Ilikua kwenye Shule moja huko Moshi
Siku nimechelewa kuamka,kengele ya parade ikalia na mm sikuweza kufika kwa wakati na ukifika kwa kuchelewa ni fimbo za kutosha.
Sasa mimi nikaona njia itakayoniokoa ni kubaki bwenini tu. Sasa pa kujificha ni wapi? Basi,nikajitwika na kutaka kuingia darini! Nilianguka karibia nitenguke kiuno.
Kunyanyuka nikamuona mwalimu wa bweni anakuja. Huyu akikukamata ni hatari sana. Sasa shuleni huruhusiwi kufunga tranka,yote yanaachwa wazi! Nikafikiria fasta,nikachukua tranka moja kubwa na kumwaga vitu Kitandani.
Kisha mwanaume nikajitwika ndani. Nilikua mdogo na nilitoshea. Tatizo hewa sasa,haikua ikitosha. Ticha akafika akaanza kukagua kuanzia uvunguni mpaka darini.
Alipomaliza,akakaa kitandani akaanza kufuta viatu vyake. Kumbe anakanyagia tranka ambalo nipo humo. Alikaa muda mrefu kidogo huku mwenyewe hewa imekua nzito mno na nahema kwa shida. Nikaona hapa Malaika mtoa roho ananichungulia. Nilichofanya nikamuinua mguu na kutoka,aisee alitoka kutoka mbio lakini aliponiona alicheka sana.
Akanipeleka staff,walimu wote walicheka sana mpaka wakashindwa kunichapa. Hahahaha!
KUTUMWA KUPELEKA BARUA KWA DEMU WA Braza.
Kama kawaida,kuwa na mahusiano ya kitoto shuleni. Braza akamuandikia demu barua lakini wanasoma madarasa tofauti. Lile jamaa likaniita likanambia peleka hii barua kwa demu wake. Mimi nikaichukua na kuanza kuipeleka. Ilikua ni usiku muda tunatoka prep. Kumfikishia demu nikamkabidhi alafu nikaanza kumpa maelekezo. Ticha wa zamu huyo katokea. Alinilabua kofi moja hilo sijapata kuliona dunia hii.
KUINGIZWA STAFF NA KUCHAPWA KAMA MBUZI.
Shule yetu ilikua ya Kanisa,kuna kipindi wale wenye mahusiano mnaitwa. Taarifa za uhusiano wenu wanazipata kutoka kwa MaSPY!
Basi,siku hiyo unaitwa na kuambiwa una mahusiano na fulani kisha uwataje wengine ambao unawafahamu wana uhusiano.
Mkishawataja,mnaambiwa kumbatianeni. Kila mtu na mpenzi wake. Walimu wanakaa kila upande,mnachapwa balaa. Mwalimu anakuchapa popote isipokua kichwani. Acha kabisa aisee.