Finally: Hongereni Wana-CCM Online!!

Finally: Hongereni Wana-CCM Online!!

Status
Not open for further replies.
dah...hata huyu anajíita father of all.naye ni walewale?.
Kama ndo hivyo kumbe hali ni ngumu.si waende vijijini wakalime.posho yenyewe inawatosha kweli kwa maisha ya bongo.kha...!!

Mkuu Ritz
Huyo father of all kama sio Matola ni Molemo haiwezekani hata siku moja tusimuone mmoja wao ndani ya hii thread wameingia kwa ID zingine wanajua moto wa william mzito wameamua kujificha

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Mjadala unaenda kwa hoja pro cdm na pro ccm bt kuna watu wanaelekea kuharibu huku mwishoni
 
Hongera zako weye mwenye maana...yote niliyoyaandika yameshawekwa hapa jamvini sasa sijui cha ajabu ni kipi. Weye naye ni magamba mwingine kwa hiyo huna jipya zaidi ya kutetea uozo wa DHAIFU na Serikali yake DHAIFU.

cha ajabu ni kuingiza personal beef yako wewe na Le mutuz.HAKUNA MANTINKI ,sioni sababu ya wewe kuingilia maisha yake binafsi after all the man isnt even running for presidential ellection.
Which led me to conclude that you dont have a point here.you are just trying to use this to attack Le mutuz personaly.
 
Ukitaka kuchafua hali ya hewa hapa jukwaani,sema ukweli kwamba cdm kwa sasa si lolote wa chochote,inayumba.
 
Mkuu Ritz
Huyo father of all kama sio Matola ni Molemo haiwezekani hata siku moja tusimuone mmoja wao ndani ya hii thread wameingia kwa ID zingine wanajua moto wa william mzito wameamua kujificha

Chama
Gongo la mboto DSM

Huyu jamaa ni bingwa wa Multiple ID's kuna siku alijichanganya nilicheka.
 
Last edited by a moderator:
- ha! ha! ha! ha! I know ila baba yangu sio mwizi na hajawahi kufukuzwa kazi na Serikali ya Tanzania tena kwa aibu!! so wewe furahia ufisadi wa baba na kuwaona wabongo wajinga huku unakula hela zao alizofisadi baba yako! ha! ha! ha!

- Njaa haikunikuta majuu kama wewe na bado haijanikuta bongo kama wewe! ha! ha! ha! baba yangu hana viwanda vya hela za ufisadi bro! ha! ha! ha!

Le Mutuz!!

hivi yule mgombea urais wa ccm aliyetaka kusilimishwa na waarabu then agombee urais ni nani vile ilikuwa mwaka 1995 mpaka kupelekea nyerere kutoa kitabu cha tanzania na hatma ya viongozi wetu.le mutuz alikuwa na umri gan?
 
Nimekuwa mwanachama wa JF kwa miaka sita sasa na kabla ya hapo nilikuwa mwanachama wa Jamboforums; Na kote huku kuwili, wakati wa kujiunga, sikuwahi kukutana na kipengele kinachouliza MISSION YAKO KAMA MWANACHAMA NI NINI; Vinginevyo kwa uelewa wangu, huu ni uwanja wa kubadilishana mawazo na kupimana kwa hoja, kwa kujenga na kwa maslahi ya taifa letu, na ni hivyo ndivyo nimekuwa nafanya kwa miaka sita;



Kwa kauli hii, basi kumbe mission yako ni kuja kupambana na hoja za Chadema; Sasa nimekusoma; Naomba ujue kwamba mimi sio mwenzako katika hilo, badala yake nipo humu kubadilishana mawazo na wana chadema, wana ccm, wana CUF, NCCR n.k kwa manufaa ya taifa, na ikitokea tunapishana, mgongano wa mawazo ni suala la kawaida towards that end;


Kwa hili naishiwa hata nguvu ya kukujibu kwani hata mwenyekiti taifa amelizungumzia hili i.e. makundi; kama hauoni factions ndani ya CCM ya sasa na haukubaliani na mimi katika hili, basi mimi na wewe tunaishi dunia mbili tofauti kabisa; Vinginevyo unaweza kuwa sahihi na mtazamo wako, lakini nitaendelea kupingana na mtazamo huo;


Yani hiki ndio kipimo chako rasmi on whether CCM imemeguka au haijameguka? No wonder tunapishana mtazamo;


Ingekuwa sio ya CCM isingeisaidia CCM;


Tuwe tuna chambua na matokeo, itatusaidia sana; Tumeshinda kata nyingi, pengine four times ya idadi ya kata walizoshinda Chadema lakini jumla ya idadi ya kura picha ni tofauti kabisa; hii inatuambia nini? Kura zetu CCM nyingi ni vijijini, Chadema ni Mijini; Na mwelekeo wa dunia ni urbanization ambapo ifikapo 2025, over 50% ya wakazi wa Africa, Tanzania ikiwemo watakuwa in urban areas; Are we investing for the future? Kwanini tunapoteza mvuto mijini? hazina yetu vijijini ni suala la muda tu;


Ninachozungumzia mimi ni FACTIONS within the party ambazo mara kwa mara kumekuwa na jitihada za kuzikutanisha kama njia ya kuokoa chama kisipasuke; Factions sio jambo jema kwa uhai wa chama, whether kuna chama kimoja au vyama mia moja ndani ya demokrasia husika;



One British Conservative - Enoch Powell (1912) alipata nena kwamba: A Party... is not a faction or club of individuals who associate for mutual assistance in acquiring and retaining office; It is a body of persons who hold, advocate and desire to bring into effect certain political principles and policies".

Huyo Mao, na pia mifano yako juu ya Democrats na Republicans wanaongelea on the later, sio the former; Sisi tupo kwenye the former na ndio hoja yangu ya msingi katika hili;



Sijafanya any scientific research zaidi ya kuwa observant wa maendeleo mbalimbali hasa huku site; wewe je, kuna research umefanya?


Ni vizuri kwamba umeweka a conditionality on this one i.e. kama itaweza..., na hii ni tofauti na hoja yako ya msingi kwenye bandiko namba moja; vinginevyo ushindi wetu sio straight forward tena kama zamani, na ndio maana Mwenyekiti ameona kuna utofauti kati ya Mukama na Kinana au Makamba na Kinana;


Hii kauli kidogo inatoka so authoritative, kana kwamba ushindi wa CCM sio lazima upitie sanduku la kura;


Chadema ina kansa na sio CCM? Tukiendelea kulikataa hili, tutakuja aibika vibaya sana siku ya siku; Chadema is experiencing growth and increase in popularity kwa sababu ya madhaifu yetu CCM, na hata mwenyekiti kalisemea hilo; Wewe unaita hiyo ni Kansa?


Kipimo cha Uimara ni nini? Sisi mgombea wetu ni yupi imara wa kuweza kukabiliana na nguvu ya Chadema ambayo sio ya dola bali ya UMMA? Tunamjua mgombea huyo? Tunamuandaa au tutampiga majungu hata kama ndiye angekuwa chaguo sahihi? I hope tutaachia nguvu za soko zitupatie mgombea imara kutoka CCM;


Mwenyewe unaanza kukubaliana na mimi kuhusu makundi ndani ya CCM ambayo hayana tija ingawa hapo awali ulileta hoja za Mao na Vyama vya marekani kwamba hivi ni vitu vya kawaida;


Hizi ndio kauli zenu CCM hata ngazi za juu, na mnajisahau kwamba milioni tano ilianza na moja; mtaendelea kupoteza watu wengi kwa kutokuwa tayari kusoma alama za nyakati; Vinginevyo hauna mamlaka ya kuniambia niende wapi kutumia haki yangu ya kikatiba katika masuala ya siasa; Lakini kama una mkono huko sijui wapi wa kuniondoa uanachama, na iwe hivyo; Mpaka muda huo ufike, rudi kwenye mwongozo wetu wa CCM (1982) ambao unasema hivi:

Ibara ya ( 5) Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi

58. Kuna mambo mawili tuliyojifunza ambayo ni muhimu pia kuyazingatia. La kwanza linahusu suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana kama njia ya kukijenga na kukiimarisha Chama na wanachama. Ni kweli kuwa katika TUJISAHIHISHE Mwalimu anasisitiza jambo hili na kwamba Katiba ya CCM inatamka waziwazi juu ya umuhimu wake. Lakini ni kweli pia kuwa hatujaijenga tabia hii ipasavyo. Mara nyingi tumependelea kuteteana, kufichiana makosa na hata kutafuta visingizio visivyo na msingi. Neno kuleana, kwetu sisi (ingawa kuna malezi mema na mabaya) limechukua nafasi ya kukosoana. Wanachama wenye upungufu husaidiwa kama wanakosolewa ili wajirekebishe...

59. Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana lina sura kadhaa. Kwanza linataka wanachama na viongozi kuwa tayari kusema kweli katika vitendo vyao na kukubali kuambizana ukweli. Pili, linataka wanachama na hasa viongozi wawe tayari kukosolewa bila kuhamaki na inapobidi kukubali kujirekebisha. Tatu ni kuwa Chama chenyewe katika vikao vyake vya ngazi mbalimbali kuwa na utaratibu wa kujikosoa.


Matumaini yangu ni TUTADUMU unconditionally i.e. hata tukiwa chama cha upinzani bila ya kuwa na dola mikononi; in fact, kwa mtazamo wangu, tukianguka 2015 ndio tutajua ukweli kina nani wanakipenda chama kwa dhati na nani walikuwa wanatafuta tu maisha ya mkato mkato; Kaka, Je, ikitokea tumeanguka 2015 utaendelea kuwa mwanachama wa CCM? I hope jibu lako halitajirudia tena kwamba 'infact ninasema hivi Wapinzani hawatashinda 2015';
Mchambuzi ni mbwa mwitu ndani ya SuRa Ya KoNdOo uchambuzi wake japo huwa na chembe ya ukweli lakini mara zote umejaa hila (UzAnDiKi). Kwa msemo wa JK huyu ni nyoka mwenye ndimi mbili. Anaposema hana mission nayo ni hila kwani kwa tunaosoma post zake tunafahamu kuwa katumwa japo wanaoshambuliwa ni akina ritz lakini huyu naye sidhani kama yupo upande wao bali upande wa pili. YETU MACHO MTASEMA YOOOOOOOOOOOOOTE.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Rejao
Kumlaumu william ni kumuonea personal attacks zimeanzishwa na makamanda wao hawana hoja zaidi ya kupiga kelele wakiishiwa na hoja wanaanza matusi na kebehi anachokifanya william ni kujibu mapigo siasa za JF ni kujibu mapigo kwa nguvu zote

Chama
Gongo la mboto DSM

chama,
Nakubaliana na wewe mkuu, but inabidi tuwe makini sana wakati wa kujibu kuchagua cha kuandika na cha kutoandika. Tuendelee kuwasambaratisha hawa wapinzani uchwara but tujue mipaka yetu!!

Naona leo mmewakimbiza kabisa. Big up mkuu.
 
Last edited by a moderator:
That is your opinion, but I beg to differ with your opinion. Maisha yake hayana siri na sioni cha ajabu yoyote kumwambia mtu aache utoto na kubadilika ili aanze kusimamia responsibilities zake kama Baba na pia mume badala ya kufanya vitu vya ajabu ajabu. Huo ni ushauri ambao ningempa hata ndugu yangu wa kutoka nitoke. Akitaka anaweza kuufuata au la na kuendelea na utoto wake.

cha ajabu ni kuingiza personal beef yako wewe na Le mutuz.HAKUNA MANTINKI ,sioni sababu ya wewe kuingilia maisha yake binafsi after all the man isnt even running for presidential ellection.
Which led me to conclude that you dont have a point here.you are just trying to use this to attack Le mutuz personaly.
 
That is your opinion, but I beg to differ with your opinion. Maisha yake hayana siri na sioni cha ajabu yoyote kumwambia mtu aache utoto na kubadilika ili aanze kusimamia responsibilities zake kama Baba na pia mume badala ya kufanya vitu vya ajabu ajabu. Huo ni ushauri ambao ningempa hata ndugu yangu wa kutoka nitoke. Akitaka anaweza kuufuata au la na kuendelea na utoto wake.

Mkuu BAK
Tueleze yako tuone nani anaishi kwa mgongo wa baba!!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chama, ni aibu kwa kiongozi ambaye wafuasi wake wanataka tumpe nchi kuburuzwa mahakamani kwa kosa la kutelekeza watoto wake wakuwazaa mwenyewe pamoja na mama yao...mama wa hao watoto anaitaka mahakama tukufu wambane Dr Slaa alipe fidia ya milioni 150 kama fidia.

Halafu anata mahakama wambane mwanamke wa sasa wa Dr Slaa amlipe milioni 500 kwa kumuibia mwanaume wake.

Haya yote makamanda wanayona ni mambo ya kawaida sababu yanafanywa na Dr Slaa.

dah...jamaa anaanza mascandal kabla hata hajanusa statehouse...hatari kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Comrade.....

Ukweli ni kwamba siasa za Tanzania sasa hivi zimeingiliwa na hazina maana yoyote......Vyama (ikiwa ni pamoja na chama tawala, CDM na vingine) vimekuwa vikundi vya mipasho, havina tofauti na enzi zile za TOT Taarab (Khadija Kopa) na Muungano Cultural Troupe(Bi Nasma Khamis Kidogo - RIP)......Siku hizi vyama badala ya kueleza nini watawafanyia watanzania, vyenyewe ni kutupiana maneno ya kejeli, kutukanana na kila aina ya upuuzi.....Ni ajabu kuona CCM badala ya kueleza ni wamewafanyia watanzania katika miaka 50 ya Uhuru (ambavyo vipo na vinaonekana) wao wanakaa na kuisakama CHADEMA na viongozi wake......

Inashangaza pia kuona CHADEMA kama chama mbadala katika siasa za Tanzania badala ya kuutumia muda huu wa kuelekea mwaka 2015 badala ya kuwaeleza watanzania nini watawafanyia mara watakapochaguliwa wao nao kila uchao wamekuwa wakiisakama CCM na viongozi wao kila uchao.....Imekuwa ni mipasho tu kila kukicha.....

Ni ajabu kuona viongozi wa vyama vya kisiasa (hasa wa CCM na CHADEMA) wakitumia muda mwingi kukashifiana na kukashifu vyama vyao badala ya kuwaeleza wananchi sera na nini wamewafanyia/watawafanyia wananchi hao wa taifa hili maskini.....Hu si wakati wa viongozi wa CHADEMA kutumia muda mwingi kuelezea udhaifu wa sekretarieti mpya ya CCM, huu ni muda wa wao kujipanga na kwenda kwa wananchi na kuwaeleza nini watawafanyia mara watakapowachagua(kumwaga sera), huu ni wakati wa kwenda kuwatongoza wananchi, huu ni wakati wa kuwashawishi wananchi kujenga imani na chama hicho, kuisakama sekretarieti ya CCM na agenda isiyochuja ya ufisadi hakutakisaidia CHADEMA kuingia madarakani, CCM imekuwa dhaifu tangu mwaka 2005 baada ya mgawanyiko uliotokana na mtandao lakini bado imeendelea kushinda uchaguzi( wa Urais, wabunge na madiwani) na kuendelea kushika dola... Agenda ya ufisadi imeanza kuzungumzwa majukwaani tangu mwaka 2006 pamoja na kuwaingia watanzania bado haijawasaidia CHADEMA kisiasa......CHADEMA wanapaswa kuutumia muda huu(ambao kimsingi ilitakiwa ianze tangu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010) kujiimarisha kisiasa na kujenga imani kwa watanzania kwa kuwaeleza nini watawafanyia pamoja na kujenga mtandano ulio imara kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa badala ya kutegemea ofisi na viongozi wa kujitolea kama ilivyo sasa......CHADEMA wanapaswa kutafuta ofisi na viongozi katika kila eneo la nchi hii (bara na visiwani) kuanzia katika ngazi ya Tawi mpaka mikoani na si kutegemea Operesheni Sangara, M4C n.k.....Kwa kufanya hivyo watakuwa karibu zaidi na wananchi......Kutumia muda mwingi kuelezea ufisadi wa viongozi wa CCM na serikali na kuiponda sekretarieti mpya ya CCM hakutakisaidia CHADEMA....Kama sekretarieti hiyo ni dhaifu ni bora CHADEMA wakatumia mbinu za kisiasa kuutumia udhaifu huo kujinufaisha kisiasa, kuisakama na kuiponda majukwaani ni dalili za KUIOGOPA..

Kwa chama changu CCM, kwa kweli sitofautiani na ndugu yangu Comrade Mchambuzi .....Niko naye ukurasa mmoja kabisa, chama chetu kina matatizo mengi sana kiasi kwamba kwa walio karibu na siasa za ndani za CCM wanaweza kudhani kuna vyama zaidi ya vinne ndani ya CCM, kinachosababisha hali hii si kingine, ni makundi ya waroho wa madaraka (wanaoutaka urais) , rushwa pamoja na kulindana ndani ya chama... Makundi ndani ya chama ndiyo imekuwa kansa inayokitafuna chama kuanzia mwaka 2005 na kadri siku zinavyokwenda kansa hii imezidi kuwa sugu na sasa makundi zaidi yanaundwa kwa ajili ya kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hii ni hatari sana, haya tunayoyasikia ya Membe na Bashe ni manynyu tu, mvua kamili itaanza kuonekana/kunyesha mwaka 2014....Makundi haya yasipodhibitiwa(japo ni too late) yatakifanya chama kiwe na hali mbaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015...Hali hii ya makundi ipo hata katika ngazi ya Ubunge na Udiwani......

Kuhusu Rushwa ndani ya chama kwa sasa; ni miujiza pekee ndiyo inayoweza kutenganisha rushwa na uongozi ndani ya chama chetu hiki....Rushwa nayo imekuwa kansa ambayo tiba yake ni ngumu kupatikana......Sijajua ni mbinu zipi hasa mzee wangu mpiganaji na muadilifu Philip Mangula atazitumia katika kupambana na rushwa na wala rushwa ndani ya chama maana karibu asilimia 90 ya viongozi wa chama na wawakilishi(wabunge,wjumbe wa baraza la wawakilishi,madiwani,masheha n.k) wameingia madarakani kwa rushwa.....Nasubiria hiyo miujiza ya kuwaondoa waliopata uongozi kwa rushwa ndani ya miezi 6......Ila kiukweli nina imani sana na sekretarieti mpya ya CCM na nimefurahishwa na utaratibu unaotumiwa na Katibu Mkuu wa CCM Kanali(mstaafu) Abdulrahman Kinana kuzunguka na viongozi wa serikali katika mikutano yake na kuwabana mbele ya wananchi.....Hii inadhihirisha kwamba sekretarieti hiyo imekuja kikazi zaidi na si porojo.....

Ni matumaini yangu kwamba mzee Mangula kama Kiongozi wa maadili ndani ya chama atasaidia katika kuondoa tatizo la kulindana na kuwashughulikia viongozi na wanachama wasio waadilifu ndani ya CCM, na kwa kuanzia waanze na makatibu wa CCM wa wilaya na mikoa na baadae kwa wale wote wenye uroho wa madaraka ambao wanatumia muda mwingi kukidhoofisha chama kwa kuendekeza makundi ndani ya chama na kuzua mpasuko ambao unakigharimu chama na utazidi kukigharimu siku za usoni.......

Siasa si uadui.......Japo ni mchezo mchafu

Tutabanana humuhumu ndani ya CCM.....

Bala.
Well said mkuu.
Pamoja
 
Last edited by a moderator:
Kwa wale wanaonifahamu hapa jamvini wanajua mimi nafanya nini. Sioni sababu yoyote ya kujieleza kwako wewe mtetezi wa uozo wa DHAIFU na magamba. Hunijui wala sina mpango wa kutaka unifahamu hunipunguzii wala kuniongezea chochote kile.

Mkuu BAK
Tueleze yako tuone nani anaishi kwa mgongo wa baba!!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
WJM,
Nakupongeza na kukuhimiza uendelee na njia hii ya kuilinda na kuihami CCM kwa akili na nguvu zako zote. Njia hii itakulipa mapema zaidi. Hivi ndivyo anavyofanya Mwigulu BUNGENI na ndivyo pia anavyofanya Wassira MAJUKWAANI. Sote tumeshuhudia idadi ya kura walizopata mkutano mkuu wa CCM uliopita. Usikatishwe tamaa wala kuyumbishwa na matusi na kejeli za humu JF. Akina Kinana na Nape wanaona jitihada zako hizi mpya. Kura zako hazikutosha kwa kuwa wengi ndani ya CCM walikuwa hawajagundua "UZALENDO" wako ndani ya CCM na sio NCHI. Kwako ni CCM kwanza NCHI baadae!
 
That is your opinion, but I beg to differ with your opinion. Maisha yake hayana siri na sioni cha ajabu yoyote kumwambia mtu aache utoto na kubadilika ili aanze kusimamia responsibilities zake kama Baba na pia mume badala ya kufanya vitu vya ajabu ajabu. Huo ni ushauri ambao ningempa hata ndugu yangu wa kutoka nitoke. Akitaka anaweza kuufuata au la na kuendelea na utoto wake.

utoto gani bana?kupiga picha na hao wadada ndo utoto.
Au kufunguka humu jf kama anavyofanya..cooomon man everyone has got his/her style ,you cant force him to do what you want in his life.IT IS HIS CHOICE.
Na yeye sio wa kwanza hapa duniani kuachana na mkewe,so huwezi kucapitalise hiyo issue na kuitumia kudiscredit
 
me nawapa pongezi moja tu, kwa kuanza kuzinduka kukijenga chama upya maana walijisahau sasa sijui kama watafanikiwa ama vipi, mungu akipenda wanaweza kusimama vizur CCM kwa sababu CCM si chama kibaya ila kuna watu wabaya na hao watu wabaya ndo wanafanya CCM hionekane mbaya na hao watu wabaya wameshindwa kuwatoa sasa ubaya unazidi, na wabaya wanazidi jaman KUFUGA MARADHI NI VIBAYA SANA MAANA YAKISHAKUWA MAKUBWA YANAKUGHARIMU ZAIDI.
 
Inawezekana wewe unaona hivyo, lakini kwa mtu mwenye umri kama wake mambo anayoyafanya ya kwenda kupiga picha na warembo ambao wanaweza kuwa binti zake na kuziweka online kwa wengi hayaingii akilini. Kumdhalilisha mkewe kwenye mitandao pia si jambo la kistaarabu na ukweli ni lazima usemwe.

utoto gani bana?kupiga picha na hao wadada ndo utoto.
Au kufunguka humu jf kama anavyofanya..cooomon man everyone has got his/her style ,you cant force him to do what you want in his life.IT IS HIS CHOICE.
Na yeye sio wa kwanza hapa duniani kuachana na mkewe,so huwezi kucapitalise hiyo issue na kuitumia kudiscredit
 
Ivi we una akili?au zote zimehamia tumboni?kwanini kila mtu unamuhusisha na Dr.Slaa?huwezi kumaliza thread bila kumtaja Dr?
- uhuni ni kuiba mek wa mwananchi unayemdanganya untaka kumuongoza! ha! ha1 ha!, tena kwa mtu mwenye PhD ya kanisani! ha! ha! ha! huo ndio uhuni!!

Le Mutuz!!
 
Kwa wale wanaonifahamu hapa jamvini wanajua mimi nafanya nini. Sioni sababu yoyote ya kujieleza kwako wewe mtetezi wa uozo wa DHAIFU na magamba. Hunijui wala sina mpango wa kutaka unifahamu hunipunguzii wala kuniongezea chochote kile.

Le Mutuz mbona anasema anakujua mpaka mdingi wako!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom