Flash Back Memories: Matukio ya Boarding School

Dah..mie nakumbuka jinsi tulivyoishi porini huku tukila mizizi na matundapori kwa miezi mitatu mimi na rafiki zangu wawili. Tulikuwa tunatafutwa kwa kuchoma moto malori mawili ya jeshi yaliojaa wanajeshi wakiwa na silaha zao 🙂
 
Ray C ktk ubora wake, kitu NIWE NA WEWE MILELE, nipo shule ya kidini, ya boys, Mwl mlezi, full unoko, kaikamata barua yng kutoka KILAKALA GIRLS, ticha si akaja kuisoma barua yote Assembly! Ticha anaisoma huku anapandisha mdadi. Masela wanamshangilia. Ilikuwa kesi ya kufukuzwa shule, thanks nilipenya tundu la sindano!
 
Kunywa pola,kudeki utumbo,kukata gogo,outdoor nadhana maneno aya wanayajua wenyewe
 
We itakua uliku mchoyo haha mpka ukaibiwa tranka lote
 
Ha ha ha ha hatareeee
 
1.kuto nunua vifaa kama vile sabuni mafuta dawa ya mswaki, kawaidah naamka mapema kugongea vya wengine

2.kusubiri chakula cha ziada baada ya muda wa kula kupita
 

Umenikumbusha nikiwa Form 5 kulikuwa na mechi ya A-Level na O-Level basi ikatokea O-Level wamshushia kichapo jamaa wa Form 5. Usiku mikakati ya kuwachapa ikapangwa, asubuhi tumeamka tunaona Polisi wanafanya Kwata nje ya Mabweni yetu. Tukaanza dialogue kwamba hakuna fujo inatokea, baada ya muda wakaondoka. Kilichotokea baada ya Assemble 0-Level walikula bakora sana na haikujalisha ulikuwepo uwanjani jana au lah. Vurugu ilitulizwa na Polisi ambao Kituo chao kipo mita 200 tu kutoka shuleni. Katika kukimbia nikaanguka kwenye matuta wenzangu wa nyuma wakanifanya daraja huku Polisi wanakuja jamaa wananikanyaga bahati nzuri nikaona shimo pembeni nikaingia humo ndio ikawa salama yangu.
 
We jamaaa umesoma lini hyo shule mbona unaandika kwa tress namna hyo
 
Nilikua pugu ujamaa 5 PCM miaka 90,umekumbusha mbali sana mambo ya pond, kudrop na mwisho wa lami, bus letu lilikua uda la kwenda kisarawe, tulikua tunapandia msimbazi
 
Wale wa Kantalamba tukutane Chanji kwa Mbombo ngafu au kwa mama kalekwa kwenye Wanzuki na kimpumu.
Na wale wa Jamhuri High school Dodoma tukutane 84 Club
Daaa umesahau chiluba na mazwi kupiga gongo,kidedi kuvutia ganja miksa chanji kwenda kuchi pilau j pili night
 
....hahahahahaaaa
 
Dah..mie nakumbuka jinsi tulivyoishi porini huku tukila mizizi na matundapori kwa miezi mitatu mimi na rafiki zangu wawili. Tulikuwa tunatafutwa kwa kuchoma moto malori mawili ya jeshi yaliojaa wanajeshi wakiwa na silaha zao 🙂
Nyie ni makomando aisee..au unatupa scenes za komando kipensi?
 
Mh! wewe ni janga kabisa. yaaaaaaaaaa.......ni unafanya uchafuzi mkubwa hivyo kwenye masanduku ya wenzio. Wangekugundua 2 nadhani wao badala ya ku**** wangeharishia kwenye sanduku lako na kitanda.
 
form 1 mpaka form 4 nimesoma shule nne, na zote nilikuwa nahama siyo kwa kufail, bali ukorofi tuu, nakumbuka nilisoma Uchama nzega ikiwa shule yangu ya pili, kulikuwa na boga kubwa sana nyuma ya Labaratory, nafikiri lilikuwa kwa ajili ya experiment, kila siku tukawa tulapigia mikakati ya kuliiba maana lilikuwa sehemu ya wazi sana, siku ya kwanza tukaja na ndoo, lile boga likagoma kuingia kwenye ndoo, mara ya pili tukaja na begi la mgongoni (kipindi kile begi la volcano lilikuwa ndo bag kali la mgongoni) humo namo likagoma, safari iliyofata tukaenda na kisu cha jikoni tukalikata katikati then tukaenda kulichemsha usiku wa manane na ulila bweni zima.
kesho yake ikawa kesi, boga halionekani, tulichezea stick hatari
 
umenikumbusha kuna washkaji walichukua ugali uliobaki usiku wakauweka kwenye mfuko wa sembe wakauweka asubuhi yake wakapiga na uji...halafu ukiuita ugali wanakumaindi...wanataka uuite white bread
ha hahaha
 
nimecheka mpaka basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…