Flyover bila hesabu ni hatari, hapo ni TAZARA leo hii

Tumeshuhudia mvua iliyonyesha leo hii jijini dsm na kusababisha baadhi ya maeneo kufurika maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji pia na miundo mbinu husika iliyojengwa kwa pesa za mvuja jasho
Hapo pichani ni Tazara flyover tazameni hali ilivyo kwa mvua moja tu ya leo!View attachment 1036989

In God we Trust
Acha tuzibe midomo yetu... wakubwa huwa hawakosei hata kama hasara itakuwa kama yote
 
Me Naona poa tu maji yataisha kahasara kadogo ukizingatia na miaka ile
Kama kahasara kadogo tu cha koro-show?

Tumezoea kugawiwa umaskini mbele kwa mbele. walisahau kuweka (nyufa) joints kama za UDSM Magufuli hostels?

Nunua kitambulisho bandugu kuunga juhudi ili zipatikane fedha za kuwekea mifereji ya kuondoa maji hayo mvua zinaponyesha.

Hapo panaonekna kama "ulaya" vile. Pamependeza sana. Awamu hii inajitahidi sana kuinyoosha nchi.

Wacha tukae kimya tu kama Mkodoa macho Kabudi alivyotuamrisha.
 
Mkuu Hata Marekani hebu tizama hii

1551820261282.png

Harvey: This is probably the worst US flood storm ever; I’ll never be the same
From the archives: The fourth largest US city, Houston, changed forever one year ago.

1551820535435.png

Washington pia
 
Mleta mada ni mchochezi,hayo maji hua yanajaa ikinyesha mvua kabla hata ya fly over,sio wote jf wanakaa katavi,wengine tumekulia Mwisho wa Lami Gongo la Mboto
 
Acha majigambo yasiyo na maana.Kusoma lugha au historia sio tatizo.Wewe uliyesoma uhandisi ulitakiwa ueleze kitaalamu tatizo liliotokea.

Lakini nilichogundua,una tatizo pia la kutoelewa lugha ya kuelezea kilichotokea.Historia ina umuhimu wake kwako na kwa wengine pia.

Acha dharau.

Chipolopolo, hebu soma kichwa cha Habari cha mada hii halafu useme mwenye dharau ni nani kati ya mleta mada anayebeza na kutukana kwamba daraja limejengwa bila hesabu (na wote mnaounga mkono), na mimi ninayeshauri kuwa makini unapotoa hoja.
 
Tumeshuhudia mvua iliyonyesha leo hii jijini dsm na kusababisha baadhi ya maeneo kufurika maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji pia na miundo mbinu husika iliyojengwa kwa pesa za mvuja jasho
Hapo pichani ni Tazara flyover tazameni hali ilivyo kwa mvua moja tu ya leo!View attachment 1036989

In God we Trust
Ni Tanzania pekee ambapo watu wanafurahi kwa kuona mabaya na kuchukia kwa kuona mazuri yanatendeka kwenye jamii yao

Ilah hamna namna kwa kuwa sisi Ni waafrika na akili zetu ni Kama za waafrika wengine
 
Tumeshuhudia mvua iliyonyesha leo hii jijini dsm na kusababisha baadhi ya maeneo kufurika maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji pia na miundo mbinu husika iliyojengwa kwa pesa za mvuja jasho
Hapo pichani ni Tazara flyover tazameni hali ilivyo kwa mvua moja tu ya leo!View attachment 1036989

In God we Trust
Acha projo za kisiasa kwa miradi ya kitaifa mzee wangu. Kwani mantiki yako unadhani Houston nao hawakuwa na mahesabu walipjenga haya maflyover makubwa kama haya eti bali walitumia vibaya hela za walipa kodi wao?
1551826085540.jpeg

Au haya mafuriko yaliyotokea Paris Ufaransa naoa unadhani walijenga hayo maflyover bila hesabeu
1551826380045.png

Haya mambo ya mvua za kuzidi kiwango ni tatizo la dunia siyo tatizo la Dar es salaam, wala tatizo la serikali ya Tanzania. Furtahia sasa tuna Flyover wala hatupigi foleni tena eneo hilo
 
Hivi hakunaga mhandisi mkazi, ambae wanapokuja wakandarasi wakigeni awaambie mazingira huwa yanakuwaje kipindi cha mvua ili wanapotutengenezea hizi barabara basi pasijekutokea mambo kama haya?
Shida sio mkazi... Company inatakiwa ijue hilo maana hawakurupiki tuu kuanza kujenga.. Shida ni sisi hatuna standard

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida sio mkazi... Company inatakiwa ijue hilo maana hawakurupiki tuu kuanza kujenga.. Shida ni sisi hatuna standard

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna barabara zinajengwa kwa matamko mkuu, "nataka mpaka ikifika mwezi wa 6 barabara hii iwe imekamilika na inapitika, tumeelewana."
Wakati eneo hilo, mvua zinagonga mwezi wa tisa na kuendelea, unafikiri hapo bila ya kuwa na mhandisi mkazi, huyo mkandarasi si atapuyanga tu mkuu
 
Shida sio mkazi... Company inatakiwa ijue hilo maana hawakurupiki tuu kuanza kujenga.. Shida ni sisi hatuna standard

Sent using Jamii Forums mobile app

Edwayne, mimi si mhandisi lakini nimefanya kazi na Wahandisi waliobobea kimataifa kwa miaka zaidi ya 35. Sikubaliani kabisa na hoja yako ya viwango (standards) eti sisi hatuna viwango. Kwa kifupi inawezekana ulitaka kusema vingine ila kwa sababu ya haraka umeandika kuhusu standards kwa vile tu neno hilo limekuja karibu. Hata hivyo standards unazozisema hazihusiani na tatizo linalozungumzwa hapa.
 
Nakanusha,hii picha sio ya Draja letu liliko ndani ya mmiliki wa jiji Makonda na ndani ya Serikali ya 'baba mdogo'
 
Back
Top Bottom