Ndugu wasomaji, ninawashauri kuwa jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Pengine utaniuliza, wewe umesimama wapi? Nataka nikuambie mimi sisimami popote(kwa maana ya kuwa mimi nasimama katikati). Kati yangu mimi na wewe hakuna anyejua chochote na kama unajua huwezi kujua kwa undani na kwa usahihi vizuri. Katikati ya wimbi zito la sintojua, humo ndani zikiwepo siasa interest, ushindani interest, roho mbaya interest, chuki interest, maslahi interest, ukabila interest, ufisadi interest na bila kusahau kuzidiana kete na kuzidiana akili interest nk ni vigumu kuweza kuupata ukweli tunaoutaka.
Ni sawa tunavyofanya kwa kila mtu kutoa mawazo yake kwa jinsi anavyoona, lakini nakushauri usipende kuchuma dhambi bila sababu ya msingi. Toa wazo lako lakini ogopa kuhukumu. Jambo unalomfanyia mwenzio siku moja utavuna hilohilo. Na si hivyo tu, unapohukumu ujue umemtangulia Mungu ajuaye vitu vyote. Katika utoaji wa wazo lako NAKUSHAURI ACHA NAFASI YA KUTO KUJUA, ILI YULE ANAYEJUA ZAIDI YAKO ATAKAPOJIELEZA AWEZE KUPATA NAFASI KWENYE MOYO WAKO BILA KUKUAIBISHA