Mwafrika,
Mkandara,
asante sana kwa hayo kweny bold. Watu wametamka sana kuhusu ujamaa na ubepari. Kuna swali hapa limeulizwa kuwa ni nchi ngapi leo duniani zinatawaliwa kibepari? Hakuna hata mmoja aliyetoa jibu.
Unajua kuna logic sana kwenye hii thread ya Mwanakijiji. Ingawa watu wengi wanadhani kuwa ujamaa ulikuwa mbovu na wanamlaumu Nyerere kwa hilo. Dunia ya leo inaongozwa na sera za kijamaa zaidi kuliko za kibepari.
Kumbuka hapa naongelea socialism na sio communism. Nyerere alitaka sera za ujamaa (socialism) na hili ndilo swali la Mwanakijiji kama hizi fikra za Nyerere zilizovutiwa zaidi kwenye utaifa na ujamaa zilikuwa na mafanikio na mapungufu gani?
Duuuh kama ulikuwepo akilini mwangu!.. Leo hii nilikuwa nikitazama documentary ya Castro - The untold story..kali kichiziiii.
Huwezi amini kuwa huyu jamaa aliwahi pokelewa Marekani kwa shangwe kubwa kuliko kiongozi yeyote duniani iwe wa ndani Marekani ama nje..yaani hadi leo hii anavunja record za mapokezi kwa viongozi wote waliomtangulia ama wa leo hii..Hakuna kiongozi duniani aliyewahi kuwavutia wananchi kila nchi aliyotembelea kama Castro yaani hakunaaaa!..
Na ndiye aliyeanzisha hili neno Socialism baada ya Marekani kudai sana kuwa yeye ni M-kommunist as a matter of fact alikuwa forced na Marekani yenyewe kuwa na ushirikiano na Russia baada ya kutoelewana na utawala wa Marekani kuhusu usafishaji wa mafuta (refinery) toka nchi nyingine. Zingwe lilianzia hapo...
Hakika kama alivyosema Rev. Kishoka kuwa wasomi wetu wanatunagusha sana sijui hii inatokana na elimu ya kuchujwa ama ndivyo tulivyo!..kweli kabisa sidhani kama kuna mtu anaweza kuja hapa na kuelezea nchi ngapi duniani zinaongozwa kibepari
Ujamaa kwa kila hali ni msisitizo wa umoja wa jamii yetu ktk kufikia malengo fulani.. Ujamaa ni nguzo ya ujenzi wa maneno kama Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.. Wayahudi wote ni wajamaa, wahindi, wazungu na kadhalika kwa sababu hawa watu wameweza ondoa takaba zao za makabila na kujenga ID moja kati yao ya Utaifa wao..Hata waislaam husema Jamaat Islam, wakimaanisha society yao. Je, Fikra za kujenga soziety moja iliyokwisha bomolewa na makabila ilikuwa wazo lisilokuwa na busara?
Hivyo fikra za mwalimu ndizo zilizojenga jamii moja ya Watanzania tukaondokana na identity ya makabila, Wakenya hadi leo wanajutia kushindwa kuunganisha makabila yao..Hao wanzungu wenzetu waliwahi jenga Ujamaa wao mika 200 iliyopita na ndio maana Msweden, Mtaliani, Mfaransa, Mjarumani, Mreno na kadhalika wote wanatambulika kama jamii moja hakuna mafungu mafungu,yet bado watu wnamlaumu mwalimu kwa sababu nje ya fikra za Ujamaa zilizoweka usiku ktk siasa za nchi za Kibepari ambao walitaka kuendela kutawala nchi zetu kiuchumi wakifikiria kuwa Uhuru wa bendera ulitosha kwa nchi zetu..that was abuse mkuu tena kubwa na sabau kubwa ya kudai uhuru huo..
Yap, somewhere tulifanya makosa aidha ktk maazui yetu ama kiutendaji lakini tupo nje ya ndoa ya mkoloni, tukiwa wasera tumewezesha vijana wetu hawa kupata elimu ambayo leo hii wanatumwagia hapa....
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba wengi wa vijana hawa hawafahamu hali aliyotuacha nayo Muingereza zaidi ya simulizi..Na hakika wafanyakazi majumbani mwa watu wanaokula bure na kulala bure baada ya kazi ngumu ya siku leo hii wanamwona JK mchawi kuweka kiwango cha malipo yao kuwa sheria kwa sababu wengi wanaachishwa kazi hizo za utumwa, kesho watakuja simulia watoto wao walivyokuwa na good time wakimtumikia Gabacholi.
Na mwisho hata neno kujitegemea.. hakuna nchi duniani isiyotaka Kujitegemea..hizi ndizo goals ambazo mwalimu alituachia lakini wabongo wanaziona wazimu tupu.. basi njooni na goals zenu.. utasikia mara sustainable economy... what a f....ikiwa huo uchumi hauwezi kujiendesha ila kwa kutegemea mikopo!..
je, kuna makosa gani kuuza fikra za kujitegemea hali mtu huyo huyo anataka nchi yetu isiendelee kuchukua mikopo toka nje?...nashindwa kuwaelewa wasomi wetu.