kazini na kila jioni wanaporudi, wote wanaishi vitongoji jirani umbali wa km 20 toka city center,mara nyingi wanaondoka muda mmoja na kurudi muda mmoja na hao ni wafanyakazi,sijahesabu wananchi wanaoenda pale kwa shida zao mbalimbali. Na hiyo ni wizara au taasisi moja,tuna wizara/taasisi/mabenki/makampuni mangapi pale katikati ya jiji? Hayo si sawa na kuna maandamano yasiyo rasmi kila siku barabarani kuelekea katikati ya jiji letu!. Tunaweza kubadili hali hii!
 
kila m2 ana mawazo yake jamani! nami hilo ndo wazo langu so sijalazimisha kila m2 akubaliane nalo!! i know what im talking, sio lazima wa2 wawapakie watu wengine bt kama familia inaweza tumia gari moja instead of magari sita incase wako sita. Preta wewe ndo unachekesha
vipi kwa sasa tanzania hatuna hizo fly overs? au tuanze tu kupaa angani? fikiri kabla
Wazo butu unaleta hapa unategemea watu wakusurpot kwenye upupu??kesho utasema tuchangiane na kwa wake zetu kwa watu walioshindwa kuoa kwa sababu ya gharama!!
 
Labda tujaribu haya:

1.Tumejaliwa hali ya hewa nzuri Africa, kwa nini tusipande baiskeli ili kuwahi maofisini, shuleni nk? at the same time unakuwa unafanya sport. Huwa naitumia sana hii njia mimi binafsi.
2. Kama mnakaa majirani na wote mnaelekea sehemu moja ya kazi au karibu karibu, basi mnaweza kupokezana zamu ya kuendesha leo mimi kesho wewe, hapa unasevu mafuta na pia unapunguza foleni barabarani.
3. Serikali, mashirika watu binafsi wawekeze kwenye mabasi makubwa ambayo yanabeba watu wengi kwa mkupuo hivyo kupunguza vipanya vinavyojaza foleni.
Mwisho sio mbaya ukatembea kwa mguu kama sehemu unayoenda sio mbali au huna mziggo wa kubeba, hii itakusadia kufanya zoezi la mwili. Kutembea kwa mguu kusichukuliwe kama vile mtu kaishiwa na pia tuache kasumba ya show off....
 
Mi nafikiri itungwe sheria ya makampuni makubwa yenye wafanyakazi wengi kama vile makampuni ya simu, mabenki, mifuko ya hifadhi na mengine yawe na staff buses. Mfano wa bank utakuta mpaka teller anaenda ofisini na private car, wako wangapi? Zamani ilikuwepo hiyo kitu ya staff buses kwa makampuni mbalimbali.
Nawasilisha.
 
wazo zuri ila wafanyakazi hawakai sehemu moja, chukulia mfano wengine wanaishi tegeta, kibamba na g'mboto.. Je kampuni iwe na magari matatu kwa ruti hizo? (hapo idadi ya magari hujapunguza) au iwe na gari moja kwa ruti zote 3 ( kazini watafika on time ikiwa hivyo?).
 
Mii simo manyage yunyenye!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Nene ndeemaaaaaaaaa

mfano mkubwa pale unapokuwa ndani ya bus, ukiangalia pembeni utaona private cars zikiwa na m2 mmoja mmoja, sasa nikakaaa na kufikiria, iwekwe sheria ni marufuku kuendesha gari ukiwa pekeako atleast wawepo wa2 watatu na kuendelea, najua kwa wenye private cars itakua ni tatizo lkn kwa sisi watumia public transport nadhani tutachekelea pia wadosi watajifunza kutoa lift kwa majirani au familia kutumia gari moja badala ya baba na gari yake, mama yake, na kila mtoto yake. hapo mnaonaje wana JF?
 
Aisee huyu jamaa sio Mtanzania tumsamehe Bure. Inamaana unapowapa watu Lift Ndio foleni inapungua?
Hii ni kali aisee. Tunaweza kupunguza foleni by:
1. Fy overs kwenye mataa.
2. Kuongeza parking fee katikati ya Mji.(many ppl will use public transport)
3. Ofisi zote za Serikali ziondolewe katikati ya Mji.
4.
5.

Ungeanza kwanza kupendekeza kuboresha hiyo huduma ya Public transport, huko wanakotumia huduma hiyo na kuacha kutumia magari yao huduma haiko kama ilivyo hapa kwetu. Vipanya?
 
ndugu wana jf. Hiyo ni kauli ya Rais ambayo aliwahi kuitoa Akimaanisha Foleni ya Dar ni ishara ya maisha bora. Nadhan ndo maisha bora aliyoahidi ndugu zangu,mnasubiri yapi tena?
 
Back
Top Bottom