SoC01 Fikra zangu juu ya wachora ramani wa kijiji chetu

Stories of Change - 2021 Competition

Niker

New Member
Sep 11, 2021
2
9
Mimi ni mwanakijiji kutoka kijiji kile kilicho staarabika, naam ndio ustaarabu huu ambao vijiji vingi kama si vyote juu ya ardhi hii ya ulimwengu huutumia, nakiri kwamba kijiji nitokacho husifiwa kuwa na watu wakarimu na wachukiao shari, kwao vita na malumbano ni jambo la kihistoria, lilitokea zamani sana, kiasi kwamba ni aghalabu kukutana na mwanakijiji alie shiriki vita ile akiwa bado na nguvu za miguu ama na mboni zinazo ona nuru na mwangaza wa jua,

Tuachane na sifa za kijiji changu, kuna jambo moja mimi kama mwanakijiji lina nisumbua sana fikrani mwangu, na jambo hilo ni hili, huku kwetu kijijini kuna utaratibu tumeuweka kuwa "kila baada ya misimu kumi ya mvua tunachagua mchora ramani mmoja ili atuchoree ramani ya kijiji chetu, na misimu hiyo kumi ikiisha tunachaguaa mchora ramani mwingine kwa misimu mingine kumi tena"

Sasa mgogoro huu wa kimawazo hauko juu ya utaratibu huu wa kijiji bali uko juu ya tabia za hawa wachora ramani. kwanza tangia utaratibu huu uanze wengine husema tumekuwa na wachora ramani sita na wengine wachora ramani watano, mimi sina hakika juu ya idadi yao na hilo si suala langu, mawazo yangu ni juu ya tabia zao watu hawa na mimi nafikiri hawatutendei vyema sisi wanakijiji tulio wachagua, kwa sababu kwanza pale tu tunapo wachagua wao hukoma kulima kama sisi, na kubakiza kazi moja tu mbele yao, kuchora ramani,

Ni jukumu la kijiji kuwalisha wao na familia zao, kuwa ezekea ma paa ya nyumba zao na kuweka mafuta kwenye chemli zao ili ndani kwao kuwe na mwanga kisha sisi huwakabidhi kinga za mikono yao ili wachore bila uoga kuwa mikono yao itachubuka ama kukatika, hakuna jambo mchora ramani atataka wana kijiji wasimpe, sisi huwapa kila kitu, japo sisi ni malofa tusio na kitu.

Licha ya juhudi kubwa za wana kijiji kutimiza matakwa ya wachora ramani wetu lakini hakuna mchora ramani hata mmoja alie wahi kukamilisha mchoro wake,wote huanza kutuambia kuwa wakikabidhiwa tu kinga za mikono yao wataanza kuchora kwanza zahanati na hospitali za mama,wake na dada zetu kujifungulia, kisha watachora shule ambazo watoto wetu husomea kisha watachora masoko ,mashamba,mito na mitaa ambayo vijana wetu huenda kufanya kazi, na baada ya kutuambia haya kila mmoja wetu hupiga makofi akijisemea "kwa mchoro huu hamna mwanakijiji atasahau juu ya adui zetu wakuu kijijini ujinga, maradhi na umasikini"

Kila mtu husema imani yetu mchora ramani huyu wa sasa ni tofauti na yule aliepita na huyu atakamilisha mchoro wetu na ramani yetu itakuwa ya mfano kwa vijiji vingine, lakini mambo huwa si mambo maana misimu kumi ya mvua huisha na hakuna nukta mpya katika mchoro wetu na bila aibu mchoraji hututupia kinga zetu za mikono tulizo mkabidhi akisema "mchoro huu ni mgumu sana nimejaribu wacha aje mwingine naamini huyu sasa hodari atakamilisha" wote husema hivyo wakisahau sisi ndio tulio waweka hapo tukawalisha, tukawanywesha tukiwapa kila watakacho huku dhiki na harufu mbaya ya ufukara ikitafuna mapafu yetu, eti "nimejaribu" na fikiri ili tukomeshe tabia hii mbaya kwa wachoraji wetu kwanza wachore ramani bila kinga ya mikono yao pili kama wakisema tena "nimejaribu" tukate kabisa mikono yao, pengine hivo mchoro wa ramani ya kijiji chetu utaisha.

ama laah! wao wataogopa kuja kuomba nafasi ya kuwa wachoraji na kama wakija basi waje na nia ya dhati na si kuomba nafasi hiyo ili waache kulima na wakome kutaabika juani pamoja nasi.
 
Aisee!!? Umeandika kitu kizuri lakin kitakuwa kigumu kupokelewa na wanakijiji maana wengi wao udanganywa.kwa visado vya mtama na mbegu za mahindi ili kuwapitisha wachora ramani na kuwa wapambe wao.
Ila lazma ifike mahara tukubari hii kaz lazma iogopwe na kuheshimiwa sio pawe mahari pa kukwepa majukumu ya kijiji wakati wa kilimo
 
Back
Top Bottom