Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,608
- 4,265
Unaisugua kwenye paji la uso!Haha, Mkuu hilo la kufuta mhuri wa stempu kumbe lilikua kila mahali?
Unaisugua kwenye paji la uso!Haha, Mkuu hilo la kufuta mhuri wa stempu kumbe lilikua kila mahali?
Kutoboa inabidi uwe na msuli hasa, kama huna, matokeo yake ndio kama hayo. Umenikumbusha classmate wangu mmoja, yeye alikua ana solve hesabu tu, na tukipiga pepa anapata C, anafeli masomo mengine yote lakini hesabu anapata C.Kuna jamaa siku ya NECTA form 2 alitoboa akaja kulala saa 11 alfajiri, matokeo yake akaja kuamka saa 5 asubuhi baada ya kelele za tuliotoka kwenye pepa kuanza kusikika mitaa ya bwenini. hahahahaaaa
Usela mzuri saaana huuUkiskia madoja sasa mm ndio nilkua rais wao.
Doja la kimataifa kukaa assemble mara moja kwa wiki.
Kuingia darasan mpaka niskie kuna paper.
Coz shule yetu ilkua porin karbu na mpaka wa burund, bac mapind yang yote kwa por huku nikijiburudidha na ndiz pamoja na maparachich na bang kwa mbal.
Kumchapa fimbo kiongoz yoyote mnaa kwa maticha.
Alaf walichokua wanashangaa sasa matokeo yakibandikwa ubaon nmewaburuza.
Bhuahahahahaha duh mkuu umenichekesha sanaa asee tupia na jina la iyo shule1. Muda wa michezo wenzangu wakiwa viwanjani Mimi nikienda kitaa kula mzigo.
2. Kufungua store ya shule usiku wa manane na kuiba sukari na mchele. Tulikuwa na funguo nyingi sana.
3. Kuiba kuku na Sungura wa mapadri kwakuwa ilikuwa seminari. Na kuwatengeneza supu usiku wa manane.
Kunywa uji na kiporo cha makande au ugali wa jana kwa kuwa huna hela za kununulia mandazi au vitumbua..au siku nyingine kupiga uji dry...
Siku ya wali maharage au nyama na ugali watu wote kwenye group lako la kula hawakosekani hata mmoja...
Kubeba kiti na meza na kwenda kusomea chimbo la porini hukoo
Kujificha darini siku ya ukaguzi wa usafi
Halafu kesho anakuchapa viboko, eti alikukuta unakunywa pombe!!!!!!!!!!!!!!!!!Tulikuwa tunatoroka kwenda vijiji vya jirani kwenda kunywa pombe za kienyeji, tukikutana na mwalimu tunamnunulia pombe mpaka atosheke
Hii itakua old moshiNachokumbuka cha kusikitisha nilifiwa na mwanangu mimi nalala kitanda cha juu yeye chini kwenye Deka aliugua tumbo tu kama masihara akaenda nyumbani karudi shule kapona kumbe ndio anaondoka hivyo ,R.I.P Brother Mungu akipenda tutaonana tena.
Msosi kujazwa mafuta taa
Mengine ni ya kawaida kama kuwafulia mabraza wa form Six na Five ....kupewa sh 50 ukanunue mkate mzima,soda ,na change ibaki mkate wakati huo ulikua 400
Na Disco zetu za mchana na watoto wa Machame Girls ,Kibosho Girls,St Marygoreth,Weruweru nk
P.O.Box inaitwa sijui Lee Pax ,Barua za watoto wa Machame,Marygoreth nk basi kidume ukiitwa assemble kupewa barua yako kichwa kinakua kikubwa (Ujiko) ndani ya barua yenyewe hamna kitu ni kiss before you open ...na makopa kopa tu .....
Ulitokea ugomvi jamaa mmoja wa Six alikula mke ya mwanakijiji akakamatwa akachezea kichapo kesho yake jioni Mungu ndio anajua ,jamaa walitugawa kwenye platoons kikosi kikasonga mbele kwenda kijijini ,wanakijiji walichezea kichapo siku tatu mfululizo ,Jamaa wa CCP wakashindwa tuliza mtiti siku ya nne defender kama 30 hivi zikazingira shule ndio msala ukazimwa
Bhuahahahahaha dah nimecheka sanaaa asee uliamua kujificha kwenye tranka wew ni bonge la mjeda aseeIlikua kwenye Shule moja huko Moshi
Siku nimechelewa kuamka,kengele ya parade ikalia na mm sikuweza kufika kwa wakati na ukifika kwa kuchelewa ni fimbo za kutosha.
Sasa mimi nikaona njia itakayoniokoa ni kubaki bwenini tu. Sasa pa kujificha ni wapi? Basi,nikajitwika na kutaka kuingia darini! Nilianguka karibia nitenguke kiuno.
Kunyanyuka nikamuona mwalimu wa bweni anakuja. Huyu akikukamata ni hatari sana. Sasa shuleni huruhusiwi kufunga tranka,yote yanaachwa wazi! Nikafikiria fasta,nikachukua tranka moja kubwa na kumwaga vitu Kitandani.
Kisha mwanaume nikajitwika ndani. Nilikua mdogo na nilitoshea. Tatizo hewa sasa,haikua ikitosha. Ticha akafika akaanza kukagua kuanzia uvunguni mpaka darini.
Alipomaliza,akakaa kitandani akaanza kufuta viatu vyake. Kumbe anakanyagia tranka ambalo nipo humo. Alikaa muda mrefu kidogo huku mwenyewe hewa imekua nzito mno na nahema kwa shida. Nikaona hapa Malaika mtoa roho ananichungulia. Nilichofanya nikamuinua mguu na kutoka,aisee alitoka kutoka mbio lakini aliponiona alicheka sana.
Akanipeleka staff,walimu wote walicheka sana mpaka wakashindwa kunichapa. Hahahaha!
KUTUMWA KUPELEKA BARUA KWA DEMU WA Braza.
Kama kawaida,kuwa na mahusiano ya kitoto shuleni. Braza akamuandikia demu barua lakini wanasoma madarasa tofauti. Lile jamaa likaniita likanambia peleka hii barua kwa demu wake. Mimi nikaichukua na kuanza kuipeleka. Ilikua ni usiku muda tunatoka prep. Kumfikishia demu nikamkabidhi alafu nikaanza kumpa maelekezo. Ticha wa zamu huyo katokea. Alinilabua kofi moja hilo sijapata kuliona dunia hii.
KUINGIZWA STAFF NA KUCHAPWA KAMA MBUZI.
Shule yetu ilikua ya Kanisa,kuna kipindi wale wenye mahusiano mnaitwa. Taarifa za uhusiano wenu wanazipata kutoka kwa MaSPY!
Basi,siku hiyo unaitwa na kuambiwa una mahusiano na fulani kisha uwataje wengine ambao unawafahamu wana uhusiano.
Mkishawataja,mnaambiwa kumbatianeni. Kila mtu na mpenzi wake. Walimu wanakaa kila upande,mnachapwa balaa. Mwalimu anakuchapa popote isipokua kichwani. Acha kabisa aisee.
N hatari Mkuu wangu,tcha anachapa viboko kama anakukata makalio. Alafu kulivyo baridi acha tu Mkuu wangu! Nilijitahidi sana,sema tcha aliendelea kukaa tu babake!Bhuahahahahaha dah nimecheka sanaaa asee uliamua kujificha kwenye tranka wew ni bonge la mjeda asee