Flash Back Memories: Matukio ya Boarding School

Flash Back Memories: Matukio ya Boarding School

Wako wapi members wa Mkwawa high school
The complex Cassino. 1990's -2000's

Wanafunzi kutorokea makanyagio kununua maandazi kwa jina la uficho zilikuwa zinaitwa nyama au banzi.

Batch ya 1999-2001 kuna jamaa alikuwa mkorofi sana ali act kama agent wa hizo nyama anachukua huko makanyagio anazileta shule. .alijulikana kama mzee wa nyama.
 
Kulala abroad( nje ya shule na kurudi asubh.) Unalala kwa mmama au mwanafunz wa kike mtaan.2 kufungiwaa na mwanamke kwa nje na wafumaniaj! Kukosa vtafunwaa vya chai# kupuliza;
 
Kweli boarding raha nakumbuka kuna mwl wa commerce wa kike alikuwa anachapa mboko na hakuna mwanafunzi alimtaka sasa bahati akafikwa na umauti bwn! Sasa kipindi anakata roho hosp hatukuwa na habari.Sasa Staff member (walimu)wakaja kututangazia kile kifo kwa majonzi makubwa eebwanae shule yote frm 1 to iv wote tuliruka juu na kushangilia kwa Furaha ila mboko tulikuwa za ukweli ila hakika hatukufanya vizuri but hasira tu
 
Hahaaaaa huu uzi umenikumbusha mbali sana nakumbuka kulikua na ticha mmoja alikua bingwa wa kukariri yani hata akiona kisogo tu anajua we ni nani sa siku moja tulikua tunajipikilisha wali kwenye mashimo yaliyotokana na adhabu tulizokua tunapewa za kufyatua matofali, sasa tukasikia sauti ya viatu inakuja upande wetu kucheck hv ni huyo ticha tulichokifanya ni kukimbia huku sketi tumezinyanyua juu kuficha kisogo mwalimu asitujue huku tukiacha sehemu za makalio wazi afu ticha mwenyewe ni wakiume daaah
Hii shule itakuwa Arusha nn mkuu
 
Haha huu uzi unachekesha hatarii, ngoja tu share kidogo
1. Nakumbuka tulivo toroka siku ya jumapili kwenda kwny sherehe kijijini mara gafla kumbe mwalimu alikuwa mwalikwa na alituona bila sisi kumuona akarudi shule chap kaitisha Rocoo (ikumbukwe huyu ticha ana pikipiki) na kuna umbali wa kutosha kutoka kwenye sherehe mpaka shule. Kama kawaida tukamaliza tukio na msosi mwingine tukaweka kwenye mifuko meusi tukaweka kweny mabegi kila na mtu na mzigo wake wa kutosha apo wa kula siku2 au 3,
kimbembe kikufika shule tuuu tulitumia chimbo letu kuingia Kama kawaida cha ajabu kila mtu anakushangaa tukajua kimenuka wee baada ya dk kadhaa kengelee ikagongwa sitakaa nisahau kilicho endelea baada ya hapo
2. Kuibiwa chupi zote na kubaki na moja tuu nashkuru mungu ilikuwa imebaki week kadhaa kufunga shule
3. Nguo zangu kuchanganywa na maharage
A level hakukua na mengi kama O level ila moja la kushangaza nlilolikuta humu ni kutongozwa na demu mwenzako na alafu couple nliona za kutosha uku (hii ilikuwa single sex)
Duu mungu ni mwema nlitoboa lakini boarding duuu lazima ukomae na ujitie ukichaa ku survive
 
Dah umenikumbusha pugu secondary wazee wa pondi mixer beto dah nimepamiss sana
 
Daaaaa Mimi nilikuwa WANTED......

Yaan kama ingekuwa nchi kama marekani ningekuwa the most notorious Killer in the country

Kiss cha kuwa wanted nikikisimulia wrote mtalia machozi...., ngoja niishie hapa
 
Nachokumbuka cha kusikitisha nilifiwa na mwanangu mimi nalala kitanda cha juu yeye chini kwenye Deka aliugua tumbo tu kama masihara akaenda nyumbani karudi shule kapona kumbe ndio anaondoka hivyo ,R.I.P Brother Mungu akipenda tutaonana tena.

Msosi kujazwa mafuta taa

Mengine ni ya kawaida kama kuwafulia mabraza wa form Six na Five ....kupewa sh 50 ukanunue mkate mzima,soda ,na change ibaki mkate wakati huo ulikua 400

Na Disco zetu za mchana na watoto wa Machame Girls ,Kibosho Girls,St Marygoreth,Weruweru nk

P.O.Box inaitwa sijui Lee Pax ,Barua za watoto wa Machame,Marygoreth nk basi kidume ukiitwa assemble kupewa barua yako kichwa kinakua kikubwa (Ujiko) ndani ya barua yenyewe hamna kitu ni kiss before you open ...na makopa kopa tu .....
Ulitokea ugomvi jamaa mmoja wa Six alikula mke ya mwanakijiji akakamatwa akachezea kichapo kesho yake jioni Mungu ndio anajua ,jamaa walitugawa kwenye platoons kikosi kikasonga mbele kwenda kijijini ,wanakijiji walichezea kichapo siku tatu mfululizo ,Jamaa wa CCP wakashindwa tuliza mtiti siku ya nne defender kama 30 hivi zikazingira shule ndio msala ukazimwa
Lyamungo ama umbwe nini?
 
Nakumbuka jamaa mmoja shabiki wa damu wa ASENALI, dah alikua jamaa angu sana, siku hiyo timu yake ilifungwa 8 na man u, alilia machozi kabisa akimlaumu wenger, dah nikimkumbushaga mpaka leo anacheka tu mwenyewe
 
Hahahhaha,umekumbusha tulivyokuwa tunafoji stemp,jamani tunafuta mhuri halafu tunatumia hiyo stemp kutuma barua,pia shida ya maji ndo ilisababisha watu tupige passport size,yaani nilishaapa kamwe wanangu hawawezi kusoma boarding schools
Hahahaha stemp inafutwa muhuri mpk inaonekana mpya na bahasha za kuchonga kwa kutumia karatasi
 
Back
Top Bottom