Flyover bila hesabu ni hatari, hapo ni TAZARA leo hii

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Tumeshuhudia mvua iliyonyesha leo hii jijini dsm na kusababisha baadhi ya maeneo kufurika maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji pia na miundo mbinu husika iliyojengwa kwa pesa za mvuja jasho
Hapo pichani ni Tazara flyover tazameni hali ilivyo kwa mvua moja tu ya leo!
FB_IMG_1551621978914.jpeg


In God we Trust
 
Hivi hakunaga mhandisi mkazi, ambae wanapokuja wakandarasi wakigeni awaambie mazingira huwa yanakuwaje kipindi cha mvua ili wanapotutengenezea hizi barabara basi pasijekutokea mambo kama haya?

Designed by Mfugale

Mtanzania

Anafaham mazingira vizuri

Sasa kilichopo kwenye technical drawing hatujuwi kama ndicho kilichofanywa

Ikumbukwe Ccm huwa na maamuzi yao kufurahisha ujinga Wa mapenzi wao.
 
unajua ulichokipiga picha wewe mtu? Lowasa kaondoka na ubonho wenu uliokuwa unawasaidia kufikiri vizuri
 
Dar es Salaam, first fly over... sasa hapo ile theory ya Contraction and Expansion on concrete ndipo itakapofanyakazi, very soon tutashuhudia cracks matokeo yake baada ya hapo ni mabaya sana. Jitihada za haraka zinahitajika. Nakumbuka sana adha iliyokuwepo pale Nyerere road karibia na Quality Plaza.
 
Tumeshuhudia mvua iliyonyesha leo hii jijini dsm na kusababisha baadhi ya maeneo kufurika maji na kuhatarisha usalama wa watumiaji pia na miundo mbinu husika iliyojengwa kwa pesa za mvuja jasho
Hapo pichani ni Tazara flyover tazameni hali ilivyo kwa mvua moja tu ya leo!View attachment 1036989

In God we Trust
Acha uzuzu hukuona uwanja wa wa ndege wa US ulijaa maji wakati wa mvua za mwaka jana!! Mbona hukulalamika mfyuuu!!
 
Huenda nimekuwa kilaza wa kiwango cha juu kabisa kiasi sijamwelewa mwandishi. Hivi kwa uono wa mwandishi, anamaanisha hiyo flyover ndiyo iliyosababisha maji yote hayo? Ina maanisha kama flyover isingekuwepo, maji yasingetuama?
 
Back
Top Bottom